Ombi la kusitisha mashambulizi kwa muda wa masaa 72 juu ya sakata la Tanganyika kuuzwa kwa DP World

Ombi la kusitisha mashambulizi kwa muda wa masaa 72 juu ya sakata la Tanganyika kuuzwa kwa DP World

Imefika wakati najiuliza, hivi angekuwa ndio Mama yangu anapigwa spana namna hii non- stop ningejisikiaje? Nimejikuta namuonea huruma tu huyu mama, maana anaweza kuwa mama yangu mzazi kabisa.

Imefika wakati najiuliza, is she being ‘black mailed’?, kwamba she has no choice? Au amekuwa -threatened usalama wake endapo ataenda kinyume na matakwa yao? Sijui na sina hakika, ila nawaza sana, huyu mama yetu anafaidika na kipi kikubwa hasa katika hili? Kama ni hongo, mbona angeweza kukwapua tu tozo za miamala kwa muda wa mwezi mmoja na zingemtosha kuishi kama malkia maisha yake yote? Kulikuwa na haja gani ya kutufanyia hivi waTanganyika? Hivi ilikuwa ni lazima kutuuza?!

Natoa ombi kwa WaTanganyika wote, kusitisha mashambulizi kwa muda wa masaa 72 ili kumpa mama yetu nafasi ya kujitathmini.

Maana imefika wakati anaongea kama anataka kulia, kuna nini nyuma ya pazia?
Pls don't bring emotions into this matter,her womanhood,has nothing to do with her being attached,criticised,
We are attaching the presidency(,ofisi ya Raisi)whoever would have been occupiying the ofisi,would have been facing the same,barrage of critical words,his or her gender not withstanding.
Umama wake pembeni,tunajua ni mama,shangazi,bibi,mke,wa Mtu,ila yupo ikulu,maamuzi yake yana madhara makubwa,
Kama ni swala la msosi Gani anampikia mumewe,au nyimbo Gani anawaimbia wajukuu zake,we don't give a shit,and don't care,ila nyimbo kuhusu rasilimali zetu na urithi wa vizazi vijavyo,hakuna rangi hataacha ona,tutamuonyesha kila rangi.if she can't withstand the heat,she should vacate the office
 
hata sijui unataka uambiwe mara ngapi, na kwa namna gani ili uache kuhamishia lawma kwa watu wengine na kuacha mhusika mwenyewe!

Wewe hata huoni maandalizi aliyofanya yeye mwenyewe kwa kazi aliyotaka kuitimiza?

Hao washauri, akina Mbarawa, Katibu Mkuu wa wizara, n.k., wewe unadhani waliwekwa kwenye nafasi hizo kwa bahati mbaya?

Kama hakusoma "100% kama unavyodai wewe; kama anajua anao udhaifu huo wa kutokuwa makini na kusoma hiyo mikataba, si hapo udhaifu huo ndio ungemfanya ateue watu makini kwenye nafasi husika ili waisome hiyo mikataba na kumpa taarifa kamili?

Mkuu 'Jidu', usidhani ninakukomalia kwa jambo lililo dogo hapa. Huyu siyo mtu wa kumkingia kifua kwa njia yoyote ile.

Huyu ni mtu anayelihujumu taifa letu kwa maksudi mazima kabisa.
Mkuu ningekubsliana na wewe, lakini mimi nimeenda kwenye udhaifu wa kibinadamu, uswahili, laiszes faire, kukosa umakini, hili ndilo linamuangusha mama.

Kwa makusudi nimezitaja Taasisi ya Urais, Usalama wa Taifa, Katibu Mkuu Kiongozi na Mwanasheria Mkuu.
Je, hawa wamefanya kazi yao?

Ndiyo maana nasema kama waliafiki mkataba kama ulivyo, basi tuna tatizo kubwa sana.

Tatizo liko bordering katika kuuza sovereighnity, uhuru wetu.
Na ndio maana watu wamekuja juu.

Suala hilo ni baya sana, mithili ya UHAINI.
 
Kwa makusudi nimezitaja Taasisi ya Urais, Usalama wa Taifa, Katibu Mkuu Kiongozi na Mwanasheria Mkuu.
Je, hawa wamefanya kazi yao?
Wafanyeje kazi zao wakati anayewateua wamekwishajua nia yake ni ipi katika kazi hiyo.

