Kwani mfalme Suleiman alikuwa myahudi?. Afadhali wapalestina wana undugu na mfalme Suleiman kwa sababu wote ni waislamu.Na ulivyosema ni ushahidi kuwa ardhi yote hiyo ni ya wapalestina.Ni ardhi ya Mtume wao na babu yao.
Sijui nani huwa anawapotosha namna hiyo yaani hata hujui kuwa sulemani alikuwa ni muislael;ngoja nikupe ilmu,sulemani ni mfalme aliyekuwa wa kabila la Yuda na ni mtoto wa daudi,kabila la Yuda ni moja ya kabila 12 za Israel,mkuu uwe unapitia historia mwenyewe usikomee kumsikiliza shekhe pekee utaendelea kula matango pori mpaka mwisho.
Nyongeza:
2 Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake;
Mathayo 1:2
3 Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu;
Mathayo 1:3
4 Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni;
Mathayo 1:4
5 Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese;
Mathayo 1:5
6 Yese akamzaa mfalme Daudi.
Mathayo 1:6
7 Sulemani akamzaa Rehoboamu; Rehoboamu akamzaa Abiya; Abiya akamzaa Asa;
Mathayo 1:7
8 Asa akamzaa Yehoshafati; Yehoshafati akamzaa Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia;
Mathayo 1:8
9 Uzia akamzaa Yothamu; Yothamu akamzaa Ahazi; Ahazi akamzaa Hezekia;
Mathayo 1:9
10 Hezekia akamzaa Manase; Manase akamzaa Amoni; Amoni akamzaa Yosia;
Mathayo 1:10
11 Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli.
Mathayo 1:11
12 Na baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli;
Mathayo 1:12
13 Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori;
Mathayo 1:13
14 Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa Eliudi;
Mathayo 1:14
15 Eliudi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa Yakobo;
Mathayo 1:15
16 Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.
Mathayo 1:16
17 Basi vizazi vyote tangu Ibrahimu hata Daudi ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi hata ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli hata Kristo ni vizazi kumi na vinne.
Mathayo 1:17