Open Letter: Rais Samia, TRA isiyo na Support yako, ni Kifo cha Taifa

Open Letter: Rais Samia, TRA isiyo na Support yako, ni Kifo cha Taifa

Kodi imekusanywa kuanzia Serikali ya Mkoloni na itaendelea kukusanywa.

Mwendazake alikosea sehemu moja. Aliwafirisi wafanya biashara wakubwa then akakosa mahali pa kukusanya kodi, ndiyo akaja na wimbo wa KIJINGA wa EFD machine.

Mkapa na Kikwette ndiyo waliojenga uchumi imara bila hiyo EFD yenu ambayo mumeifanya ndiyo collection driver.

Ukiwa kiongozi unapswa ufuate Pareto principle kwenye kujenga uchumi. Pareto Principe inasema ni Asilimia 20% tu ya walipa kodi ndiyo huleta 80% ya mapato yote. Hao ndiyo una deal nao kama Twiga Cement, TCC, TBL, BAKHRESSA, MODEWJI, IPP etc. Hawa akina kajamba nani waliobakia ambao ni 80% wanachangia 20% tu ya mapato ambao ni vituo vya petrol station, maduka ya Kariakoo, mabaa, guest house, mabasi etc.

Yaani nguvu kubwa inatumika kwenye chanzo kikubwa cha kodi. Hiyo ndiyo AKILI

Lakini akili mbovu ya Mwendazake iliwakera na kuwa harass wafanyabiashara kama Yusuf Manji ikasahau kuwa ni mlipa kodi kupitia wafanyakazi aliowaajiri, bidhaa anazo nunua na ku export as well as anazo import.

Tuna Imani na Rais SSH tutakusanya kodi iliyo ya haki na maisha yataendelea
 
UMEPOTOSHA ALICHOSEMA MH.RAIS MAKUSUDI HALAFU MATAGA WENZIO WANAKUSIFIA.

MAMA ALISEMA TUNAHITAJI KODI ZIKUSANYWE ILA SIO ZA DHULUMA.

ALISEMA, KUNYANG'ANYA WATU PESA KWENYE AKAUNTI ZAO, KUSINGIZIA KESI ZA UHUJUMU UCHUMI NA KUTOA MAKADIRIO YASIO SAHIHI HIYO HAIKUBALIKI.

MAGOFOOL ALIKUSANYA KODI KWA MUDA MFUPI TU MIAKA MITATU YA KWANZA BAADA YA HAPO BIASHARA ZIKAFA AKAANZA KUKOPA HELA NJE NA KUTOA TAKWIMU ZA MAKUSANYO ZA UONGO.

KAMA ALIKUSANYA PESA NYINGI MBONA MIRADI YOTE INAFANYIKA KWA MIKOPO AU MISAADA KUTOKA NJE? MBONA AMESHINDWA KUAJIRI NA KUPANDISHA MISHAHARA?

JIULIZE MAGOFOOL DENI LA TAIFA ALIKUTA SH.NGAPI NA KAACHA SH.NGAPI. UKIJUA HILO HUWEZI KUJA KUANDIKA UHARO HAPA TENA.
 
Weka clip aliposema wabembelezwe msitupotoshe nyie maafisa wa TRA. Hakuna Mhe.Rais aliposema watu wabembelezwe kulipa kodi, alisema tumieni akiri kwa maslahi mapana ya Serikali na mlipa kodi pia.
Hawa ni sukuma Gang mkuu
 
UMEPOTOSHA ALICHOSEMA MH.RAIS MAKUSUDI HALAFU MATAGA WENZIO WANAKUSIFIA.

MAMA ALISEMA TUNAHITAJI KODI ZIKUSANYWE ILA SIO ZA DHULUMA.

ALISEMA, KUNYANG'ANYA WATU PESA KWENYE AKAUNTI ZAO, KUSINGIZIA KESI ZA UHUJUMU UCHUMI NA KUTOA MAKADIRIO YASIO SAHIHI HIYO HAIKUBALIKI.

MAGOFOOL ALIKUSANYA KODI KWA MUDA MFUPI TU MIAKA MITATU YA KWANZA BAADA YA HAPO BIASHARA ZIKAFA AKAANZA KUKOPA HELA NJE NA KUTOA TAKWIMU ZA MAKUSANYO ZA UONGO.

