Oman: Rais Samia ataka kuwepo Maritime transport ya kusafirishia Wanyama wakiwa hai kutoka Tanzania kwenda Oman

Tatizo ni marehemu kumpendekeza huyu "Bibi" kuwa mgombea mwenza wake mwaka 2015.
Marehemu katuachia balaa kubwa sana.
 

Mkuu tatizo la muafrika ni kujidhalilisha sana yaani utajiri wetu ila tukikutana nao utaona tunavyojidhalilisha mara kuweka mikono nyuma kwa unyenyekevu, mara wengine wakawapokee mikoba Yaani tafrani tupu

Viongozi hawajiamini kabisa
Mali zetu badala ya kuwapangia tunavyotaka Sisi au kuweka bei juu kila kitu

Mbona wao walimdindia mzungu na kusaini mikataba ya mafuta ya miaka 50 ila leo Oman mafuta 100% ni ya kwao bila ubia na mzungu maana yake mkataba umeisha na sasa wanakula Neema

Ndio maana unaona Oman inatamba sasa ingawa walikuwa masikini wa mwisho katika nchi za Gulf

Hebu angalia Rais wetu mmoja alipokaribishwa Oman zamani kidogo yaani Rais anashangaa makochi ya mfalme na chandeliers za juu
Unamuona kabisa anavyozubaa daa

Kama kweli tungekuwa na nia ya wananchi kuwa na maisha ya raha tuache ubinafsi na kujitajirisha baadhi ya watu

Unashangaa mtu ana nyumba 40 za nini kwani akila kama mbuzi vibaya
Yeye mpaka ale kama Punda?

Nilihadithiwa na babu yangu akasema unajua tofauti ya ulaji wa Mbuzi na Punda?

Mbuzi anakula huku akiachia na ya kesho
Kwa hiyo atakula juu juu tu ili na kesho arudi tena

Punda sasa (viongozi) anakula mpaka mizizi na yale meno yake makubwa [emoji23]
Hajali kesho atakula nini

Ndio maana punda utamkuta anaishi sehemu za jangwa jangwa tu Hakuna majani ya kutosha maana Alisha kula mpaka mizizi

Sisi ndio tuko kama punda na tusipobadilika tuajikuta hatuna kitu

Wewe utabanwa ila wao watapewa kila kitu
Kwanini ?
Udhalili wetu
 
Akili ni nyingi sana hizi.
 
USSHAMBA WA WATANZANIA UMEWAFANYA KUWA NA WOGA WA KILA KITU.
UJINGA PIA NAO UNACHANGIA.
HII HABARI YA UTUMWA ULE WA KALE HAIPO TENA DUNIANI,BALI SASA MASIKININDIO UNAOKUFANYA UBAKI KUWA MTUMWA
-TUMEKUWA WAOGA WA KUJICHANGANYA ,TUMEKUWA KAMA ''JOKA LA MDIMU''
 

Mkuu waafrika ni shida tupu
Hivi hao wanyama tumewatumia kwa lipi?

Kama India, Philippine , Malaysia na Bangladesh
Wametumia Nyati kwa kuwalimisha na Tembo wanavuta magogo
Nyani wanafukuza nguruwe na ndege kwenye mashamba yao

Haya kama hayana akili ya viwanda electronics Basi hata kumfunza Nyati alime wameshindwa
Hao wamefanya hivyo tangu enzi na enzi hata Egyptians pia

Sisi tumebaki maneno tu ooh Tembo wanaenda
What a shit hole
Tumefaidi nini na Mito yetu Maziwa na hata beaches zetu ni za kujisaidia tu
 
Upo sahihi boss, usisahau lakini Tz ni moja ya nchi yenye idadi kubwa ya mifugo Africa (Ukiondoa Sudan Kusini), kama kuuza mifugo ni njia ya kupanua biashara si mbaya.

Ila kuhimiza uwekezaji kwenye hiyo sekta hapa nchini (pamoja na uvuvi) ndio inafaa zaidi.
 
Mkuu msamehe bure
 
Job Ndugai alishasema, iko siku tutauzwa ndo tumeanza hivyo kuuzwa
 
Hii nchi ina wajinga wengi sana. Yaani Wanyama hai wanapeleka dhana ya TWIGA, SIJUI SIMBA aiseeee.

Jmn Watz wanyama hai inamaanisha MBUZI, KONDOO, NG'OMBE, KUKU nk.

Mbona huwa tunawaza negativity all the way.....
Ametoa list ya wanyama watao safilishwa?
 
USSHAMBA WA WATANZANIA UMEWAFANYA KUWA NA WOGA WA KILA KITU.
UJINGA PIA NAO UNACHANGIA.

Sawa kabisa, Lazima nchi yoyote duniani iwe na mentali ya kikoloni ndiyo itaendelea.

Haijalishi kuwa ni North Korea wataiba pembe za ndovu au kutumia wezi wa mitandaoni , Russia pamoja na siasa zake za kikomunisti nao wana mentaliti ya kikoloni wa aina yake hata China yenye chama cha kikomunisti cha China CCP vilevile wanaendeleza ukoloni na ubeberu wa aina fulani kumiliki masoko, kutoa milungula ya fedha kupitia misaada kwa nchi rafiki lakini nyuma ya harakati zote hizo ni kutaka kujinufaisha kama Taifa .


Ni nchi za kiafrika ndiyo vinadanganywa kuwa kuendeleza ukoloni wa kiaina nje ya mipaka yake kuwa ni jambo baya, wakati nchi zote ikiwemo Iran, Israel n.k zinaendekeza ukoloni, ubeberu wa kiaina kwa manufaa ya nchi zao nje ya mipaka yake .
 
Namkumbuka ndugai,old is gold!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…