Pia unakosea sasa kumfikiria Samia kuwa na sifa hizo ulizotaja hapo.
Huyu ni "manipulator" mkubwa sana. Hii ndiyo hatari iliyotaka kumnasa Mbowe, sasa sijui kama huyo Mbowe shatoka kwenye hatari hiyo aliyokuwa kategeshewa.
 
Mimi sikupumua kwa furaha alivyoingia mama yenu, kauli na vitendo havikunivutia kwa chochote, zaidi niliona kiti kimebaki wazi na ndege inajiendea tu bila rubani, matokeo sasa ndio tunayaona!
 
Hakuna anayemchukia mama Samia.
Alianza vizuri sana kwa kuanza kusahihisha madudu ya Magufuli.
Sote tulipumua kwa furaha kuwa jinamizi la ukandamizi sasa limepotelea mbali.

Kwa kauli na vitendo mama Samia alitufurahisha.

Tatizo kubwa ni kutokuwa makini, mifano ipo mingi ila hili suala la DP World limemuumbua vibaya.

Ninaweza kusema 100% kuwa hiyo mikataba hakuisoma.
Hapo ndio nakuwa na wasiwasi na Taasisi ya Urais ambamo Usalama wa Taifa wamo, Katibu Mkuu Kiongozi yumo, na hata kwa pembeni Mwanasheria Mkuu yupo.
Hayo madudu hayakuoekanaje?
Na hapo ndo nadiriki kusema tuna laiszes faire, uswahili mwingi huko juu kiuongozi.

Kwa makosa tuliyoyaona kulaumiwa ni lazima, lakini busara ni kuyasahihisha!
Mm sikupumua kwa furaha alipoingia, kauli na vitendo vyake havikunifurahisha kwa chochote, zaidi nilitambua dhahiri kiti kimebaki wazi, na fikra zangu hazikunidanganya maana matokeo ndio sasa tunayaona..
 
Hakuna anayemchukia mama Samia.
Alianza vizuri sana kwa kuanza kusahihisha madudu ya Magufuli.
Sote tulipumua kwa furaha kuwa jinamizi la ukandamizi sasa limepotelea mbali.

Kwa kauli na vitendo mama Samia alitufurahisha.

Tatizo kubwa ni kutokuwa makini, mifano ipo mingi ila hili suala la DP World limemuumbua vibaya.

Ninaweza kusema 100% kuwa hiyo mikataba hakuisoma.
Hapo ndio nakuwa na wasiwasi na Taasisi ya Urais ambamo Usalama wa Taifa wamo, Katibu Mkuu Kiongozi yumo, na hata kwa pembeni Mwanasheria Mkuu yupo.
Hayo madudu hayakuoekanaje?
Na hapo ndo nadiriki kusema tuna laiszes faire, uswahili mwingi huko juu kiuongozi.

Kwa makosa tuliyoyaona kulaumiwa ni lazima, lakini busara ni kuyasahihisha!
Mimi na wenye mawazo kama mimi, tunatambua kuwa Utawala uliopita ulikuwa na nia ya dhati kuongoza nchi hii kuliko Awamu zote. Hoja hii haina maana kuwa Utawala huo haukuwa na mapungufu, la hasha. Moja ya mapungufu ni masuala ya kisiasa ambapo ulibana uhuru wa wanasiasa kutimiza wajibu wao. Lakini, kwa ulinzi na usimamizi wa rasilimali za taifa na uwajibika, ulifanya vizuri
 
Mwenzako hata hajali,anakula upepo wa feri..hata hivyo ones huruma vizazi vinavyokuja sio wa sasa..our fate was already sealed by the actions of our forebearers
 
Acha uongo na ujinga wewe,Acha ubaguzi kwa misingi ya aina yoyote Ile,Hakuna wa kuuza Taifa letu Wala Rasilimali zetu zilizopo ndani ya ardhi yetu kwa maslahi yake binafsi.mali na Rasilimali zetu za asili zipo katika mikono salama ya mzalendo wa kweli na aliyetukuka kiuadilifu mh Dr mama Samia suluhu Hassani,ndio maana watanzania Ni wenye utulivu , uvumilivu na subira kwa kuwa Wana Imani kubwa Sana na Rais wetu.
 
