Ongezeko la bei ya mafuta: Je, Bunge lina meno ya kuiwajibisha EWURA?




Nakubaliana na wewe kote kasoro hapa [emoji116]

“Hakuna mfanyabiashara anaeweza fanya hoarding ya bidhaa for profiteering purposes where supply outstrips demand…”



Unless tunaishi dunia ya tofauti lakini the last time I checked it’s a Liberal world.


Majuzi tu hapa issue ya kukosekana kwa mahindi, ghala la chakula kuchomwa moto, mchele kupotea?
 
Sisi kama bunge jukumu letu siyo kuhukumu wakosaji serikalini. Zipo mamlaka zenye jukumu la kufanya hilo.
Nakushauri utafute "ilimu" juu ya utenganisho wa mamlaka kati ya bunge, serikali na mahakama.
 
Msimamizi wa EWURA ni mume wa spika, what do you expect?
 
Ndio shida hilipo; mnafikiria upuuzi kwenye vichwa vyenu contrary to economic facts.

Hakuna mtu anaewajuhumu personally, shida ni poor macroeconomic policy za serikali.



Lazima watu wahisi kuhujumiwa personally maana huwezi kuitaja Serikali bila kumtaja Mzee Kikwete.


Kingine kinachofanya watu waamini kwamba wanahujumiwa kwa makusudi ni hao hao watunga hizo policy ndio wafanyabiashara wakubwa wa petroleum & diesel.

Hapa mtanzania wa chini mnunuzi wa lita 20-50 anakwepa vipi hii mitego ya kumkamua?
 
Hako kaspika kama ka kibwengo kataondoka very soon kwenye hicho kiti
Kwanza, mtake radhi Spika wetu, yeye siyo kibwengo.
Pili, Spika wetu hawezi kuondoka madarakani kwa sababu wewe unataka iwe hivyo.
Nikuhakikishie tu kwamba Spika wetu ataendelea kuwepo utake usitake Na kama itakukera, hamia burundi.
 
Sisi kama bunge jukumu letu siyo kuhukumu wakosaji serikalini. Zipo mamlaka zenye jukumu la kufanya hilo.
Nakushauri utafute "ilimu" juu ya utenganisho wa mamlaka kati ya bunge, serikali na mahakama.
Basi Bunge litoe azimio la kumuomba radhi Lowassa..... mlimhukumu badala ya kuachia mamlaka nyingine kufanya hivyo
 

Hapo kwenye taarifa za Bei kuvuja ndipo mtihani ulipo.


Si ajabu kwa Tanzania hii kukuta wafanyakazi tena wenye dhamana ya uongozi huko EWURA nao wanamiliki vituo vya mafuta ama hisa za vituo vya mafuta.


Na hizi taarifa za bei kuvuja ni lazima ziendelee kuvuja maana wafanyabiashara wa mafuta ni viongozi wakubwa serikalini na wengine ni wabunge wawakilishi wa wananchi.
 
Basi Bunge litoe azimio la kumuomba radhi Lowassa..... mlimhukumu badala ya kuachia mamlaka nyingine kufanya hivyo
Bunge halikukurupuka kumuondoa Mheshimiwa Lowasa Madarakani kama mleta mada anavyolitaka bunge likurupuke. Kwa Mh. Lowasa, hoja ya yeye kuhusika kwenye ufisadi Ililetwa hoja bungeni. Bunge kwa umoja wao likairidhia. spika akaunda tume kuchunguza hoja hiyo. Tume ikafanya kazi yake na ikaleta majibu ya uchunguzi wao. Tume ilidhibitisha Mh. Lowasa kuhusika na ufisadi wa Richmond. Kilichofuata ni Bunge lilimwadhibisha kwa kufuata taratibu
 
mkuu
Ni busara kukaa kimya kuliko kujimwambafai kuwa unajua taratibu na sheria.

Kwa hivyo EWURA ni mwiko kuundiwa tume ya kibunge na maamuzi kuchukuliwa?
 


Kwa maelezo haya ni wazi Kwa Tanzania wamiliki wa vituo vya kuuza mafuta ndio either importers ama wana affiliation na importers.

Inawezekana kwa Tanzania, Serikali mpaka sekta binafsi, vyote vinaendeshwa na Syndicate group?

Maana huu mtiririko unatia mashaka;

Rais mstaafu na mtoto wake wanahusishwa na umiliki wa vituo vingi vya mafuta nchini (?)

Mtoto wa Rais anazungumza na Rais wa Uganda (?)

Spouse wa Speaker wa Bunge la JMT ndio Mkurugenzi wa ‘chombo’ muhimu Nishati ya Mafuta (?)

Vituo asilimia 90 nchi nzima wamiliki ni wale wale (?)

Asilimia 99 wamiliki wa vituo vya mafuta ni watumishi wa ummah wenye dhamana ya uongozi Serikalini ama nasaba zao (?)

 
Mkuu
Umeandika ukweli unaoishi.

Tatizo ni CCM
 
Sisi kama bunge jukumu letu siyo kuhukumu wakosaji serikalini. Zipo mamlaka zenye jukumu la kufanya hilo.
Nakushauri utafute "ilimu" juu ya utenganisho wa mamlaka kati ya bunge, serikali na mahakama.


Nadhani mtoa mada analizungumzia Bunge kwa tafsiri ya wawakilishi wa wananchi na hapa wanapaswa kusimama na kusema kwa ajili ya wananchi.
 
Bunge lipi?
Lile dhaifu au Bunge la waitikiaji?
 
Nadhani mtoa mada analizungumzia Bunge kwa tafsiri ya wawakilishi wa wananchi na hapa wanapaswa kusimama na kusema kwa ajili ya wananchi.
Mwananchi yupi labdaa unamuongelea hapa??? Acha kujidai hujui Bunge hakuna linachofanya kwa manufaa ya wanancho yani Mafuta yanapandaa kila siku hakuna cha maana kinasemwaa.. Spika anapewa taarifa ya Ujanja ujanja wa kuchezesha tenda analetaa siasaa.. Ni upuuzi wa ovyoo sanaa taasisi kubwa wanapeana kwa kujuanaaa na bado msiojitambua mnashupaza shingo kutetea Madudu.
 
Mkuu
Umeandika ukweli unaoishi.

Tatizo ni CCM


Sio kwamba Tatizo ni wananchi wanaoendelea “kuikubali” CCM?


Maana kama hali halisi ni hivyo basi hata zile pande zote kuanzia kwa CHAUMA mpaka CHADEMA, hakuna pa kutokea ila kwa wananchi wenyewe.

Maana sioni kwa unono wa funza huyu hawa wengine wanakosaje kunyonya/kunyonyeshwa protein yote hiyo. Hata Kama ni kwa lazima (maridhiano?)
 


Sasa kwa mfano hapa hizi Sentensi zetu mbili ndizo zimetufikisha mahakamani mbele ya hakimu, ukaulizwa kosa langu Mimi hapo kwenye hiyo Sentensi yangu liko wapi?

Unauelewa kiasi gani wa kusoma na kutambua alama za maandishi?

Una utulivu kiasi gani ndani na nje ya mwili wako?

Ubongo wako ulishawahi kutikiswa ukiwa mtoto?

Umetumwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…