ONYO kwa akina dada wote kuhusu huduma ya kukuza makalio itakayoanza kutolewa Mloganzila

ONYO kwa akina dada wote kuhusu huduma ya kukuza makalio itakayoanza kutolewa Mloganzila

cha msingi nikikaa siumii hivyo hizi 'calio' zangu zinanitosha tu tena zaidi ya sana na kila siku nampa Mungu sifa na utukufu kwa uumbaji wake uliotukuka..!!

'If you don't know who you are, everyone will tell you their clear idea of how you're meant to be', but to each their own..!!
 
Mloganzila wanajitangaza kwamba wanataka kuanza kukuza makalio. Lakini najiuliza, kwa utaalamu upi? Kwa umakini upi? Wa watu wapi? Hawa hawa wanaosahau mikasi tumboni mwa wagonjwa? Hawa hawa wanapasua kichwa badala ya mguu?

Hawa hawa walioshindwa kuwaokoa majeruhi wa ajali ya moto ya Msamvu mpaka wakafa wote? Hawa hawa wanaopasua utumbo mpana wakati mgonjwa anaumwa appendicitis??

Mloganzila wataleta maafa makubwa kwa akina dada ktk huduma yao hii mpya ya kukuza makalio. Mpaka leo kule Uingereza huduma hii Ina 67% ya kufanyika vizuri (operesheni 33% za huduma hii huleta madhara huko Uingereza).

Chonde chonde akina dada mtaoza makalio.
Ni muhimu kuanza kuliko kuogopa kuanza watakao fanikiwa ni sawa ambao hawatafanikiwa wafanya operation watapata uzoefu kupititia wao,miaka itakavyokwenda ndivyo ubora utakavyo ongezeka ,narudia ni bora kuanza kuliko kuogopa kuanza
 
Screenshot_20231012-153648.jpg
 
Mkuu,

Kwanza nikiri uzi wako umejaa kejeli na dhihaka kwa Madaktari wa Kitanzania. Umetutusi na kutuona hatuna tunachokijua.

Pili, katika kushibisha hoja yako umetanabaisha mifano kadhaa ya makosa yaliyofanyika hapo nyuma. Yalikuwa ni makosa yasiyovumilika, lakini ulipaswa kulinganisha takwimu zako na makosa.

Je, kuna visa vingapi vya wagonjwa kuachiwa mikasi na visu tumboni? Je, ni wagonjwa wangapi walifanyiwa upasuaji kwa mafanikio? Linganisha ili tuweze kuona risky ya kupata huduma kwa wagonjwa wetu.

Binadamu tunajisahau sana. Nadhani ni hulka tuliyoumbwa nayo. Mazuri mengi na pasuaji zilizofanyika kwa mafanikio makubwa, yote yanapuuzwa. Na badala yake vinakumbukwa visa vichache sana vilivyotokea.

Swala la Mafuta kule Morogoro unawalaumu madaktari bure. Wengi waliungua kwa asilimia kubwa sana. Hata hivyo, kuna waliookolewa. Hapa ulifurahisha jukwaa.

Lakini, ukisoma taarifa ya hospital ya Mloganzila wamesema wazi kuwa upasuaji huo utafanywa na Madaktari wazawa wakiongozwa na Daktari Bingwa wa upasuaji rekebishi, Dr Mokhit Bhandari kutoka India.

Maana yake ni kuwa wataalam wetu wa upasuaji watakuwa wakiongozwa na huyo Daktari kutoka India. Hivyo kama huwaamini wataalamu wetu, nenda kwa hao mnakokimbiliaga.

Unachopaswa kufahamu ni kuwa, hata katika hospital hizo na kwa wataalam hao, siyo upasuaji zote zinakuwa na mafanikio. Ila kwa sababu umekaza ubongo, huwezi kuelewa.

Acha kejeli za kipumbavu.
 
Mloganzila wanajitangaza kwamba wanataka kuanza kukuza makalio. Lakini najiuliza, kwa utaalamu upi? Kwa umakini upi? Wa watu wapi? Hawa hawa wanaosahau mikasi tumboni mwa wagonjwa? Hawa hawa wanapasua kichwa badala ya mguu?

