Open Letter: Rais Samia, TRA isiyo na Support yako, ni Kifo cha Taifa

Nchi zilizoendelea ndio Kuna Kodi kubwa kuliko kawaida na tena ndio nguvu unatumika Sana. Unakumbuka kilichomkuta Messi na Ronaldo mahakamani?
Huku Africa kwenye Kodi bado Sana, watu wanaonewa huruma sana
Pasi na ushaidi unapiga kelele
 
Nchi zilizoendelea ndio Kuna Kodi kubwa kuliko kawaida na tena ndio nguvu unatumika Sana. Unakumbuka kilichomkuta Messi na Ronaldo mahakamani?
Huku Africa kwenye Kodi bado Sana, watu wanaonewa huruma sana
Na for your information alichoongea Prof Assad kuhusu weledi wa rasilimaliwatu serikalini ni ukweli mtupu, na ndio maana wastaafu wengi wa Serikali hawana maisha marefu baada ya kustaafu kulinganisha na private sector
 
Huyu mleta hoja unaweza kudhani ni raia mwenye nia njema! Lakini huyu anaweza kuwa mmoja wa watumishi vi.laza wa TRA waliokuwa wanapata rushwa kubwa kutokana na mfumo haramu wa Task force kukusanya kodi! Mhe .Rais Mama Samia kuwa macho sana na hawa "_Majambazi" waliojificha TRA.
Kodi ni sheria (Tax law Act) ,kila kitu kuhusu aina za mapato( taxable income) zimeainishwa vizuri na namna ya kutoza kodi! Sasa shida inakuja wapi kama sheria hiyo inafuatwa?!
Huyu ni mmoja wa watoza kodi walioxoea kutumia NGUVU badala ya AKILI!
Sasa anaona mfumo uliokuwa unawapa rushwa kubwa kubwa unakufa na wao walishazoea kujinufaisha!
Cha msingi sana wigo wa walipakodi uongezeke( tax base) na sheria ya kodi ifuatwe, kodi itakusanywa kwa wingi tu na malengo ya trillion 2 kwa mwezi yatafikiwa.

Kunyanyasa wafanyabiashara kwa vitisho na ubabe siyo njia endelevu ya kuongeza mapato ya Serikali.
 
Akili za watanzania waachie wenyewe ipe wakati miezi michache mbele utaona mada humu za watu kulalamika mishahara imechelewa na hiyo miradi kama inategemea mikopo kuna phase zitasimama kwa sababu soon tutakuwa atuaminiki tena na wakopeshaji.

Wala sio uganga hilo jambo linakuja soon, mama anadhani maswala ya kodi ni mzaha mzaha, wa kusikiliza story za kwenye social media.
Kusimamisha miradi ambayo haikupangiliwa vizuri hakuepukiki. Kwenye project management kuna kitu kinaitwa critical path analysis. Ambapo kila activity ina muda wake wa kutekelezwa huku ikizingatia mtegemeano na raslimali fedha.

Kodi hakuanza kukusanya Magufuli, bali zimmmekuwa zikikusanywa toka wakati wa Mkoloni, Awamu ya 1 - 4. Magufuli alikosa mpangilio wa miradi mikubwa hususan (SGR na STIGLERs) ndiyo maana kila wakati aliona fedha anazokusanya hazitoshi.

Pili Magufuli ni mtu wa propaganda. Siyo kweli kwamba alikusanya Sana kumzidi JK. Yawezekana walikuwa sawa. Nasema hivi kwa kuwa wakati wa JK Halmashauri zilikuwa zinakusanya na kutekelezwa mipango yao ya maenseleo. Ila wakati wa Mwendazake alizipokonya Halmashauri na fedha zote zikaingia Hazina.

Tatu Magufuli alikuwa anakopa wastani wa Tsh 5 Trilion kwa mwaka wakati JK alikuwa anakopa wastani wa Tsh 2 Trilion. Deni la Serikali wakati wa BWM likikuwa Tsh 10 Trillion, wakati wa JK 30 Trillion na Mwendazake hadi anakufa liko Tsh 60 Trillion.

