kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Mpira ni taasisi yenye lugha yake, taratibu zake na sheria zake. Mpira ndio taasisi inayoruhusu mtu kuuzwa kwa mkataba fulani wa muda fulani kwa kiasi fulani. Hii inafanyika kwakuwa:
1. kila timu inataka wachezaji wazuri kuliko timu pinzani.
2. Wachezaji wazuri sio wengi sana kwenye jamii.
3. Kila timu inataka kushinda kwa gharama yoyote, haipendi kufungwa.
4. Mpira ni pesa, hivyo wachezaji ni pesa (bidhaa) pia.
Sababu hizi ndio zilizosababisha mpira ukawa na taasisi zake maalumu chini ya FIFA ambazo haziingiliwi na serikali na wanasiasa kwenye uendeshaji wake.
Ombi la Rais lazima liheshimiwe na Yanga na lazima litekelezwe kwa kufuata lugha na kanuni za kimpira kwakuwa utekelezaji wake utaacha alama, njia na utaratibu ambao utatumika kutatua matatizo mengine yajayo nchini yatayofanana na hili la Fei Toto na Yanga.
Ukweli ni kwamba Fei Toto:
1. Anatakiwa na timu nyingine ambayo haitakii kujitokeza wazi. Hiki ni kinyume.
2. Fei Toto ana mkataba mbichi na Yanga.
3. Fei Toto anataka kuvunja mkataba kwa unilaterally, kinyume na taratibu za mpira.
Swali hapa ni njia itakayotumiwa na Yanga kumaliza mgogoro na katoto Fei Toto itatoa SoMo gani kwa wachezaji wengine Yanga na timu nyingine nchini?
Je, njia hiyo inaweza kutumiwa tena kumaliza mgogoro mwingine unaofanana na huo kama ukijitokeza?
Soma:
- Rais Samia: Sifurahii Mgogoro wa Yanga na Feitoto. Nataka umalizike