Nimeona wapambe wa fei toto wakifuraishwa sana na kauli ya Rais Samia juu ya kuiomba Yanga kumalizana Fei.
Nimeona baadhi ya wasioelewa wala kutambua hili jambo lipo kiutaratibu zaidi na sio kihisia wala kimihemko.
Ndiyo maana hata Rais katumia kauli ya kuomba na sio Amri akijua fika kuwa masuala ya soka ayaingiliwi kivyovyote na mambo ya kisiasa.
Na fei mwenyewe ndiye mwenye uwezo wa kulihitimisha ili jambo kwa kufuata utaratibu, sheria na kanuni za kimkataba aliousaini na sio vinginevyo.
Asitegemee kwamba ataachwa tu bure aondoke eti kwa kuwa Rais kasema iyo kitu aitokaa itokee.
Bahati nzuri yeye mwenyewe keshatamka hana tatizo lolote na Yanga wala mkataba wake.
Basi yeye mwenyewe ndiye anayeonekana ana ukorofi achutame kwa kufata utaratibu, na utaratibu ni kwenda pale yanga wamtajie dau wanalotaka kwa timu yoyote inayomuitaji iweke mpunga mezani aondoke zake.
Jambo analolazimisha kwamba aachwe tu bure kama anavyotaka yeye na wapambe wake waliomrubuni ili wampate bwerere alitowezekana na atateseka sana.
Viongozi wa yanga wako very clear na Fei angekuwa smart kichwani hili jambo lingekuwa lilishakwisha kitambo sana, lakini jeuri yake na wapambe wake ndio vimemfikisha hapa.
Anajua keshayakoroga pakubwa ndiyo maana anaona ata aibu kwenda pale yanga anapakwepa kama ugonjwa wa ukoma, na awezi kulimaliza hili bila kuihusisha yanga ambao ndio mwajiri wake.
Kwa maana hiyo napenda kuwaeleza waliofurahia kauli ya Rais ya kwamba fei mwenyewe ndiye mwenye utashi wa kulimaliza hilo jambo lake kwa kufata utaratibu na sio yanga.
Yanga wameshampa option 3 za kufata ili aondoke ivyo ni juu yake kusuka ama kunyoa itifaki inazingatiwa.