Oman: Rais Samia ataka kuwepo Maritime transport ya kusafirishia Wanyama wakiwa hai kutoka Tanzania kwenda Oman

Oman: Rais Samia ataka kuwepo Maritime transport ya kusafirishia Wanyama wakiwa hai kutoka Tanzania kwenda Oman

Tatizo ni marehemu kumpendekeza huyu "Bibi" kuwa mgombea mwenza wake mwaka 2015.
Marehemu katuachia balaa kubwa sana.
 
Sio mbaya tatizo letu udhibiti hatuna,ndio maana unaona malalamiko maana yalishatokea huko nyuma,wanyama wanasafirishwa ambao hawapo hata hawaruhusiwi,hilo la kufuga sawa maana hata sisi tuna shida ya kula nyama ya porini,zilianzishwa bucha za nyama pori kila ukienda unaambiwa nyama hakuna,jamaa wanasema masharti magumu,lakini utashangaa huko uarabuni wanyama wataenda kirahisi mno

Mkuu tatizo la muafrika ni kujidhalilisha sana yaani utajiri wetu ila tukikutana nao utaona tunavyojidhalilisha mara kuweka mikono nyuma kwa unyenyekevu, mara wengine wakawapokee mikoba Yaani tafrani tupu

Viongozi hawajiamini kabisa
Mali zetu badala ya kuwapangia tunavyotaka Sisi au kuweka bei juu kila kitu

Mbona wao walimdindia mzungu na kusaini mikataba ya mafuta ya miaka 50 ila leo Oman mafuta 100% ni ya kwao bila ubia na mzungu maana yake mkataba umeisha na sasa wanakula Neema

Ndio maana unaona Oman inatamba sasa ingawa walikuwa masikini wa mwisho katika nchi za Gulf

Hebu angalia Rais wetu mmoja alipokaribishwa Oman zamani kidogo yaani Rais anashangaa makochi ya mfalme na chandeliers za juu
Unamuona kabisa anavyozubaa daa

Kama kweli tungekuwa na nia ya wananchi kuwa na maisha ya raha tuache ubinafsi na kujitajirisha baadhi ya watu

Unashangaa mtu ana nyumba 40 za nini kwani akila kama mbuzi vibaya
Yeye mpaka ale kama Punda?

Nilihadithiwa na babu yangu akasema unajua tofauti ya ulaji wa Mbuzi na Punda?

Mbuzi anakula huku akiachia na ya kesho
Kwa hiyo atakula juu juu tu ili na kesho arudi tena

Punda sasa (viongozi) anakula mpaka mizizi na yale meno yake makubwa [emoji23]
Hajali kesho atakula nini

Ndio maana punda utamkuta anaishi sehemu za jangwa jangwa tu Hakuna majani ya kutosha maana Alisha kula mpaka mizizi

Sisi ndio tuko kama punda na tusipobadilika tuajikuta hatuna kitu

Wewe utabanwa ila wao watapewa kila kitu
Kwanini ?
Udhalili wetu
 
Kama Somalia na Australia wanapeleka Ng'ombe na Mbuzi wa kutosha huko Oman, Oman anatafuta nini tena kutoka Tanzania?

Hivi unadhani Oman wana uhaba wa Mbuzi au Ng'ombe mpaka waje kuwasaka Tanzania?

Hivi Oman wanaposema wanataka kununua wanyama hai kutoka Tanzania unadhani wanataka Ng'ombe na Mbuzi? Ili wakawafuge au kuwachinja?


Jiongeze ndugu.
Akili ni nyingi sana hizi.
 
USSHAMBA WA WATANZANIA UMEWAFANYA KUWA NA WOGA WA KILA KITU.
UJINGA PIA NAO UNACHANGIA.
HII HABARI YA UTUMWA ULE WA KALE HAIPO TENA DUNIANI,BALI SASA MASIKININDIO UNAOKUFANYA UBAKI KUWA MTUMWA
-TUMEKUWA WAOGA WA KUJICHANGANYA ,TUMEKUWA KAMA ''JOKA LA MDIMU''
 
Kuna watu wanajiandikia tu humu ili mradi na yeye awe yumo!

Watu wanapewa fursa wanaanza matusi na kashfa! Sijui mara Twiga wetu,mara Tembo wetu! Na hizi fikra zimekuwepo miaka na miaka! Bila kubadili hizi mentality tutaendelea kulalamika maisha magumu milele na milele.

Mkuu waafrika ni shida tupu
Hivi hao wanyama tumewatumia kwa lipi?

Kama India, Philippine , Malaysia na Bangladesh
Wametumia Nyati kwa kuwalimisha na Tembo wanavuta magogo
Nyani wanafukuza nguruwe na ndege kwenye mashamba yao

Haya kama hayana akili ya viwanda electronics Basi hata kumfunza Nyati alime wameshindwa
Hao wamefanya hivyo tangu enzi na enzi hata Egyptians pia

Sisi tumebaki maneno tu ooh Tembo wanaenda
What a shit hole
Tumefaidi nini na Mito yetu Maziwa na hata beaches zetu ni za kujisaidia tu
 
Wanyama hai sawa..ila tutapigwa sana...mana watachukua faida yote kutoka kwenye kwato..pembe..ngozi na offals.