Mwacheni Mama Rais SSH atekeleze majukumu yake bila pressure. Amesema hataki Kodi ya dhuluma
 
Jana nilinunua mabati ya milioni kadhaa, mhindi kaniambia tuandike risiti ya bei pungufu ili nipunguziwe kiasi cha laki 2, nikagoma (sikugoma kwasababu ya kuwa sihitaji hela la hasha, lugha aliyotumia huyu mfanyabishara....eti kama siridhiki niende nikanunue huko Chato! Najua madhara ya hiki nilichocanya, nilinunua tu, Haki ya Mungu ngoja wenye akili tuangalie huu mchezo wa TRA na wafanyabiashara...historia itajirudia, ambulance za kubeba wagonjwa zitakosa mafuta, polisi hawatawahi eneo la uharifu maana magari yatakuwa mabovu na ule utekaji wa mabasi utarudi!
 
Mimi nimeishi Netherlands 5 years na nimekua nikilipa PAYE Kule TRA inaitwa Belasting Dienst, na nimetembelea 9 countries across Europe, hata police customer care ni kama upo 5 Star Hotel, tatizo la waajiriwa wengi wa Idara za Serikali ni lack of exposure na kukazania GPA
Mara ya kwanza nilipotoka Tanzania kwenda Switzerland na baadaye Australia, nilijiuliza sana kama na sisi huku Tanzania ni wanadamu kamili.

Nchi za wenzetu, wanaheshimu sana utu na ubinadamu wa watu wote. Hiyo haijalishi mwanadamu huyo ni kiongozi, raia wa kawaida au mtuhumiwa.

Kuna wakati nilikuwa Switzerland, ikaja kujulikana kuwa kuna Wasudan waliingia kwa kupitia mataifa mengine bila kufuata taratibu. Kwa vile Wasudan ni weusi, hivyo kila mweusi alitiliwa mashaka.

Nakumbuka wakati huo nikiwa kijana kabisa, polisi waliponijia, waliniambia:

English, French, Germany? Nikawaambia, English. Kisha wakaendelea:

"Excuse me Sir, my name is ---------, accompanied by ------ and ------. Our main duty is to enforce the law. We want to clear ourselves. We would like to confirm - you are in a country after having met all the immigration requirements. If you don't mind, can we see your passport?

Baada ya kuwaonesha passport yangu, wakatizama sehemu ilipogongwa visa yangu, wakanirudishia. Kisha wakaniambia. We are done. Thank you for your cooperation.

Kisha wakaniuliza, is Tanzania a nice country? Nikawaambia Yes. Mmoja akauliza, do you know Zanzibar, nikawajibu. Wakaniuliza, it is in which part of Africa, nikawajibu. Hapo niling'amua kuwa ingawa tulikuwa tunaendelea na mazungumzo ya kawaida, hawa bwana walikuwa bado kazini. Walikuwa wanataka kujua kama kweli mimi ni Mtanzania, na hiyo passport ni halali, na wala sijapata, pengine kwa njia za panya.

Baadaye, wakaniomba msamaha kwa kunipotezea muda. Mmoja akanipa business card yake, na kusema, feel free to contact me in case you have uncomfortablly been treated by any one while in the country.
 
Sasa kutana na wabongo, impression ya kwanza nitapataje rushwa kwa huyu bwana, mm hata traffic police akinikamata kwa overspeed unamwona mostly anafocus compromise na ukimwambia timiza wajibu wako kitaaluma kwa Maana ya fine hata facial expression unaona hakuipenda
 
