ONYO kwa akina dada wote kuhusu huduma ya kukuza makalio itakayoanza kutolewa Mloganzila

cha msingi nikikaa siumii hivyo hizi 'calio' zangu zinanitosha tu tena zaidi ya sana na kila siku nampa Mungu sifa na utukufu kwa uumbaji wake uliotukuka..!!

'If you don't know who you are, everyone will tell you their clear idea of how you're meant to be', but to each their own..!!
 
Ni muhimu kuanza kuliko kuogopa kuanza watakao fanikiwa ni sawa ambao hawatafanikiwa wafanya operation watapata uzoefu kupititia wao,miaka itakavyokwenda ndivyo ubora utakavyo ongezeka ,narudia ni bora kuanza kuliko kuogopa kuanza
 
Mkuu,

Kwanza nikiri uzi wako umejaa kejeli na dhihaka kwa Madaktari wa Kitanzania. Umetutusi na kutuona hatuna tunachokijua.

Pili, katika kushibisha hoja yako umetanabaisha mifano kadhaa ya makosa yaliyofanyika hapo nyuma. Yalikuwa ni makosa yasiyovumilika, lakini ulipaswa kulinganisha takwimu zako na makosa.

Je, kuna visa vingapi vya wagonjwa kuachiwa mikasi na visu tumboni? Je, ni wagonjwa wangapi walifanyiwa upasuaji kwa mafanikio? Linganisha ili tuweze kuona risky ya kupata huduma kwa wagonjwa wetu.

Binadamu tunajisahau sana. Nadhani ni hulka tuliyoumbwa nayo. Mazuri mengi na pasuaji zilizofanyika kwa mafanikio makubwa, yote yanapuuzwa. Na badala yake vinakumbukwa visa vichache sana vilivyotokea.

Swala la Mafuta kule Morogoro unawalaumu madaktari bure. Wengi waliungua kwa asilimia kubwa sana. Hata hivyo, kuna waliookolewa. Hapa ulifurahisha jukwaa.

Lakini, ukisoma taarifa ya hospital ya Mloganzila wamesema wazi kuwa upasuaji huo utafanywa na Madaktari wazawa wakiongozwa na Daktari Bingwa wa upasuaji rekebishi, Dr Mokhit Bhandari kutoka India.

Maana yake ni kuwa wataalam wetu wa upasuaji watakuwa wakiongozwa na huyo Daktari kutoka India. Hivyo kama huwaamini wataalamu wetu, nenda kwa hao mnakokimbiliaga.

Unachopaswa kufahamu ni kuwa, hata katika hospital hizo na kwa wataalam hao, siyo upasuaji zote zinakuwa na mafanikio. Ila kwa sababu umekaza ubongo, huwezi kuelewa.

Acha kejeli za kipumbavu.
 
Mimi nadhani kwa matibabu amabyo ni ya urembo, wanatakiwa wapate ridhaa ya Serikali kwanza, na si kwa wao kujiamulia tu
Nina shaka kama leseni za kazi zao zinawaruhusu pia kufanya matibabu ya urembo ambayo hatukuwahi kuwa nayo hapo kabla
 


Kama hizo % ni correct then mtoa mada na point ya kusikilizwa, Udaktari wa hii nchi ni wa hovyo kabisa kwa basics, kwenye makalio wataoza sana.
 
Swala la Mafuta kule Morogoro unawalaumu madaktari bure. Wengi waliungua kwa asilimia kubwa sana. Hata hivyo, kuna waliookolewa. Hapa ulifurahisha jukwaa.
Kusema walifungua kwa asilimia kubwa ni uwongo wa kuzimu. Watu wamekaa siku 3 Morogoro. Baadaye wakahamishiwa Muhimbili mkawalaza juu ya vitanda badala ya kuwaweka kwenye majokofu watu ambao ngozi (thermoregulator) imeharibiwa na moto. Hata hivyo huko Muhimbili walikaa zaidi ya wiki ndipo wakafa. Ni kukosa weledi. Mpo mpo tu.

Kama unaofanywa na wataalamu toka nje basi andikeni kuwa wataalamu toka nje watakuja Tanzania kukuza makalio. Msiiitaje Mloganzila ambayo huku uraiani inajukqna kama chinjachinja kwasabb ya udumavu wa ujuzi wa madaktari.
 
mfu mtarajiwa hawezi kumfufua mfu....ukikubaliana nao basi kubali piah wanaweza kuumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