Kula bata na kupiga picha maeneo flani ni vitu viwili tofauti. Kuna mwanangu mmoja, sometimes anazumba sana na Omary Nyembo. Yeye ana uraia wa EU lakini saa zote yuko Bongo. Ukiwa na passport ya UE unaweza kwenda popote Duniani bila shida. Jamaa ni mtu wa kulipuka pamba sana na ana swagga za kuua, halafu ni photogenic kwelikweli. Mchizi sio ana mkwanja sema huko Dunia ya Instagram na Tiktok wabongo wanamkoma. Yaani yale mapicha kama ya kwenye magazines, New York, Sydney sijui miji makubwa yote Europe. Sasa kuna watu wanafikiria jamaa ni boss kumbe ni style tu ya maisha.