Unafuatilia mambo ww au unasema tu!!
unajua ni wabantu wangapi nje ya somalia wanaookolewa kutokana na Ethnic cleansing!!
Nimekuwekewa na headline hapo!!
Mkuu tatizo la sisi ni chuki baina yetu ndio maana hata sisi wakija Waethiopia wakimbizi watawekwa mbele ya makamera na polisi wanapiga nao picha kama wahalifu
Kila leo tunapiga kelele tabia ya kuwafanya wahalifu ndugu zetu sio vizuri,
Ukimbizi unakubalika na ipo kisheria zipo nchi wanaopokea na kupewa hela za wakimbizi kama sisi
Na wapo wasiopokea wakimbizi ila wanachangia kiasi kikubwa cha fedha kwa Umoja wa mataifa
Wakati Wasomali wanapigana vita ya ndani kumuondoa Siad Barre
Wengi walikimbia wakaingia Yemen ila walipofika pwani ya Yemen wengi waliuwawa na wanajeshi na kuzama baharini
Lakini mambo yakageuka baada ya miaka na Saudia wakaanza kumchapa Yemen kwa makombora na ndege za kivita
Wakakimbia nao kupata hifadhi Somalia
Ila Somalia hawakulipa kisasi kama mnachotaka nyie wafanyiwe bali waliwakaribisha na kuwapa hifadhi na chakula pia
Leo wapo bado na wanaishi na biashara wameanza na kuna mpaka Waalimu wa shule na wafanyakazi sehemu nyingi tu na maisha yanaenda
Dunia hii haiendi kwa matakwa ya watu bali inatokea tu kulingana na maisha yalivyo
Sioni sababu ya kuwa na chuki kwa binadamu yeyote
Mimi leo nifanyie ubaya ila kesho ukiugua nakuja kukupa pole na kama unahitaji nakusaidia bila kuangalia ulinifanya nini
Uwe na siku njema