Na Jambo la kujifunza nchi ziliizoendelea kodi zinakusanywa in a very professional way na hakuna intimidation zinazodiscourage investment, mama yupo 100% perfect kwenye hili kurestore investors confidence, business community ni partners katika development sio maadui, ukiwaua mayai endelevu utapata wapi?, kuna fursa kibao za kodi wajaexplore wanakamua waliopo mpaka damu, unaenda kumdai mtu ana lodge 1.2 bn means ameingiza gross profit 12 bn annually, logically is it possible? Mimi ningetamani wafanyabiashara waliofanikiwa wangekua kwenye TRA BOARD of Directors
Watu wengi mnashindwa kuelewa kuwa mosi uwekaji wa vitabu tanzania ni kizungumkuti, ambayo ndio chanzo cha kupata taarifa, na hizo taarifa wanaotakiwa kuwa nazo ni wafanya biashara, pili ni utoaji wa receipt, mkiambiwa tumechelewa sana muelewe hivyo. Hiyo mifumo ipo siku nyingi lakini ukija Tz watu hawataki iwepo na wanayofanya hivyo ni wafanya biashara , kuwekwa wizara ya technology n.k ya Faustine, inatakiwa kujulikana imewekewa kwa sababu gani, ni kuimarisha mifumo ua taarifa ambayo tumechelewa sana kuiweka. Rejea issue za flow meter na issues za in transit, na issue za wenye ma basi, halafu uje kwenye maduka yetu, na pia mfumo yetu ya malipo ndio utajua kiasi cha ukwepaji wa kodi Tanzania.
Na Mimi nina muheshimu sana Nyerere, alijaribu kuweka hiyo mifumo, lakini watu hawakumuelewa, sijui elimu au makusudi, na income tax ya wakati ule elimu ilikuwa ndogo, na vyeti fake.

JPM NA MSISITIZO WA NYERERE KUHUSU KODI

Wakenya wana piga kazi sana ukweli ndio huo sisi tumezoea dhuluma hatujui kufuata sheria Kenya wana jua haki ya kisheria kuliko sisi!
TRA ipewe wakenya tu watafuata sheria bila kudhulumiwa serikali wala wafanya biashara!
Wewe hao watu ni wezi balaa!
Unataka watuibie sio!?
 
Watu wengi mnashindwa kuelewa kuwa mosi uwekaji wa vitabu tanzania ni kizungumkuti, ambayo ndio chanzo cha kupata taarifa, na hizo taarifa wanaotakiwa kuwa nazo ni wafanya biashara, pili ni utoaji wa receipt, mkiambiwa tumechelewa sana muelewe hivyo. Hiyo mifumo ipo siku nyingi lakini ukija Tz watu hawataki iwepo na wanayofanya hivyo ni wafanya biashara , kuwekwa wizara ya technology n.k ya Faustine, inatakiwa kujulikana imewekewa kwa sababu gani, ni kuimarisha mifumo ua taarifa ambayo tumechelewa sana kuiweka. Rejea issue za flow meter na issues za in transit, na issue za wenye ma basi, halafu uje kwenye maduka yetu, na pia mfumo yetu ya malipo ndio utajua kiasi cha ukwepaji wa kodi Tanzania.
Na Mimi nina muheshimu sana Nyerere, alijaribu kuweka hiyo mifumo, lakini watu hawakumuelewa, sijui elimu au makusudi, na income tax ya wakati ule elimu ilikuwa ndogo, na vyeti fake.
Tatizo wanaoajiriwa kuweka mifumo wanaweka mifumo ya matumbo yao, just imagine maafisa biashara wa halmashauri zote wanalipwa mishahara ya mwaka huku wakitekeleza jukumu la kurenew leseni tu kipindi cha mwaka mpya wa fedha wa Serikali tu, hawahangaiki hata kuwa train wafanyabiashara wadogo wakue na wajifunze kuweka kumbukumbu zao kiusahihi, ili baadae wakue na wawe walipa kodi wakubwa
 
Kipindi cha mwendazake wafanyakazi wa TRA walikuwa wanakula rushwa sana kwa wafanyabiashara,hasa kitengo cha enforcement. Sasa inaonekana wewe mleta mada umetumwa ili kurudisha lile zoezi muendelee kuwabambikia watu mikodi
 
Kusimamisha miradi ambayo haikupangiliwa vizuri hakuepukiki. Kwenye project management kuna kitu kinaitwa critical path analysis. Ambapo kila activity ina muda wake wa kutekelezwa huku ikizingatia mtegemeano na raslimali fedha.

