Ole Sabaya hata kama alikuwa na hatia lakini sio ya unyag'anyi wa kutumia silaha. Hakimu aliyehukumu hana weledi

Hukumu iliyotolewa haina weledi wa kisheria na endapo atakata rufaa hukumu itatupiliwa mbali kwa kuwa haijakidhi kwa sababu nyingi sana.

Hapa imethibitisha kwamba ndani ya CCM sio wapinzani wa kisiasa ndio waliokuwa wanamchukia JPM na wasaidizi wake watiifu kuliko hata shetani. Kwa msingi huu mahakama imetumika vibaya na ubaya huu hautakoma visasi vitaendelea mpaka chama cha CCM kitang'olewa madarakani pamoja na kwamba katiba na vyombo vya dola vinawalinda.

Wananchi wataing'oa CCM katika utawala ujao
 
Na mbowe amefanya ugaidi wake kwa maelekezo ya nani?
 
hv kwa mazingira ya kawaida ya kiutendaji mkuu wa wilaya fulani anaweza kwenda wilaya nyingine na kufanya zoezi la upekuzi wa magendo.ni nani hasa mwenye mamlaka ya kufanya upekuzi wa magendo.ni mkuu wa wilaya au ni jukumu la polisi?na kwanini u rule out kwa jambo ambalo huna uelewa nalo.nadhani sheria inampa mtu aliyetiwa hatiani nafasi ya kukata rufaa so let the law takes its own course.hatuna haja ya kuanza kulaumu au kumlaumu mtu hapa ila tunataka sheria zichukue mkondo kwa yoyote anayeenda kinyume.
 
Na mbowe amefanya ugaidi wake kwa maelekezo ya nani?
Mpuuzi wewe ameshahukumiwa??? Marekani yenyewe limeshindwa kuwatia hatiani magaidi wanaowashikilia huko Guantanamo bay. Itakuwa hao mapolisi wasiojua hata PGO
 
Na mbowe amefanya ugaidi wake kwa maelekezo ya nani?
Mbowe hakufanya ugaidi ila hujuma za kisiasa ili kujipatia nafasi ya yeye na chama chake kung'ara.

Ugaidi haubagui wa kumdhuru awe ndugu, rafiki, mzazi nk ili mradi lengo la kupeka ujumbe kwenda utawala husika kwamba hakuridhika au kuridhishwa na kutendewa isivyo
 
Kila siku mahakimu kama hawa wanaumbuka High Court.
Kwa taarifa yako ilitakiwa apigwe miaka 90, mawakili wake "wakamuombolezea" ndiyo maana miaka 30 kwa kila count imeenda kwa pamoja!
Pelekeni High Court mkapigwe 90!
 
Haendi kama mkuu wa wilaya, (he/she is empowered to do something different for a separate special assignment from the appointing authority, which doesn't require written document especially when it involves confidentiality handling of the matter being focussed to be accomplished within time bound)
 
Kwani kuvaa silaha kiuoni ndio kufanya uhalifu?
Jifunze sheria za Tanzania ndiyo utajua vizuri.

Kwa Bongo kuwa na silaha in public (including kisu) kwenye public inaweza kukupeleka ndani miaka 20!!
 
Wewe ni nani hata umkosoe hakimu mzoefu katika kazi yake ambayo ameizoea na mpaka kuizeekea!!??

Mawakili wa Sabaya wamesema hukumu iko sawa na wameshukuru, sasa huyu jamaa sijui yeye ni nani kutoa huu utopolo.
 

UTOPOLO....
 
Hata Sabaya kwenye utetezi wake hakuweza kuishawishi mahakama kuwa silaha zilikuwa ni kwa ajili ya kazi gani
 
Mawakili wa Sabaya wamesema hukumu iko sawa na wameshukuru, sasa huyu jamaa sijui yeye ni nani kutoa huu utopolo.
Tena wakili amekiri kuwa mahakama imemsamehe mteja wao maana alitakiwa kutumikia miaka 30 kwa kila kosa i.e. x3= 90 yrs lakini atatumikia vifungo hivyo kwa pamoja = 30 yrs.
 
Wewe ni nani hata umkosoe hakimu mzoefu katika kazi yake ambayo ameizoea na mpaka kuizeekea!!??
Yeye ni kada wa kijani asiyekuwa na taaluma yoyote. Shenzi sana hili li@idugunde
 
Jifunze sheria za Tanzania ndiyo utajua vizuri.

Kwa Bongo kuwa na silaha in public (including kisu) kwenye public inaweza kukupeleka ndani miaka 20!!
The matter in issue is armed robbery.
 
Eneo linapofanyika uporaji ikigundulika tu hata mmoja alikuwa(alikwenda) na kisu cha kukatia nyanya hiyo tayari ni "armed robbery" haijalishi ilitumika au haikutumika kikubwa ni uwepo wa silaha hiyo wakati wa uvamizi.
 
Kwani wewe siyo jaji? Kahukumu vizuri ilibufurahi
Na bado ya uhujumu uchumi, utacheka zaidi
 
Duh.."Confidentiality"= "Robbering assignment?"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…