Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
Mwaka huu mwanzoni kabisa niliwaambia kuwa Jimbo la Hai ni mojawapo ya Jimbo ambalo litavuta hisia za Siasa za Tanzania, hapa hakuna kulala, ni mwendo wa mahuburi, ngumi na jino kwa jino. Hii Ni kutokana na umuhimu wa Jimbo hili kwa Upinzani na kwa CCM. Kwa Upinzani ndipo anapotokea Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni. Yaani hawatokubali inyeshe mvua liwake jua kupoteza eneo hili kwani itakuwa aibu ya mwaka. Kwa CCM hapa wanataka kumpiga mchungaji na Kondoo watawanyike, wanajua kabisa ukitaka kumuua nyoka gonga kichwani....
NGUVU YA CCM.
Mipango ya Ushindi wa CCM unaanzia Kichwani kwa Ole Lengai Sabaya, yaani CCM kwa ujumla wanategemea Ole Sabaya awasaidie kumngoa Mbowe pale Hai. Sabaya ndiye DC anayeongoza eneo gumu kuliko yote kati ya maDC wote nchini yaani kupewa jukumu la kuongoza eneo ambalo anatokea Kiongozi mkuu wa Upinzani sio kazi ndogo.
Jukumu la pili alilopewa au alilojipa Ni la kuhakikisha Mbowe hashindi Hai jukumu ambalo Ni zito ambalo hata Bashiru Ally Kakurwa hawezi kulibeba.
Sabaya anapambana kweli matokeo yake anaweza kuumia au akaishinda hii vita, lazima impact itakuwa aidha aumie au ashinde. Niliwahi kusema Kama hatopata usaidizi huyu kwa Jasusi Mbowe ataonekana hafai hata U DC. Pale CCM nani anaweza kuja kuwaongoza watu wanaomuita Mbowe kaka na akaeleweka? Mbowe Hai sio Mbunge tu Bali Ni kaka yao Kama wanavyomuita.
Nguvu ya Pili ya CCM Ni kuwa Sabaya anajitahidi Sana kufanya Siasa na watu wa Tambarare. Siasa maendeleo, siku za karibuni tunaona barabara zikichongwa, hospital ikijengwa nk. Sabaya anajitoa sana kuhakikisha image ya Serikali na Chama inaelewaka Hai. Aidha kwa kutumia mbinu nzuri au mipango Michafu lakini anapambana sana.
UDHAIFU WA CCM
Udhaifu CCM ni kwamba imejisahau, wanamtegemea Mkuu wa Wilaya afanye Kila kitu. Haitawezekana peke yake awaletee Ushindi halafu pia Ni kinyume cha Sheria mkuu wa Wilaya kufanya Siasa za wazi. Ndio maana hata waosema ni yeye ametuma watu wamshambulie Lisu hawana ushahidi wa moja kwa moja.
Udhaifu wa pili Ni kwamba CCM Haina network ambayo Mbowe anayo. Nitaelezea hapa chini nitakapokuwa naelezea nguvu za Mbowe.
Udhaifu wa tatu ambao hauonekani Ni Kifo cha Mzee Mengi. At least Mengi alikuwa Ni mmojawapo ya watu ambao walikuwa wanaweza kuwaambia Viongozi wa Dini Jambo wakalisikia, au hata jamii yake (Wachaga) jambo na wakamsikia.
Udhaifu wa nne Mkoa wa Kilimanjaro Ni Mkoa ambao hauna Agenda ya kuombea kura. Yaani hakuna Jimbo ambalo utapata kura kwa kuahidi hospital, Au umeme, au maji au barabara. Hivi Ni vitu ambavyo vipo toka uhuru. CCM Mara nyingi imekuwa ikitumia agenda hizi kuombea kura kwenye majimbo ya Kilimanjaro hizi sio agenda.
NGUVU YA CHADEMA.
Mbowe karelax kabisa sidhani hata Kama anawaza Sana kuhusu Ushindi wake. Nguvu kubwa waliyoanayo Chadema Ni aina ya mgombea waliyenaye. Mbowe kwa Sasa ndiye mhimili wa Siasa za Upinzani nchini.
Uimara wa Pili wa Chadema Hai Ni network ambayo Mbowe anayo. Mbowe anaungwa mkono na taasisi za Kidini lipo chini ya capert na ndio wanaompa nguvu sana, Mbowe anaungwa mkono na wafanyabiashara wengi toka Hai, Mbowe anaungwa mkono na hata baadhi ya wanaccm waliopo Hai.
Uimara wa tatu ni desturi na Mila za Kabila la wachaga. Kabila hili likishamuamini mtu sio rahisi kuwabadili. Hawaogopi kujilipua kwa kitu wanachokipenda. Mbowe anapendwa Sana na jamii yake. Hawa ndio wanaomuitaga Kaka si rahisi kuwabadilisha mtizamo, watakuchekea usoni lakini kwenye Sanduku la kura watakuadhibu tu. Ndio maana Kabila hili linaongoza katika kuendesha Siasa za Upinzani. Ndio Kabila linalotoa Viongozi wengi wa vyama vya Upinzani nchini. Hii Ni hulka yao kwa maana hiyo ukitaka kuwawin lazima Kwanza wakupende na wakuamini.
Uimara wa nne wa Mbowe Ni kulitawala jukwaa kwa Hoja. Ukimruhusu huyu mtu akupige kwa Hoja atakuua kabisa.
UDHAIFU WA MBOWE.
Udhaifu mkubwa wa brother Mbowe hakuna Jambo kubwa ambalo amelifanya kwenye Jimbo lake.
Pili eneo analotokea si rafiki Sana kwa Siasa za sasa. Mbowe anatokea eneo la milimani, Kuna tetesi kuwa eneo la tambarare ambalo Lina watu wengi nao wameanza kuwaza kutoa mtu wao kuwa Mbunge. Hii Ni kwa sababu eneo hili halijaendelea kwa Sana Kama eneo la Milimani hivyo Wana hasira.
Udhaifu wa Tatu Mbowe amejikita zaidi kwenye siasa za kitaifa na kusahau watu wake. Huu ni udhaifu kwa wabunge wengi wa Upinzani.
Swali ninalojiuliza Sabaya atauweza huu Mbuyu ambao umeshindikana Miaka na Miaka?
Ukitaka kumshinda Mbowe kirahisi tenganisha urafiki wake na Kanisa, tenganisha urafiki wake na wafanyabiashara wa Hai. Mwisho kabisa CCM ndani ya Mkoa na nje ya Mkoa wakitaka kushinda Hai wamsaidie Sabaya, peke yake hatoweza.
Ole Mushi
0712702602.