Kodi hakuanza kukusanya Magufuli, bali zimmmekuwa zikikusanywa toka wakati wa Mkoloni, Awamu ya 1 - 4. Magufuli alikosa mpangilio wa miradi mikubwa hususan (SGR na STIGLERs) ndiyo maana kila wakati aliona fedha anazokusanya hazitoshi.

Pili Magufuli ni mtu wa propaganda. Siyo kweli kwamba alikusanya Sana kumzidi JK. Yawezekana walikuwa sawa. Nasema hivi kwa kuwa wakati wa JK Halmashauri zilikuwa zinakusanya na kutekelezwa mipango yao ya maenseleo. Ila wakati wa Mwendazake alizipokonya Halmashauri na fedha zote zikaingia Hazina.

Tatu Magufuli alikuwa anakopa wastani wa Tsh 5 Trilion kwa mwaka wakati JK alikuwa anakopa wastani wa Tsh 2 Trilion. Deni la Serikali wakati wa BWM likikuwa Tsh 10 Trillion, wakati wa JK 30 Trillion na Mwendazake hadi anakufa liko Tsh 60 Trillion.

Mwacheni Mama Rais SSH atekeleze majukumu yake bila pressure. Amesema hataki Kodi ya dhuluma
Mkuu watu wanapotaka kukukopa awaangalii sana unadaiwa kiasi, wanachochali wao ni ratios zako mfano; debt interest to income ratio, interest cover and so forth.

Na ratio zina bench mark zake wewe kama serikali yako gearing ratio zake ni over 70% hakuna mtu atakupa hela yake kirahisi.

Basically kinachofanywa na IMF or any other international lender kwenye risk assessment za national financing is just basic financial accounting wamebadili tu terminologies to fit economics.

Kingine serikali ni ‘going-concern’ akitoka mmoja akija mwingine alichokuta kiko mezani ni mzigo wake as far as the world is concerned.

Kama ni miradi ambayo ipo kwenye pipeline aijaanza bado raisi akiona terms sio nzuri it’s OK kuzifuta. Lakini kama ni project ambazo zipo nusu ni jukumu lake kumaliza, kama ni madeni ya nchi ni yake kuyalipa.

Sasa ata kama Magufuli alikopa sana kaondoka anauwezo wa kulipa, na wewe ukafika ukashindwa kulipa madeni ina maana viatu vya kazi havikutoshi.

Na kama kuna miradi ambayo ipo tayari ya kimkakati ukashindwa kuimaliza kisa kukosa mapato kazi imekushinda.

Usione hao maraisi wengine wanashangaa hayati kawezaje kutimiza mengi kwa muda mfupi, kukopesheka sio kazi raisi kama unavyodhani; you need to improve your collection. Vinginevyo tusahau maendeleo watanzania, turudi kwenye vicious povert cycle tuliyoizoea tangia dunia iumbwe.

Mwisho miradi yote ya kimkakati aliyofanya Magufuli kwenye infrastructures iliyoisha na ambayo ipo njiani ina multiplier effect kubwa sana kwenye uchumi, kuacha hiyo miradi ni sawa na kusema tumezaliwa maskini na tufe maskini tu; “ponda mali, kufa kwaja” wajao watajijua wenyewe.
 
Mkuu watu wanapotaka kukukopa awaangalii sana unadaiwa kiasi, wanachochali wao ni ratios zako kama za debt interest to income ratio, interest cover to income and so forth.

Na ratio zina bench marks zake wewe kama serikali yako gearing ratio zake ni over 70% hakuna mtu atakupa hela yake kirahisi.

Basically kinachofanywa na IMF or any other international lender kwenye risk assessment za national debt management is just basic financial accounting wamebadili tu terminologies to fit economics.

Serikali ni ‘going-concern’ akitoka mmoja akija mwingine alichokuta kiko mezani ni mzigo kama ni miradi ambayo ipo kwenye pipeline aijaanza bado akiona terms sio nzuri, kama ni project ambazo zipo nusu ni jukumu lake kumaliza, kama ni madeni ni yake kuyalipa.