KAMA ALIKUSANYA PESA NYINGI MBONA MIRADI YOTE INAFANYIKA KWA MIKOPO AU MISAADA KUTOKA NJE? MBONA AMESHINDWA KUAJIRI NA KUPANDISHA MISHAHARA?

JIULIZE MAGOFOOL DENI LA TAIFA ALIKUTA SH.NGAPI NA KAACHA SH.NGAPI. UKIJUA HILO HUWEZI KUJA KUANDIKA UHARO HAPA TENA.
Kama wewe ni mwislamu, jioni pata futari nutalipa. Kama mkristu pata soda weekend imeanza.

Hawa watu ni wajinga Sana na wanajifanya wasahaulifu. Wanamtukuza mtu aliyekuja kuharibu uchumi wetu kwa kukosa mipango sahihi na kutosikia ushauri
 
Tuelewe spirit ya Rais kuhusu kodi ni kuwa wigo wa kodi upanuliwe na wawe wabunifu. Lakini pia falsafa ya Rais ni kuwa ukusanyaji wa kodi ufanyike kwa weledi na ufasaha bila kubambakiza kodi na kuwanyanyasa wafanya biashara ambao baadhi wamekimbia nchi na kufanya uchumi kusinyaa. Hivyo, watu wasipotoshe nia njema ya Rais.

Kitendo cha kuchukua mali au fedha za mfanya biashara benki ni kinyume na lengo zuri la ongeza mtaji, ongeza biashara na ongeza kodi (OMOBOK) ILi kuleta maendeleo ya dhati.

Rais yuko sahihi walipa kodi wabadilishe "mindset" zao kuhusu kodi na biashara. Wafanya biashara ni partners wao. Wabadilishe mbinu km ambavyo ukaguzi wa mahesabu CAG walipo kuja na njia mbinu mpya na mbadala

Watoke kwenye enforcement ya kuharasss(reactive) kwenda kwenye proactive. Hii ni pamoja na kuelemisha na kujenga mitizamo chanya na endelevu ya kulipa kodi kuliko sasa. Itafika mahala kodi za nguvu zitakwama kabisa. Kamishna Mkuu wa TRA ana kazi kubwa ya kubadilisha mitizamo na mbinu za utendaji wa watu wake,mifumo ya ufuatiliaji na ushirikishwaji wa jamii badala ya kukaa ofisni na kucheza na makaratasi bila kuzingatia uhalisia wa biashara za watu vinginevyo hakuna mwekezaji atayekuja nchini. TRA msaidie mama acheni kutumia mbinu zilezile katka mazingira mapya. Hii ni pamoja na kurejesha VAT returns.

Rais Hayati Mgafuli aliwahi pia kulionya hili la kunyanyasa wafanya biashara na kupelekea Kichere kamishna mkuu wa wakati ule kumwondoa madarakani na kumteua Katibu Tawala.

Kuhusu kusemea hadhara masuala ya kodi badala ya vikao vya ndani, Rais hafundishwi namna ya kusema so fa masuala ya kisera na maelekezo hutolewa hadhara ili kuweka uwazi.

Kimsingi zingatieni maelekezo ya Rais vinginevyo tunahitaji -total transformation sekta ya kodi. Hata hivyo-Wito -wafanya biashara walipe kodi
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Mkuu nakubaliana na wewe 100%.Statement za Rais Samia kuhusu ukusanyaji kodi ni msumari wa mwisho katika ukusanyaji kodi na mustakali mzima wa mapato ya serikali. Rais Samia anapaswa kutambua kwamba hakuna mfanyibiashara anayependa kulipa kodi kwa hiari,kwa hiyo her soft approach ni suicide. Hii ina maana kwamba ni lazima mbinu zozote zile zitumike ili kuhakikisha kwamba wafanyibiashara wanalipa kodi,kama hawataki kulipa kwa hiari.

Niseme pia kwamba Rais Samia ana contravesial statements nyingi,hata kwenye sector ya madini,ambazo naamini baadae zitatuletea matatizo.Naomba Mungu tu kwamba statements zake hizo zisiwe zina reflect utendaji wake,otherwise it will be a disaster.