Hawa hawa walioshindwa kuwaokoa majeruhi wa ajali ya moto ya Msamvu mpaka wakafa wote? Hawa hawa wanaopasua utumbo mpana wakati mgonjwa anaumwa appendicitis??

Mloganzila wataleta maafa makubwa kwa akina dada ktk huduma yao hii mpya ya kukuza makalio. Mpaka leo kule Uingereza huduma hii Ina 67% ya kufanyika vizuri (operesheni 33% za huduma hii huleta madhara huko Uingereza).

Chonde chonde akina dada mtaoza makalio.
Mimi nadhani kwa matibabu amabyo ni ya urembo, wanatakiwa wapate ridhaa ya Serikali kwanza, na si kwa wao kujiamulia tu
Nina shaka kama leseni za kazi zao zinawaruhusu pia kufanya matibabu ya urembo ambayo hatukuwahi kuwa nayo hapo kabla
 
uzi tayari
uzi wako wa ujumla wake una kejeli taaluma ya udaktari na madaktari wa Tanzania..

mapungufu unayosema yanaonesha jinsi gani una chuki binafsi.

Ajali ya Moto .. Mtu akisha ungua 80% ya mwili , hata india huko uwezekano wa kupona ni mdogo.. lakini pia kwenye hiyo ajali wapo walio pona.

Kupasua kichwa badala ya goti. issue ilisha kuwa solved kitambo.. siyo kosa la daktari.. ndiyo maana hao madaktari wapo kazini hadi hivi leo.

Mbona husemi kuhusu kupona kwa prof J, na wagonjwa wengine mahututi,
Mbona husemi kupona kwa yule jamaa alipata ajali ya mwendokasi..

licha ya mazingira magumu, na posho kiduchu na kufanya kazi under pressure ya kisiasa Madaktari wa Tanzania wana jitahidi sana..

Kuhusu hizo operation -
-Kwanza kwa kuanzia watakuwa na madaktari kutoka India
- Ukiona wame amua kufanya hivo, basi ujue wameji ridhisha , na wataalamu wanaweza.
hakuna daktari anayefurahia kufanya kitu kika mdhuru mgonjwa


ni rahis kubwabwaja hapa.. ila siku yaki kufika utapelekwa kwa hao hao madaktari unao wakashfu.. na utakuwa unawasikiliza kwa kila kitu.


Kama hizo % ni correct then mtoa mada na point ya kusikilizwa, Udaktari wa hii nchi ni wa hovyo kabisa kwa basics, kwenye makalio wataoza sana.
 
Swala la Mafuta kule Morogoro unawalaumu madaktari bure. Wengi waliungua kwa asilimia kubwa sana. Hata hivyo, kuna waliookolewa. Hapa ulifurahisha jukwaa.
Kusema walifungua kwa asilimia kubwa ni uwongo wa kuzimu. Watu wamekaa siku 3 Morogoro. Baadaye wakahamishiwa Muhimbili mkawalaza juu ya vitanda badala ya kuwaweka kwenye majokofu watu ambao ngozi (thermoregulator) imeharibiwa na moto. Hata hivyo huko Muhimbili walikaa zaidi ya wiki ndipo wakafa. Ni kukosa weledi. Mpo mpo tu.

Kama unaofanywa na wataalamu toka nje basi andikeni kuwa wataalamu toka nje watakuja Tanzania kukuza makalio. Msiiitaje Mloganzila ambayo huku uraiani inajukqna kama chinjachinja kwasabb ya udumavu wa ujuzi wa madaktari.
 
Hii dunia bhana!,Maarifa yanatupeleka kubaya kiasi cha kumkufuru Mungu wetu,Juzi kuna Sehemu nimeona andiko kuwa Wanasayansi kufika mwaka 2040 watakuwa na uwezo wa kufufua wafu.Hii ni ajabu.Tuombe tu Mungu aturehemu.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
mfu mtarajiwa hawezi kumfufua mfu....ukikubaliana nao basi kubali piah wanaweza kuumba
 
Back
Top Bottom