Uzi Tayari [emoji23][emoji23]
Uzi wako wa ujumla wake una kejeli taaluma ya udaktari na madaktari wa Tanzania.
Mapungufu unayosema yanaonesha jinsi gani una chuki binafsi.
Ajali ya moto
Mtu akisha ungua 80% ya mwili, hata India au Marekani huko uwezekano wa kupona ni mdogo, lakini pia kwenye hiyo ajali wapo walio pona kwa matibabu ya madaktari hao hao.
Kupasua kichwa badala ya goti.
Issue ilisha kuwa solved kitambo, tena jwa tume iliyoundwa na serikali. Halikuwa kosa la daktari. Ndiyo maana hao madaktari wapo kazini hadi hivi leo, wanaendelea na upasuaji kama kawa.
Mbona husemi kuhusu kupona kwa Prof. J na wagonjwa wengine mahututi ambao wameponea mikononi mwa madaktari hao hao?
Mbona husemi kupona kwa yule jamaa alipata ajali ya mwendokasi? Hata watu maarufu kama Mufti na Askofu Ruwa 'ichi walipata changamoto na wakatibiwa hapa hapa.
Kila leo operations za moyo zina fanyika Muhimbili, na wagonjwa wana pona.
Licha ya mazingira magumu, na posho kiduchu, na kufanya kazi under pressure za kisiasa (mfano issue ya kusema watoto na wazee bure, issue ya bima kwa watoto, issue ya kusema consultation fee ni hela ya kumuona daktari), madaktari wa Tanzania wana jitahidi sana. Ukiangalia ranks za mishahara na nchi zingine za Afrika Mashariki, utagundua take-home za madokta Bongo ni dhaifu sana. Ndiyo maana mna wachukulia poa.
Facts.
Hata Kenya kuna baadhi ya vitu wanakuja kujifunza Tanzania, mfano Emergency medicine hawana kule kwao. Ila kuna Mtanzania wewe una negative attitude na vya kwenu.
Jiulize kwa nini Wasudan wameamua kuja Tanzania na siyo nchi nyingine? Kujifunza kwa hao hao madaktari unaosema vilaza?!
Malawi Zambia hawana kabisa vyuo vya madaktari wa meno. Wana kuja Bongo ku take notes.
Hospitali ya kanda ya Mbeya imepewa tuzo maalumu ukanda huu wa SADEC kwa kufanya vizuri kwenye Kaizen Five S. Mataifa mbalimbali wana kuja kujifunza. Wana jifunza kwa hao hao unao waita vilaza?!
Kuhusu hizo operation
-Kwanza kwa kuanzia watakuwa na madaktari kutoka India.
Hii ni kawaida kufanya na wazoefu.
Ukiona wameamua kufanya hivyo, basi ujue kuna jopo lilisha tumwa kabla na wamejiridhisha na utaalamu wanaweza.
Bilashaka "watu wa system" wameridhia hii kitu. Wameona faida na madhara.
-Hakuna daktari anayefurahia kufanya kitu kika mdhuru mgonjwa.
Ni rahis kubwabwaja hapa. Ila siku yakifika utapelekwa kwa hao hao madaktari unao wakashfu. Na utakuwa unawasikiliza kwa kila kitu.