Open Letter: Rais Samia, TRA isiyo na Support yako, ni Kifo cha Taifa

Labda nikuulize swali mkuu,umetumia njia zote za kiungwana ili mfanyibiashara alipe kodi na halipi,what do you do,a straight answer please.

Unajua,nilitegemea Rais asisitizie juu ya umuhimu wa wafanyibiashara kulipa kodi kama sheria inavyowataka kufanya.Then nilitegemea aseme kwamba kwa mfanyi biashara yeyote ambaye hatapenda kulipa kodi kwa hiari,sheria itachukua mkondo wake,kwa kuwa zipo sheria.

Mkuu huwezi kumbembeleza mfanyibiashara asiyetaka kulipa kodi kwa hiari.Ukimbembeleza hata lipa.Lazima sheria zimbane ili alipe.
 
Watu waliomshauri kuhusu hili swala wana nia ya kumkwamisha..na hakika atakwama kama hatarudi nyuma.
mnapenda mapato yasiyotokana na uhalisia.Mapato yanayotokana na faini au mapatano na DPP hayalipeleki taifa mbali na hayaonesha uhalisia wa uchumi tulio nao.Mapato halisi na endelevu ni yale yanayotokan na shughuli za kiuchumi,biashara,maduhuli,utalii,matumizi binafsi ya watu.
 
Kwa hiyo tangu mliopanza kukusanya kodi kwa njia kandamizi deni la taifa limeshuka kwa % ngapi?
 
Mtoa mada inaonyesha Ni mfanyakazi wa TRA aliyeneemeka na kodi za dhuluma ambazo Mama hazitaki, nawashauri wabadilike nyakari zimebadilika...
 
Ww utakuwa likwepa kodi
 
Hata aliyeandika uzi huu ni mtumishi wa TRA asie na weledi au mnufaika wa rushwa katika task force
 
Mali bila daftari hupotea bila Habari, Muheshimiwa Raisi wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi
 
Kodi za dhuluma hazina baraka! Unaweza nunua ndege kwa kodi za dhuluma na hayo mandege yasiruke na kuleta hasara au ukatumia kodi za dhuluma kujenga bwawa la umeme na mito ikakauka na bwawa likaishiwa maji ikawa Ni hasara ya ajabu...
 
Kwa hiyo tangu mliopanza kukusanya kodi kwa njia kandamizi deni la taifa limeshuka kwa % ngapi?
Swala sio deni kushuka au kupanda ni kuaminika na wakopaji unaweza lipa madeni yako. Sio unakopa hata kama deni lako dogo, halafu kila siku unachelewesha malipo, hakuna mtu atakupa hela yake kirahisi.

IMF Magufuli alipoanza walikuwa wagumu kutoa hela yao, ikabidi Dr Mpango kwenda NY kukutana na ‘Paris Club’ kutafuta mikopo yao. Ni kupitia kukua kwa makusanyo ya ndani IMF wenyewe wakarudi kujipendekeza kuikopesha Tanzania.
 
Hata aliyeandika uzi huu ni mtumishi wa TRA asie na weledi au mnufaika wa rushwa katika task force
Najua ni mtumishi wa TRA,lakini ni kweli kwamba huwezi kumbembeleza mfanyibiashara asiyetaka kulipa kodi.Uta-coerse to some point,lakini akikataa ni lazima alazimishwe na sheria kufanya hivyo.
 
Mali bila daftari hupotea bila Habari, Muheshimiwa Raisi wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi
Na Jambo la kujifunza nchi ziliizoendelea kodi zinakusanywa in a very professional way na hakuna intimidation zinazodiscourage investment, mama yupo 100% perfect kwenye hili kurestore investors confidence, business community ni partners katika development sio maadui, ukiwaua mayai endelevu utapata wapi?, kuna fursa kibao za kodi wajaexplore wanakamua waliopo mpaka damu, unaenda kumdai mtu ana lodge 1.2 bn means ameingiza gross profit 12 bn annually, logically is it possible? Mimi ningetamani wafanyabiashara waliofanikiwa wangekua kwenye TRA BOARD of Directors
 
H
hesabu za kodi haziendi kwa mfumo wa namna hii mkuu.
 
Ww utakuwa likwepa kodi
Nalipa kodi yote vizuri bila kuchelewesha.
Hilo ondoa shaka, na hata TRA nilifanikiwa angalau walanikadiria vizuri hata enzi zile za mateso hivyo kwa upande wangu nalipa vizuri bila matatizo.
Lakini kuna majirani zangu hapa wanabaki kusema mbona huyu hamjamfanyia ivyo?? Kwakweli bado wanaumia.
 
Nchi zilizoendelea ndio Kuna Kodi kubwa kuliko kawaida na tena ndio nguvu unatumika Sana. Unakumbuka kilichomkuta Messi na Ronaldo mahakamani?
Huku Africa kwenye Kodi bado Sana, watu wanaonewa huruma sana
 
Tax base ya TRA ni ndogo sana,
Nchi hii watu wengi wapo vijijini lakini ukweli ni kwamba vijijini zipo biashara nyingi tu ambazo hazijasaliwa na TRA,

TRA wanapaswa wasikae maofisini waende vijijini wakasajili watu,waige mfano wa makampuni ya simu,

TRA wanapopewa target ya makusanyo ya 2trln wanachojua wao ni kuwapandishia watu kodi badala ya kuongeza wigo wa wa kodi.

Halafu ukweli ni kwamba nguvu waliopewa TRA awamu ya tano wamejineemesha Sana kwa rushwa kubwakubwa utawala huu hawa jamaa wametajirika sana kwa rushwa ,

Ninamashaka muandishi wa makala hii ni mfanyakazi wa TRA anaetetea tumbo lake.

NOTE
Ikifika mahali ukaona mfanyabiashara anafikia maamuzi yakuhamisha biashara zake nje ya nchi anaikimbia nchi yake haya sio maamuzi rahisi sana lazima TRA itakua na tatizo lazima wajirekebishe.
 
Najua ni mtumishi wa TRA,lakini ni kweli kwamba huwezi kumbembeleza mfanyibiashara asiyetaka kulipa kodi.Uta-coerse to some point,lakini akikataa ni lazima alazimishwe na sheria kufanya hivyo.
Nilishawashauri TRA mambo mengi kama mzalendo ili wasipoteze kodi, mfano kodi ya matangazo ya biashara ilipohamishwa kutoka local Government, trucks za Coca-Cola, TBL na Bakhresa to mention few walipandua mabango yote baada ya TRS kugoma kuwa flexible kupokea fixed annual rates, matokeo yake wakakosa kabisa, second niliwahi kuwashauri kupendekeza sheria ya kuruhusu wenye Magari yenye namba za zamani kuhuwisha kwenda namba mpya, mfano A kwenda D huku ukudelete old number kwenye mfumo kwa ada say 500,000 Tshs, wangepata pesa nyingi tena widely nk nk
 
Mzee prof assad alisema inabidi to format systems ni kweli kabisa system inabidi iwe formatted
 
Nchi zilizoendelea ndio Kuna Kodi kubwa kuliko kawaida na tena ndio nguvu unatumika Sana. Unakumbuka kilichomkuta Messi na Ronaldo mahakamani?
Huku Africa kwenye Kodi bado Sana, watu wanaonewa huruma sana
Mimi nimeishi Netherlands 5 years na nimekua nikilipa PAYE Kule TRA inaitwa Belasting Dienst, na nimetembelea 9 countries across Europe, hata police customer care ni kama upo 5 Star Hotel, tatizo la waajiriwa wengi wa Idara za Serikali ni lack of exposure na kukazania GPA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…