Said Stuard Shily
JF-Expert Member
- Jul 18, 2017
- 2,396
- 2,108
Leo eneo la Kinyerezi kwenye kampeni za Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi ambaye ndie Rais Mtarajiwa hilo halina ubishi, Kumbilamoto amemuomba msamaha Dkt. Magufuli kuwa walifanya makosa makubwa sana akiwa Meya wa Ilala kupitia CHADEMA kuhujumu miradi ya Serikali ili kuonesha Rais Magufuli hawezi kutatua matatizo ya wananchi, hivyo amesema CHADEMA ni Chama kinachozungukwa na watu wasiolitakia Taifa letu mema hasa sisi wanyonge.
===
Aliyekuwa Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala, ambaye pia alikuwa ni Diwani wa Vingunguti, Omar S. Kumbilamoto amumomba radhi Dkt. Magufuli leo katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kinyerezi
Kumbilamoto ameomba radhi kwa kuwa alikuwa Upinzani katika Umoja uliojulikana kama UKAWA katika Uchaguzi Mkuu wa 2015
Kwasababu hiyo ameomba radhi kwa Rais, CCM, wananchi na viongozi wa Ilala kwa mabaya waliowafanyia kipindi yuko upinzani
Ameyasema hayo alipopewa muda wa kuzungumza kwenye mkutano wa kampeni
Nukuu:
Kabla sijaongea, nichukue fursa hii kwanza kukuomba msamaha wewe binafsi, Chama cha Mapinduzi na wananchi kwa ujumla kwa mabaya tuliyowafanyia wakati tupo upinzani. Naomba sana unisamehe Mheshimiwa Mwenyekiti.
Mheshimiwa Rais, katika manispaa yetu uliingiza miradi ya Soko la Kisutu, Machinjio ya Vinginguti na Hospitali ya Kivule.
Ukaingiza bilioni 17.6 ujenzi wa daraja la Ulongoni, bilioni 4.3 ujenzi wa Daraja la Zimbili na uliingiza takribani bilioni 115 ya barabara za BMDP.
Nisikufiche Mheshimiwa Rais, miradi hii ilikwama kwa maelekezo kwamba tukifanya sisi kama ukawa tutakupa kiki wewe Rais Magufuli. Ilibidi na sisi tutii, tukakuhujumu. Kwahiyo naomba unisamehe sana.
Baada ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala sisi kurudi, miradi hii yote tukaikwamua na hivi sasa ipo kwenye maendelezo na mingine imeshakamilika.
Lakini kubwa zaidi Rais kilichotuuma sisi tukawa upinzani kulikuwa na mikopo ya Asilimia 10 ambapo mikopo hii ilikuwa haitoki na wala wananchi hawaijui – 2010 hadi 2015. Ulipoingia ukaagiza itoke hii mikopo takribani bilioni 10 na hapa nimpongeze Mkurugenzi , pesa hizi zimewafikia wananchi wa kawaida – mama lishe na bodaboda.