Sasa kama Magufuli ata kama alikopa kaondoka anauwezo wa kulipa na wewe ukafika ukashindwa kulipa madeni ina maana viatu vya kazi havikutoshi. Na kama kuna miradi ambayo ipo tayari ya kimkakati ukashindwa kuimaliza kisa kukosa mapato kazi imekushindwa.

Usione hao maraisi wengine wanashangaa hayati kawezaje kutimiza mengi kwa muda mfupi, kukopesheka sio kazi raisi kama unavyodhani; you need to improve your collection. Vinginevyo tusahau maendeleo watanzania, turudi kwenye vicious povert cycle tuliyoizoea tangia dunia iumbwe.
Collection sio kuua private sector, madini na utalii sustainable pia lazima ziwe endelevu
 
Mhe Rais, naomba utumie dakika chache kusoma barua hii wewe mwenyewe, na kama hautapata muda naomba wasaidizi wako wakusaidie kuusoma na kukufikikishia.

Naandika haya kama Raia aliye na wasiwasi baada ya kutafakari kwa kina juu ya "TONE" yako uliyokwishaitoa hadharani kuhusu taasisi hii nyeti inayokusanya mapato ya nchi.

Pia ni baada ya kukaa na baadhi ya maafisa kodi ambao wanakiri kwamba toka kauli yako kazi yao imekuwa ngumu kupindukia ni kama wamewekwa benchi!

Mhe. Rais, kwa sasa kuna mambo makuu mawili yanayotokea ambayo sidhani kama umeshayajua.

i) Wafanyabiashara wameacha kutoa risiti za EFD na ukiwadai wanasema kabisa WASISUMBULIWE maana Rais wao ameshatoa maelekezo hayo. Wapo HOLIDAY!

Hata TRA wenyewe wamecancel mazoezi ya ku-enforce utoaji risiti. Maana wanajua wakienda watabagazwa!

Swali kubwa hapa, Je, Kodi gani itakusanywa na nchi bila watu kutoa risiti? Unawezaje kutrack mauzo ya mlipa kodi bila kutoa risiti ya EFD?

ii) Wafanyabiashara hawapeleki tena malipo ya kodi kwa kama kasi ya awali, kila mmoja ameset mind ya kupinga kodi maana anaona kama kile alichokadiriwa si sahihi baada ya kauli ya Rais.

Wataalam wenyewe wanasema impact yake itaonekana katika taarifa za mapato mwezi huu na ijayo!

Mhe Rais, katika taasisi zote chini yako zinazohitaji Top Level Presidential Support ya moja kwa moja ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Bila TRA yenye support ya Rais, Taifa linakufa, na hakika litashindwa kufikia malengo yake.

Ni sawa na katika taasisi za kawaida, kitengo ambacho kinaleta mapato kwa taasisi, ndicho Mkurugenzi Mkuu hukitolea macho na kukipa support yote inayohitajika ili aweze kufikia malengo yake kibiashara.

Mhe Rais, sitaki kurejea katika maagizo yako ya nyuma kuhusu namna TRA wanavyofanya kazi ambayo uliyatoa hadharani, ila ningekuwa mmoja wa washauri wako ningeshauri usiongee sentensi zile hadharani bali uongee moja kwa moja na Viongozi na Wafanyakazi wa TRA indoors.

Kwa nini??. Kwa sababu nature ya mfanyabiashara ni kulalamika na kuficha mapato yake halisi. Hakuna mfanyabiashara hata mmoja aliye genuine ya kipato chake, Popote duniani. Hakuna!

Mhe. Rais, unaweza kukuta mfanyabiashara anafanya biashara yenye mauzo ya Billioni 2 anadeclare faida ya milioni 4, Seriously?

Katika mazingira hayo unahitaji Taasisi yenye nguvu na mamlaka ili iweze kutafuta wapi mtu huyu alipodanganya ili Serikali iweze kukusanya kodi yake. Otherwise, utachukua hio hio Milioni 4 alafu maisha yanaendelea wakati kwa hakika labda mtu huyo alipaswa kulipa milioni 50.

