Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18

Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18

Karibia yote 6 ni mazito
Uzuri ni kuwa hayana dhamana kwa hiyo yupo yupo sana tu hapo mjini Kisongo. Tulipokuwa tunalalamikia sheria ya makosa haya kunyimwa dhamana hayawani wa CCM walitucheka,sasa imekula kwa kipenzi chao.
Screenshot_20210604-141546.jpg
 
Mwendazake aliwapa Sana Vijana nafasi ya Uongozi, bahati mbaya walikosa Mentor mzuri kuwafunza ethics za Utumishi na Uongozi wa Umma kwa ujumla labda kwa kuwa aliyewateua hakujali rule of law.

Hili liwe funzo kwa Vijana wote watakaoaminiwa na kupewa nafasi za uongozi, wawe wanatenda kwa kufata sheria na taratibu za Nchi.

Wao kama ni gali, linasoma Zero kilomita, hivyo wanasafari ndefu kulitumikia Taifa.

Wanaowateua Wamejiwekea Kinga ya Kutoshtakiwa, wao hawana.

Tafadhali Makinikeni
 
Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai Ole ngai Sabaya leo tar. 04.06 2021 amefikishwa mahakani akiwa na wenzake watano.

Sabaya peke yake amesomewa mashitaka sita likiwemo la Uhujumu uchumi na utakatishaji fedha pamoja na unyang'anyi kwa kutumia silaha.

Kesi imeahirishwa mpaka June 18 2021 na watuhumiwa wote wamerudishwa rumande kwani makosa hayo hayana dhamana.

Chanzo cha habari: Azam
View attachment 1808137
 
Back
Top Bottom