Ombi: Serikali ituruhusu wananchi kutumia uwanja wa ndege Chato kuanikia mpunga, mihogo na mahindi wakati huu hakuna ndege

Inaitwa legacy ya kufa kufaana 😂😂😂
 
Subiri kidogo, kwani michembe siku hizi haianikwi juu ya paa? hukumsikia polepole akisema huo uwanja utatumika na ndege zinazohitaji kutua kwa dharura.....wasiwasi wangu unaweza usipate ndege yenye dharura kwa zaidi ya miaka 20, itabidi awepo mtu wa kufyeka nyasi na vichaka....
 
Usisahau na dagaa tena kwenye lami zinakauka vizuri Sana bila mchanga.
Mbunge awasilishe hoja
 
Hilo wazo ni zuri litapunguza gharama za kuwalipa wafyeka nyasi
 
Fursa tele we njoo sehemu ya kuanikia ipo
 
Ujamuelewa mtoa mada ule uwanja ukiachwa hivi hivi utaharibika kwa nyasi nk.Wananchi wakipewa kuanikia mazao watausafisha na watautunza hadi ikifika muda wa kutumika tena
 
Umenikumbusha miaka ya 2004, 2005, 2006 Maeneo ya Maseyu na vijiji fulani kabla ya kufika Morogoro ukitokea Dar walikuwa wanaanika mazao yao kandokando ya highway ya Dar - Moro (nje ya ule mchirizi wa njano)
Mpala leo hii kwa wakazi wa kuanzia nzega mpaka tinde nao hufanya hivyo hivyo 😀
 
Ni bora iwe hivyo ili Meneja wa kiwanja na waajiriwa wenzake angalau wapate shughuli ya kufukuza ndege (nyuni) kuliko kusinzia maofisini!
 
Senge unataka kuanika matako?laana ya mungu itakufikia ulipo pumbavu
 
Je kabla ya uwanja kujengwa hawakuwa na mahali pa kuanika mazao mpaka waende uwanja wa ndege?
walianika majumbani, ila tatizo mazao yalichanganyika na vijiwe/mchanga.Kuanika pale airport kero ya michanga kwenye mpunga ndio basi tena. Nadhani umeelewa.Mfano mzuri wa resource sharing- with proper schedulling mukulima anafaidi ,msafiri anafaidi.
 
Siyo mbaya sirkali ingewatoza angalau 200/=@mkulima kwa siku itapata mapato kuliko kukaa bila kazi ya kutua ndege

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…