Mwisho:
Natambua kupitia maneno ya Makamu wako, Mhe. Mpango, umeweka malengo ya Trillion 2 kwa Mwezi, lakini ukweli ni kwamba hata kama sheria zitabadilika na baadhi ya kodi kupungua lazima kuna nyingine zitapanda ili kufikia lengo la Trillion 2. Sasa nani atatumika kuenforce ukusanyaji huo? Je ni hao hao TRA? Je wataweza ku-enforce huo ukusanyaji bila support yako? Au kuna watu wanaku-sabotage ili ushindwe kufikia malengo hayo?

Naomba kuhitimisha kwa kukushukuru kwa muda wako.

Wako,
Raia aliye na wasiwasi.
15 April, 2021

Nyongeza muhimu kutoka kwa baadhi ya wadau [emoji116]
Yetu macho ila inaogopesha sana
 
Collection sio kuua private sector, madini na utalii sustainable pia lazima ziwe endelevu
Sasa private sector imekufa vipi wewe unanunua chakula supermarket ya serikali, una kwenda kwenye starehe ya ukumbi wa serikali, unaweka mafuta ya gari kituo cha serikali, unanunua simu yako kwenye duka la serikali, umejenga nyumba yako na mafundi wa serikali.

Ni huduma gani hasa katika maisha yako ya kila siku unapewa na serikali mpaka useme private sector imekufa?

If anything unatumia barabara bure, watoto wako wanasoma bure, wanapata mikopo ya chuo kikuu bila ya uonevu, huduma za afya bei nafuu, usiku umewekea taa barabarani masela yasikukabe; hayo ndio matumizi ya kodi unayolipa.

Haya ndio mambo mnayoyaokota mitandaoni bila ya ushahidi wowote.
 
Mhe Rais, naomba utumie dakika chache kusoma barua hii wewe mwenyewe, na kama hautapata muda naomba wasaidizi wako wakusaidie kuusoma na kukufikikishia.

Naandika haya kama Raia aliye na wasiwasi baada ya kutafakari kwa kina juu ya "TONE" yako uliyokwishaitoa hadharani kuhusu taasisi hii nyeti inayokusanya mapato ya nchi.

Pia ni baada ya kukaa na baadhi ya maafisa kodi ambao wanakiri kwamba toka kauli yako kazi yao imekuwa ngumu kupindukia ni kama wamewekwa benchi!

Mhe. Rais, kwa sasa kuna mambo makuu mawili yanayotokea ambayo sidhani kama umeshayajua.

i) Wafanyabiashara wameacha kutoa risiti za EFD na ukiwadai wanasema kabisa WASISUMBULIWE maana Rais wao ameshatoa maelekezo hayo. Wapo HOLIDAY!

Hata TRA wenyewe wamecancel mazoezi ya ku-enforce utoaji risiti. Maana wanajua wakienda watabagazwa!

Swali kubwa hapa, Je, Kodi gani itakusanywa na nchi bila watu kutoa risiti? Unawezaje kutrack mauzo ya mlipa kodi bila kutoa risiti ya EFD?

ii) Wafanyabiashara hawapeleki tena malipo ya kodi kwa kama kasi ya awali, kila mmoja ameset mind ya kupinga kodi maana anaona kama kile alichokadiriwa si sahihi baada ya kauli ya Rais.

Wataalam wenyewe wanasema impact yake itaonekana katika taarifa za mapato mwezi huu na ijayo!

Mhe Rais, katika taasisi zote chini yako zinazohitaji Top Level Presidential Support ya moja kwa moja ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Bila TRA yenye support ya Rais, Taifa linakufa, na hakika litashindwa kufikia malengo yake.

Ni sawa na katika taasisi za kawaida, kitengo ambacho kinaleta mapato kwa taasisi, ndicho Mkurugenzi Mkuu hukitolea macho na kukipa support yote inayohitajika ili aweze kufikia malengo yake kibiashara.

Mhe Rais, sitaki kurejea katika maagizo yako ya nyuma kuhusu namna TRA wanavyofanya kazi ambayo uliyatoa hadharani, ila ningekuwa mmoja wa washauri wako ningeshauri usiongee sentensi zile hadharani bali uongee moja kwa moja na Viongozi na Wafanyakazi wa TRA indoors.