Finally ningemshauri Rais awe makini na hotuba anazotoa,they should not have contravesial statements,unless it is by design.So far tunaamini kwamba it's a slip of the tongue sio by design.
Huna point yoyote!

Pumba tupu!

Raisi Samia Suluhu Hassan hataki kodi za dhuluma.

HAKI HUINUA TAIFA
 
Ningekuwa Samia ningewabadilishia kazi TRA wote maana mmeanza kuwa na nyodo. Miaka 6 mnanyanyasa Watanzania na kujineemesha binafsi, Rais kawaambia ukweli mnajifanya kununa? Acheni kukusanya kodi, msipofikia malengo kwa ustaarabu mjue Mameneja wa mikoa na Wilaya hawana kazi instantly. Mnaanza kutikisa kiberiti kwa vile mmesemwa uovu wenu? Acheni muone kama mtabaki mlipo, allahhhh!!
Na wewe unawatisha kama Task Force,au wewe ni Task Force ya kutisha TRA🤣🤣🤣
 
Wewe si lolote zaidi ya mpigania legacy, wewe ni genge tu wala TRA hawawezi kuandika utopolo uliouandika hapo. Ulikuwa unaona raha sana watu kufunga biashara na kuwa masikini kama wewe ,unaposikia hali ya hewa nzuri inakuja upande wao ndipo sasa roho yako mbaya inakuuma.

Mama Samia hakutoa maelekezo ya kuacha kulipa kodi,, kama TRA hawakusanyi kodi huo ni udhaifu wao na wanapaswa kuwajibishwa.

Ila nakufahamu msimamo wako umekaa upande wa kutetea ule ukatili uliokuwa unakulisha wewe na familia yako.
Uovu wenu wa kunyanyasa watu umekwisha,, nenda katubu umrudie Muumba wako.
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji106]
 
Kama wewe ni mwislamu, jioni pata futari nutalipa. Kama mkristu pata soda weekend imeanza.

Hawa watu ni wajinga Sana na wanajifanya wasahaulifu. Wanamtukuza mtu aliyekuja kuharibu uchumi wetu kwa kukosa mipango sahihi na kutosikia ushauri
Mwendazake adi magari ya kuchukua maiti alitaka yawe na EFD machine eti ni vyanzo vya kodi na hili ni alipoona Corona inaua sana yule mzee dah
 
Asilimia 20% tu ya walipa kodi ndiyo huleta 80% ya mapato yote. Hao ndiyo una deal nao kama Twiga Cement, TCC, TBL, BAKHRESSA, MODEWJI, IPP etc. Hawa akina kajamba nani waliobakia ambao ni 80% wanachangia 20% tu ya mapato ambao ni vituo vya petrol station, maduka ya Kariakoo, mabaa, guest house, mabasi etc.
Observation makini kabisa. Wafanyaji Biashara wadogo wakipangiwa kodi rafiki bila shaka watalipa,hili limedhibitika nchi ya jirani.
 
Akili za watanzania waachie wenyewe ipe wakati miezi michache mbele utaona mada humu za watu kulalamika mishahara imechelewa na hiyo miradi kama inategemea mikopo kuna phase zitasimama kwa sababu soon tutakuwa atuaminiki tena na wakopeshaji.

Wala sio uganga hilo jambo linakuja soon, mama anadhani maswala ya kodi ni mzaha mzaha, wa kusikiliza story za kwenye social media.
Mama hataki kodi za dhuluma. Period.

HAKI HUINUA TAIFA
 
Miaka mitano ya Magufuli atujaona IMF wala WB kuja kukutana na wizara ya fedha kisa wasiwasi wa nchi kuweza kulipa madeni yake kutokana na makusanyo madogo ya kodi kama ilivyozoeleka zama za JK. If anything walikuwa hawana shida kumkopesha.

Huko baadae mambo yakienda mrama wasitafute mchawi mwingine Magufuli sijui alikopa sana, la hasha matatizo haya wakubali tu huko mbele wameyatengeneza wao.
Unawaza kizamanizamani! Pole!

Mama hataki kodi za dhuluma

HAKI HUINUA TAIFA
 
Labda nikuulize swali mkuu,umetumia njia zote za kiungwana ili mfanyibiashara alipe kodi na halipi,what do you do,a straight answer please.

