This is...
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 5,050
- 5,204
Mkuu wala si muda mrefu umebaki, na kabla ya Hilo kutokea lazima kwanza makao makuu ya papa yashift kutoka vatcan kwenda Jerusalem.Haya si kwamba ni mtu anaota anaandika,ni lazima yatimie kikamilifu.Na yako ktk hatua nzuri kabisa.japo pengine mm na ww hatutakuwa hai.Hilo jambo halitotokea.Bindadamu huwa tunafanya jeuri ya hali ya juu kama kutahiniwa na Mwenyezi Mungu wakati YEYE hapatai hasara yoyote lakini siku ile jeuri inapoingilia uwezo na maamuzi yake wazi wazi huwa hatoi fursa kwa jeuri hiyo,hutoa adhabu kali na kumfedhehesha mkosaji na habari yake hubaki historia ya muda mrefu ujao hata wengine baadae wakijifanya hawakusikia.
Aliwahi kufanya hivyo mfalme wa Yemen aliyeabudu dini za kishirikina akitaka kuivunja Alkaaba,babu yake Mtume Muhammad s.a.w aliposikia jeshi kubwa asiloweza kupambana nalo liko karibu akaamuru watoto na jamaa zake wakajihifadhi majabalini na akasema anamuachia Mwenyezi Mungu nyumba yake ailinde anavyopenda.Mfalme na jeshi lake wakati alkaaba iko karibu kabisa hawakuifikia wakafa vifo vya kutisha na waliobaki wakarudi kwao katika hali ya kudhalilika sana.Mwenyezi Mungu aliyefanya hivyo yupo na AlAqSA ni miongoni mwa nyumba zake hizo.Wataendelea kuuvunjia heshima na kuzuia waislamu wasiingie lakini siku wakikusudia kuuvunja ndio mwisho wao.
Angalia Mwenyezi Mungu anavyowafedhehesha japo kidogo ili watu wazingatie.Donald Trump alivyofanya kwa Jerusalem mwaka jana tu anaondoka madarakani kwa aibu kubwa na kuwa kichekesho kwa dunia.