Ole Sabaya kaa kimya uchunguzwe, acha kuchonganisha mamlaka za nchi. Utaingia matatizoni

Mimi hapa ndio huwa sielewi. Kabla na baada ya Ole Sabaya kusimamishwa mlikuwa mnajaza nyuzi humu za kumshambulia! Ila yeye au mtu akimtetea ni kosa sio? What's the meaning of natural justice!?
 
Kuna wengine wamefikia hatua ya kumwambia Rais Samia eti ajitafakari.
Halafu wakikumbushwa wanayemsema ni mh. Rais wanawaita wanaowakumbusha kuwa ni wapinzani. Kuna mmoja wao juzi alianzisha uzi wake humu akijitapa kwamba yeye amebobea kwenye maswala ya uongozi huku akidai mama hajakomaa bado
 
Unataka kumchonganisha raisi na watu wake wakati yeye mwenyewe karuhusu uhuru wa habali?
Kwani sabaya akirukaruka kisha akatulia wewe unaona raisi ana shida gani nae?
Nyie ndo.wachonganishi,
 
... mtu mwenyewe alishakutwa na kitambulisho fake cha tiss lakini bado akateuliwa na kuendelea kudumu katika nafasi ya u-dc. Mamlaka ya uteuzi tuieleweje?
 
Mimi bado nina mashaka naye kuwa ni Mtu wa Kitengo (bado kile kitambulisho alichoshikwa nacho cha kufoji cha TISS mwaka fulani) harafu akaachiwa bado napata mashaka!
Mambo yataishia uchunguzi bado unaendelea.
 
Mwigullu alipotumbuliwa na Maghufuli alikaa kimya,, na badala yake akaanza kummwagia sifa.
Mwishoe Mwigullu kalamba uwaziri tena.
Kimya ni kizuri sana.
 
The flavor of tit for tat principle is very sweet, kama kweli alitenda hizo vitu I pray that he be prosecuted immediately and I will rejoice in his regret and pains! πŸ˜πŸ˜πŸ˜ŽπŸ‘Œ
 
Uchunguzi huru ukifanyika Sabaya hachomoki
 
Kuna wengine wamefikia hatua ya kumwambia Rais Samia eti ajitafakari.

Maajabu makubwa haya, nimeshangaa sana kajitu kanadhubutu kutoa kauli ya namna hii "JITAFAKARI" kwenye mamlaka ya juu kabisa ya nchi! Wameharibu kabisa!

Hata kama mh Rais alikuwa na mpango wa kusamehe hii kauli ni kudharau na kushusha mamlaka ya nchi! Sina uhakika kwa kauli kama hii mama ataacha kumchukulia hatua dhabiti!

Sabaya angekuwa na akili angeacha kutengeneza haya makundi ya kumtetea kwenye mitandao ya jamii! Angetulia kwa busara hili wimbi lipite!

Hakuna asiyefahamu uovu alioutenda kwa watu! Ameumiza watu wengi sana!
 
Ndugu yangu nikurekebishe kidogo sabaya hapaswi kuchunguzwa sababu ushahidi wa ujambazi wake upo wazi na hakimu atakayemshughulikia hatapata tabu. Yeye mwenyewe anajua jela inamuhusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…