Unajua,nilitegemea Rais asisitizie juu ya umuhimu wa wafanyibiashara kulipa kodi kama sheria inavyowataka kufanya.Then nilitegemea aseme kwamba kwa mfanyi biashara yeyote ambaye hatapenda kulipa kodi kwa hiari,sheria itachukua mkondo wake,kwa kuwa zipo sheria.

Mkuu huwezi kumbembeleza mfanyibiashara asiyetaka kulipa kodi kwa hiari.Ukimbembeleza hata lipa.Lazima sheria zimbane ili alipe.
Hizo zama zenu za kutumia ubabe na nguvu kukusanya kodi za dhuluma zimepita! Tambueni kwamba hizi ni zama mpya za serikali ya kutumia akili na weledi!

TRA wanajua how to be professional. Na kodi ya kutosha itakusanya kwa weledi.

HAKI HUINUA TAIFA
 
Sikubaliani na mfumo wa kuwaumiza walipa kodi hasa wafanyabiashara wakati na wakubwa kwa sababu tu ya kwenda kufanya dili za kununa mandege na mareli ili wazungu na matajiri wanaotoka Ulaya wapande kwa bei rahisi nabiuwaumiza watanzania wa kawaida wenye vifuso vyao na kirikukuu za kubeba viazi kutokea mbea na kwengineko.

Hivi huoni kuwa awamu ya tano ilikua inawaumiza watu wanaojitafutia fedha wenyewe huku ikitumia fedha nyingi kununua wapinzani na kulipa mamishahara makubwa wakurugenzi wa Tarura,TRA ,Bandari,Tanapa, Sumatra, Ewura, Tanroad na wabunge, mawaziri huku wakiwa hawazalishi chochote zaidi ya kuwaumiza wafanyabiashara ili wao waishi maisha ya kifahari kwa mishahara mikubwa na rushwa nono.
Mwacheni mama Samia afanye kazi aliyotumwa na Mungu kuwafariji watanzania walioletwa duniani kuifurahia dunia kwa haki sio kuumizana kwa sababu ya kujenga masanamu na mapiramidi yasiyo na uhai wala roho wala hayajui kumsifu na kushukuru Mungu.

Unashangaa nini kuona mtaji mkubwa unatoa faida ndogo?
Mbona ATCL ina mtaji wa matrilion ya fedha lakini haipati faida ?

Kama mtu hatoi risiti sheria si ipo afikishwe mahakamani kama anakaidi sio kwenda kufunga akaunti zake na kuiba fedha zake huku mkifikisha kidogo mnakojua na nyingine kuweka mifukoni mwenu.
Nani anajua mlikopelela fedha zote mlizokwapua kwa wafanyabiashara ? Je, mlitoa risiti au Tax clearance kwa wenyewe hasa wale waliokufa kwa presha.

Tusimamie sheria kwa haki na kuongeza wigo wa walipa kodi.
 
Huyu mleta hoja unaweza kudhani ni raia mwenye nia njema! Lakini huyu anaweza kuwa mmoja wa watumishi vi.laza wa TRA waliokuwa wanapata rushwa kubwa kutokana na mfumo haramu wa Task force kukusanya kodi! Mhe .Rais Mama Samia kuwa macho sana na hawa "_Majambazi" waliojificha TRA.
Kodi ni sheria (Tax law Act) ,kila kitu kuhusu aina za mapato( taxable income) zimeainishwa vizuri na namna ya kutoza kodi! Sasa shida inakuja wapi kama sheria hiyo inafuatwa?!
Huyu ni mmoja wa watoza kodi walioxoea kutumia NGUVU badala ya AKILI!
Sasa anaona mfumo uliokuwa unawapa rushwa kubwa kubwa unakufa na wao walishazoea kujinufaisha!
Cha msingi sana wigo wa walipakodi uongezeke( tax base) na sheria ya kodi ifuatwe, kodi itakusanywa kwa wingi tu na malengo ya trillion 2 kwa mwezi yatafikiwa.

Kunyanyasa wafanyabiashara kwa vitisho na ubabe siyo njia endelevu ya kuongeza mapato ya Serikali.
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Sio kweli, tuwe tunaandika Vitu vyenye uhalisia. ungeweka ushahidi wa mfanyabiashara aliyedaiwa kodi akagoma au akakataa kutoa risiti. Tusizushe mambo kwa faida zetu binafsi

Chief, kweli unadhani it’s that easy kutoa “evidence” ya mkwepa kodi mashuhuri?

