Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,443
- 4,006
Hukumu iliyotolewa haina weledi wa kisheria na endapo atakata rufaa hukumu itatupiliwa mbali kwa kuwa haijakidhi kwa sababu nyingi sana.Nimesoma baadhi ya nukuu za hakimu Amworo anakiri kuwa Sabaya alikuwa na silaha eneo la tukio . Lakini hii sio sababu ya kudai kuwa alitenda unyang'anyi wa kutumia silaha.
Ili unyang'anyi wa kutumia silaha utimie lazima mtuhumiwa atishie kwa silaha, kutumia silaha na kisha kupora mali. Ukifuatilia kesi ya Sabaya utaona kuwa hakuna mahala hili linathibitishwa.
Lakini hata mashahidi wa mashitaka wanakiri kuwa Sababya na wenzake walikwenda na magari ya Serikali kufanya upekuzi juu ya magendo. Hapa ndipo utaona kama kuna walakini, maana hata mkuu wa wilaya ya Arusha wakati huo alifahamu.
My take; Mahakimu wanaofanya kazi kwa kukariri hawafai.
Hapa imethibitisha kwamba ndani ya CCM sio wapinzani wa kisiasa ndio waliokuwa wanamchukia JPM na wasaidizi wake watiifu kuliko hata shetani. Kwa msingi huu mahakama imetumika vibaya na ubaya huu hautakoma visasi vitaendelea mpaka chama cha CCM kitang'olewa madarakani pamoja na kwamba katiba na vyombo vya dola vinawalinda.
Wananchi wataing'oa CCM katika utawala ujao