Mimi nimeishi Netherlands 5 years na nimekua nikilipa PAYE Kule TRA inaitwa Belasting Dienst, na nimetembelea 9 countries across Europe, hata police customer care ni kama upo 5 Star Hotel, tatizo la waajiriwa wengi wa Idara za Serikali ni lack of exposure na kukazania GPA
Mara ya kwanza nilipotoka Tanzania kwenda Switzerland na baadaye Australia, nilijiuliza sana kama na sisi huku Tanzania ni wanadamu kamili.
Nchi za wenzetu, wanaheshimu sana utu na ubinadamu wa watu wote. Hiyo haijalishi mwanadamu huyo ni kiongozi, raia wa kawaida au mtuhumiwa.
Kuna wakati nilikuwa Switzerland, ikaja kujulikana kuwa kuna Wasudan waliingia kwa kupitia mataifa mengine bila kufuata taratibu. Kwa vile Wasudan ni weusi, hivyo kila mweusi alitiliwa mashaka.
Nakumbuka wakati huo nikiwa kijana kabisa, polisi waliponijia, waliniambia:
English, French, Germany? Nikawaambia, English. Kisha wakaendelea:
"Excuse me Sir, my name is ---------, accompanied by ------ and ------. Our main duty is to enforce the law. We want to clear ourselves. We would like to confirm - you are in a country after having met all the immigration requirements. If you don't mind, can we see your passport?
Baada ya kuwaonesha passport yangu, wakatizama sehemu ilipogongwa visa yangu, wakanirudishia. Kisha wakaniambia. We are done. Thank you for your cooperation.
Kisha wakaniuliza, is Tanzania a nice country? Nikawaambia Yes. Mmoja akauliza, do you know Zanzibar, nikawajibu. Wakaniuliza, it is in which part of Africa, nikawajibu. Hapo niling'amua kuwa ingawa tulikuwa tunaendelea na mazungumzo ya kawaida, hawa bwana walikuwa bado kazini. Walikuwa wanataka kujua kama kweli mimi ni Mtanzania, na hiyo passport ni halali, na wala sijapata, pengine kwa njia za panya.
Baadaye, wakaniomba msamaha kwa kunipotezea muda. Mmoja akanipa business card yake, na kusema, feel free to contact me in case you have uncomfortablly been treated by any one while in the country.