Ongezeko la bei ya mafuta: Je, Bunge lina meno ya kuiwajibisha EWURA?

Mahakama ya nyokooo...kafee mbelee hukooo!
 
Sasa mwanaume unatetea Watu wanatafunaa nchii wananchi wanatesekaa kila siku au unalipwaaaa watu waleee...!!

Umelewa?

Una matatizo ya macho?

Una historia yoyote ya maradhi makubwa kukudhoofisha afya yako ukiwa mtoto?

Hukupata lishe bora wakati wa ukuaji wako?

Unakijua kiswahili vizuri??
 
Kila siku mnamsema bibi kidude kuwa hataweza kurudi bungeni.

Sasa huko ewura ndo wanakusanya hela za kampeni ili rupia ipenyezwe vizuri na ushindi upatikane.

Bunge linauwezo wa kuiwajibisha taasisi yeyote ile ukiondoa mahakama. Sema kwa hili bunge letu haliwezi hata kumuita mtu binafsi kama lilivyofanya kwa paskali na CAG.
 
Kwanza, mtake radhi Spika wetu, yeye siyo kibwengo.
Pili, Spika wetu hawezi kuondoka madarakani kwa sababu wewe unataka iwe hivyo.
Nikuhakikishie tu kwamba Spika wetu ataendelea kuwepo utake usitake Na kama itakukera, hamia burundi.
Atabaki kuwa kibwengo maji tu mbegu ya vijini mtwezo
 
Je Bunge letu linaweza kushughulikia kilio cha wananchi kuhusu huu upumbavu wa EWURA?
Mkuu Msanii ,japo siungi mkono matumizi ya lugha kali ya machukizo na matukano kwa kutumia maneno "huu upumbavu wa EWURA", kwasababu whatever EWURA does ni kwa mujibu wa mamlaka yake, sio busara kumtukana mtu mpumbavu wakati anatimiza wajibu wa kwa mujibu wa mamlaka yake!, mtukane aliyetunga hayo mamlaka!.

Ila ume raises a very important issue ya kitu kinachoitwa the doctrine of Separation of powers check and balance kati ya mihimili ya serikali, Bunge na Mahakama.

Bunge ndio mhimili wa kutunga sheria na kuisimamia serikali, Mahakama ni mhimili wa kutafsiri sheria na kutoa haki, serikali ni mhimili wa kutekeleza sheria na kuzihudumia Bunge na Mahakama.

Lakini serikali kupitia by laws inatunga sheria na kupoka madaraka ya Bunge, na mamlaka za Udhibiti zina quasi judicial bodies ambazo zimepoka mamlaka ya Mahakama kwa kusikiliza mashauri na kutoa maamuzi final and conclusive kitu ambacho is not right!.

Huu ni ujinga, only Spika Sitta ndio aliwahi kuukemea, EWURA ilivifungia baadhi ya vituo vya mafuta kwa hoja ya kuuza mafuta machafu. Uamuzi huo ulikuwa ni final and conclusive. Wenye vituo wakalalamika Mahakama kuwa aliyewaletea mafuta machafu ndie awajibike na aadhibiwe, mahakama iamuru EWURA wavifungulie!, EWURA wakatia pamba Masikioni na kugoma kuvifungua. Spika Sitta akaingilia kati
kuwa ni Mahakama Kuu pekee ndio yenye mamlaka ya kutoa maamuzi final and conclusive!, ila kuvifungulia kuendelea kuuza mafuta machafu sio uamuzi wenye maslahi kwa taifa hivyo Spika Sitta akaikomelea Mahakama, Jaji Mkuu wa wakati huo, Jaji Agustino Ramadhan akasema Spika Sitta ameghafilika, Bunge lina uwezo wa kuisimamia serikali tuu na sio kuingilia Mahakama!, Spika Sitta akajibu mapigo kuwa ni Jaji Mkuu ndiye amefilisika, mamlaka Kuu ya nchi ni katiba, na katiba hiyo inapata mamlaka toka kwa wananchi ndio wenye katiba, hivyo Bunge ndilo wawakilishi wa wananchi, Mahakama inapotoa maamuzi ya ajabu ajabu ambayo hayana maslahi kwa taifa, Bunge haliwezi kunyamaza!. Spika Sitta alisema kati ya mihimili mitatu ya dola, mhimili wa Bunge ndio supremacy!.

Spika Sitta alishitakiwa kwenye chama ili anyanganywe kadi ya CCM!, JK akamnusuru, ila alipogombea tena uspika, CCM wakampiga chini kwa hoja ya kumjaribu Mwanamke!. Spika Sitta: Kelele za Kingunge hazininyimi usingizi
P
 
Mkuu tusiingilie familia za watu(Mama Spika na Baba Mkurugenzi Mkuu EWURA).
 
Bunge lile unalifananisha na bunge hili la washabikia singeli na amapiano
Uchawa

Ova
 
Watumie busara wao kwanza kwenye Kuongoza na kuweka maslahi ya taifa mbelee sio Matumbo yao na familia zaooo..!! Wanapeana vyeo kifalaa tuu..
Bunge la sahv wameweka matumbo yao mbele

Ova
 
Mkuu acha kutetea upuuzi,uyo ndiyo tatizo kwenye nchi kwa sasa na ata Mama hana sauti kwasababu ya uyo mtu.Ifike mahala atambue kuwa hii nchi siyo ya ukoo wake,alipewa nafasi kuongoza kama wenzake waliomtangulia,atulie aache wengine nao waongoze!
 
Kila kitu vita vya Urusi na Ukraine,mbona Sukari inazalishwa hapo Kilombero na Kagera lakini inauzwa 3200 kwa kilo!
Nchi imetekwa hii Mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…