Page zote zina sahihi yake kwa chini
Uwe unaelewa hata Kama akili yako Ni ndogo ,mikataba bado haijaingiwa na kufanyika,kilichopo kwa Sasa Ni Ile Nia ya kutaka kushirikiana ,kwa hiyo mambo ya mikataba na namna sisi Kama Taifa na wenye Mali tutakavyo faidika yatakuja baadaye ,ambapo huko tutaona habari za ukomo wa mkataba,maeneo ya uwekezaji,mashariti ya mkataba,namna ya usuluhishi wa migogoro,utatuzi wa migogoro ya kimslahi baina ya pande mbili, mahali pa kutatulia migogoro, Tutapata Nini kwa wakati gani kwa kias gani Cha fedha n.k.
 
Hayo madudu sio kuwa hayakuonekana, ni makusudi wafikie malengo yao...mafisadi yanayoizunguka meza ya rais...RA na Msoga
Acha uongo na uzushi wako wa kijinga jinga usio na misingi ya hoja ya aina yoyote Ile zaidi ya kuleta umbea wa mitaani
 
Unaweza kumchukulia kama mama, sio wewe peke yako, hata sisi wengine wote. Mama siku zote kwa muonekano, haiba, umuhimu wake kwenye jamii, naweza kusema ni Miungu wetu hapa ulimwenguni.

Ndio, ni miungu yetu hapa ulimwenguni kwasababu, ukiachilia mbali ile mbegu ya baba iliyofanya mimba ikatungwa, lakini baada ya hapo kuanzia ukuaji wa mimba kwenye stage zote, magonjwa ya hapa na pale yanayoambatana nayo, mpaka uchungu siku ya kujifungua, baada ya hapo malezi mpaka tunakua, hakika hayupo wa kufananishwa na mama.

Tatizo dogo linalomkuta mama yetu huyu, ni ile nafasi aliyoshikilia, tumeiweka Tanganyika yetu mikononi mwake, kisheria, na kiutaratibu, kumkosoa sio kwamba hatumpendi, hapana, tunamuonesha njia, kwasababu akiyumba yeye, Tanganyika yetu, na thamani ya utu wetu, ndani ya mipaka yetu, itapotea, hivyo ni vyema kwake kutulindia heshima ya Tanganyika yetu, na utu wetu, ili nasi tuendelee kumlindia heshima yake kama Mama kiongozi wa nchi yetu.

Asipuuze anapoambiwa, afungue masikio yake atusikie, hii Tanganyika yetu tunaipenda sana, ndio alpha na omega, hatuna pengine pakukimbilia, ndio maana tunapoona na kuhisi thamani ya ardhi yetu tuliyopewa na Mungu inaelekea kupewa wageni, tunaogopa, tunashtuka, ndio maana hatuchoki kupiga kelele kila sekunde, kila saa, kila dakika, kila siku, kila wiki, hata miezi, tutaililia Tanganyika yetu kwa sauti kuu bila kuchoka.
 
Huu ujambawazi wa ccm Tz sasa umetisha!
Tukikaa kimya wanaweza kuanza kuuza hadi mikoa! serious msicheke!
Ccm na hawa viongozi wake ni kama wanajua wanakufa kesho ndio maana ya ushetani huu!
 
Kelele za Chura hazimzuii Ngombe kunywa maji...., Nadhani maneno haya hata JK aliwahi kuyatamka....
 
Imefika wakati najiuliza, hivi angekuwa ndio Mama yangu anapigwa spana namna hii non- stop ningejisikiaje? Nimejikuta namuonea huruma tu huyu mama, maana anaweza kuwa mama yangu mzazi kabisa.

Imefika wakati najiuliza, is she being ‘black mailed’?, kwamba she has no choice? Au amekuwa -threatened usalama wake endapo ataenda kinyume na matakwa yao? Sijui na sina hakika, ila nawaza sana, huyu mama yetu anafaidika na kipi kikubwa hasa katika hili? Kama ni hongo, mbona angeweza kukwapua tu tozo za miamala kwa muda wa mwezi mmoja na zingemtosha kuishi kama malkia maisha yake yote? Kulikuwa na haja gani ya kutufanyia hivi waTanganyika? Hivi ilikuwa ni lazima kutuuza?!

Natoa ombi kwa WaTanganyika wote, kusitisha mashambulizi kwa muda wa masaa 72 ili kumpa mama yetu nafasi ya kujitathmini.

Maana imefika wakati anaongea kama anataka kulia, kuna nini nyuma ya pazia?
Mimi sina huruma na wapigaji, mashambulizi yaendelee mpaka ajiuzulu.
 
Back
Top Bottom