Kwa nini??. Kwa sababu nature ya mfanyabiashara ni kulalamika na kuficha mapato yake halisi. Hakuna mfanyabiashara hata mmoja aliye genuine ya kipato chake, Popote duniani. Hakuna!

Mhe. Rais, unaweza kukuta mfanyabiashara anafanya biashara yenye mauzo ya Billioni 2 anadeclare faida ya milioni 4, Seriously?

Katika mazingira hayo unahitaji Taasisi yenye nguvu na mamlaka ili iweze kutafuta wapi mtu huyu alipodanganya ili Serikali iweze kukusanya kodi yake. Otherwise, utachukua hio hio Milioni 4 alafu maisha yanaendelea wakati kwa hakika labda mtu huyo alipaswa kulipa milioni 50.

Mwisho:
Natambua kupitia maneno ya Makamu wako, Mhe. Mpango, umeweka malengo ya Trillion 2 kwa Mwezi, lakini ukweli ni kwamba hata kama sheria zitabadilika na baadhi ya kodi kupungua lazima kuna nyingine zitapanda ili kufikia lengo la Trillion 2. Sasa nani atatumika kuenforce ukusanyaji huo? Je ni hao hao TRA? Je wataweza ku-enforce huo ukusanyaji bila support yako? Au kuna watu wanaku-sabotage ili ushindwe kufikia malengo hayo?

Naomba kuhitimisha kwa kukushukuru kwa muda wako.

Wako,
Raia aliye na wasiwasi.
15 April, 2021

Nyongeza muhimu kutoka kwa baadhi ya wadau 👇
Kwa kweli unastahili kupewa nishani ya Mzalendo mkereketwa! Mungu akubariki sana! Wafanyabiashara ni watu muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa. Tatizo ni kwamba watanzania hatuna elimu ya kodi kama sehemu ya uzalendo. Tangu chekechea mpaka chuo kikuu hakuna mahali elimu ya kodi na umuhimu wake inafundishwa!
Kwa hiyo karibu wafanyabiashara wote hawalipi kodi kwa hiari! Ukiwapa mwanya watakwepa kodi au watatoa kodi kwa udanganyifu! Kwa sababu ya mazoea ya kukwepa kodi, wafanyabiashara wakifuatiliwa vilivyo kuhusu kodi wanahisi wanaonewa! Wakitoa kodi wanahisi faida inapungua maana walizoea kuifanya kodi iliyopaswa kulipwa kama sehemu ya faida!
Kwa sasa hivi TRA watakuwa na wakati mgumu sana wa kufuatilia kodi, maana wametafisirika kama vile walikuwa wanabambikiza kodi! Mama huu ushauri uliopewa ni wa muhimu sana! Wasaidizi wako wengine wanaweza wasikushauri huku wakitazamia ukwame halafu waseme hakuwa anakubali ushauri! Kwa mazingira ya Tanzania hiki kizazi chetu ni cha kulipa kodi kwa lazima wala katika hili tusidanganyane! Tuwekeze kwenye elimu ya kodi tangu chekechea ili vizazi vijavyo vione fahari ya kulipa kodi!! Mama kaza buti kabisa kwa habari ya kodi ikiwezekana katika hili uwe mkali kuliko mtangulizi wako. Ukikamata mkwepa kodi mfilisi kabisa ili wengine waogope! Vinginevyo we are bound to fail!
 
Najua ni mtumishi wa TRA,lakini ni kweli kwamba huwezi kumbembeleza mfanyibiashara asiyetaka kulipa kodi.Uta-coerse to some point,lakini akikataa ni lazima alazimishwe na sheria kufanya hivyo.
Weka clip aliposema wabembelezwe msitupotoshe nyie maafisa wa TRA. Hakuna Mhe.Rais aliposema watu wabembelezwe kulipa kodi, alisema tumieni akiri kwa maslahi mapana ya Serikali na mlipa kodi pia.
 
Back
Top Bottom