Sikubaliani nalo hili.

Wauziwe meat and meat products sio myama hai.

Haya mambo JPM aliyakataa ya kuuza malighafi...hatuwezi kuza viwanda vya ndani na raia wetu watakosa kazi na ajira.

#MaendeleoHayanaChama
Upo sahihi boss, usisahau lakini Tz ni moja ya nchi yenye idadi kubwa ya mifugo Africa (Ukiondoa Sudan Kusini), kama kuuza mifugo ni njia ya kupanua biashara si mbaya.

Ila kuhimiza uwekezaji kwenye hiyo sekta hapa nchini (pamoja na uvuvi) ndio inafaa zaidi.
 
Tuhamasishe viwanda vijengwe hapa, ng'ombe achnjwe pale vingunguti, ngozi ipelekwe kwenye kiwanda cha Rostam pale morogoro. Ajira zitapatikana hapa, serikali itapata kodi nk.

Wanyama wakienda wazima, kuna kipato tutakikosa, serikali inatakiwa ishauriwe kwa hekima waelewe. Sasa nyinyi vijana wa kulipwa pesa kdg na kumsifia mama siku nzima upo online kwenye mada za kumtetea mama, huna unalojua zaidi ya matusi.

Vijana kama wewe ni bora sperms zingepotelea chooni, kwani mpo duniani kua "ass kissers" eti leo unamtukana hadi Mwalimu Nyerere... Dahhh.
Mkuu msamehe bure
 
Salaam Wakuu,

Rais Samia katika Kongamano la Wafanyabiashara wa Oman na Tanzania, amesema kuna umuhimu Mkubwa wa kuangalia Usafiri wa Majini akimanisha Meli yenye Uwezo wa kusafirisha Wanyama wakiwa hai kutoka Tanzania kwenda Oman.

Watu hapa wasifikilie Wanyama Pori tu, Bali ni Habari njema kwa Wafugaji wa Tanzania kwani sasa Wataanza Kusafirisha Ng'ombe, Sungura, Kitimoto, Mbuzi, Swala, Twiga nk hasa kwa wawindaji wenye Vitaru.

Pia kazungumzia kuhusu meli za Kuvua samaki Bahari Kuu.

Amewataka Oman waje kuwekeza Tanzania ardhi ipo ya kutosha.

Watanzania Kaeni Mkao wa kula.

............................................................................


Rais Samia akiwa kwenye kongamano Kiuchumi nchini Oman, amesema kuwepo kwa vyombo vya usafirishaji vya majini kusafirisha wanyama walio hai na bidhaa mbalimbali kwenda Oman kutaboresha biashara kati ya pande hizo mbili

Pia amegusia japokuwa tuna makubwa ya kuvua, kwa sasa hamna uvuvi wenye tija kwa taifa, amesema “kuna nchi zinakuja Tanzania kuvua na hatuwezi kuwafukuza kwa sababu hatuna vifaa, hivyo wanavua na kuondoka, hili ni eneo lingine ambalo tunaweza kushirikiana kwa pamoja”

Amesema kuwa kongamano la mwaka huu limekusudia kuangazia namna Tanzania itashirikiana na Oman katika sekta za utalii, kilimo, Uzalishaji (viwanda) mifugo na uvuvi na usafirishaji wa majini.
Job Ndugai alishasema, iko siku tutauzwa ndo tumeanza hivyo kuuzwa
 
Hii nchi ina wajinga wengi sana. Yaani Wanyama hai wanapeleka dhana ya TWIGA, SIJUI SIMBA aiseeee.

Jmn Watz wanyama hai inamaanisha MBUZI, KONDOO, NG'OMBE, KUKU nk.

Mbona huwa tunawaza negativity all the way.....
Ametoa list ya wanyama watao safilishwa?
 
USSHAMBA WA WATANZANIA UMEWAFANYA KUWA NA WOGA WA KILA KITU.
UJINGA PIA NAO UNACHANGIA.

Sawa kabisa, Lazima nchi yoyote duniani iwe na mentali ya kikoloni ndiyo itaendelea.

Haijalishi kuwa ni North Korea wataiba pembe za ndovu au kutumia wezi wa mitandaoni , Russia pamoja na siasa zake za kikomunisti nao wana mentaliti ya kikoloni wa aina yake hata China yenye chama cha kikomunisti cha China CCP vilevile wanaendeleza ukoloni na ubeberu wa aina fulani kumiliki masoko, kutoa milungula ya fedha kupitia misaada kwa nchi rafiki lakini nyuma ya harakati zote hizo ni kutaka kujinufaisha kama Taifa .


Ni nchi za kiafrika ndiyo vinadanganywa kuwa kuendeleza ukoloni wa kiaina nje ya mipaka yake kuwa ni jambo baya, wakati nchi zote ikiwemo Iran, Israel n.k zinaendekeza ukoloni, ubeberu wa kiaina kwa manufaa ya nchi zao nje ya mipaka yake .
 
Back
Top Bottom