Unakumbuka issue ya watu wa oil ambayo ilimeletea Chief Max kadhia ya mahakamani mpaka leo?

Speechless!
 
Acha kiherehere mkuu. Wafanyabiashara wasisumbuliwe kabisa.
 
Kulipa kodi ni takwa la sheria, hao wafanyabiashara wanatakiwa kulipa kodi kutimiza wajibu wao, wakigoma wacha sheria ichukue mkondo wake, hao maafisa wa TRA unaosema wameamua kukaa pembeni kwa kuogopa kubagazwa ni wazembe wanatakiwa kuadhibiwa.
👊👊
 
Mhe Rais, naomba utumie dakika chache kusoma barua hii wewe mwenyewe, na kama hautapata muda naomba wasaidizi wako wakusaidie kuusoma na kukufikikishia.

Naandika haya kama Raia aliye na wasiwasi baada ya kutafakari kwa kina juu ya "TONE" yako uliyokwishaitoa hadharani kuhusu taasisi hii nyeti inayokusanya mapato ya nchi.

Pia ni baada ya kukaa na baadhi ya maafisa kodi ambao wanakiri kwamba toka kauli yako kazi yao imekuwa ngumu kupindukia ni kama wamewekwa benchi!

Mhe. Rais, kwa sasa kuna mambo makuu mawili yanayotokea ambayo sidhani kama umeshayajua.

i) Wafanyabiashara wameacha kutoa risiti za EFD na ukiwadai wanasema kabisa WASISUMBULIWE maana Rais wao ameshatoa maelekezo hayo. Wapo HOLIDAY!

Hata TRA wenyewe wamecancel mazoezi ya ku-enforce utoaji risiti. Maana wanajua wakienda watabagazwa!

Swali kubwa hapa, Je, Kodi gani itakusanywa na nchi bila watu kutoa risiti? Unawezaje kutrack mauzo ya mlipa kodi bila kutoa risiti ya EFD?

ii) Wafanyabiashara hawapeleki tena malipo ya kodi kwa kama kasi ya awali, kila mmoja ameset mind ya kupinga kodi maana anaona kama kile alichokadiriwa si sahihi baada ya kauli ya Rais.

Wataalam wenyewe wanasema impact yake itaonekana katika taarifa za mapato mwezi huu na ijayo!

Mhe Rais, katika taasisi zote chini yako zinazohitaji Top Level Presidential Support ya moja kwa moja ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Bila TRA yenye support ya Rais, Taifa linakufa, na hakika litashindwa kufikia malengo yake.

Ni sawa na katika taasisi za kawaida, kitengo ambacho kinaleta mapato kwa taasisi, ndicho Mkurugenzi Mkuu hukitolea macho na kukipa support yote inayohitajika ili aweze kufikia malengo yake kibiashara.

Mhe Rais, sitaki kurejea katika maagizo yako ya nyuma kuhusu namna TRA wanavyofanya kazi ambayo uliyatoa hadharani, ila ningekuwa mmoja wa washauri wako ningeshauri usiongee sentensi zile hadharani bali uongee moja kwa moja na Viongozi na Wafanyakazi wa TRA indoors.

Kwa nini??. Kwa sababu nature ya mfanyabiashara ni kulalamika na kuficha mapato yake halisi. Hakuna mfanyabiashara hata mmoja aliye genuine ya kipato chake, Popote duniani. Hakuna!

Mhe. Rais, unaweza kukuta mfanyabiashara anafanya biashara yenye mauzo ya Billioni 2 anadeclare faida ya milioni 4, Seriously?

Katika mazingira hayo unahitaji Taasisi yenye nguvu na mamlaka ili iweze kutafuta wapi mtu huyu alipodanganya ili Serikali iweze kukusanya kodi yake. Otherwise, utachukua hio hio Milioni 4 alafu maisha yanaendelea wakati kwa hakika labda mtu huyo alipaswa kulipa milioni 50.

Mwisho:
Natambua kupitia maneno ya Makamu wako, Mhe. Mpango, umeweka malengo ya Trillion 2 kwa Mwezi, lakini ukweli ni kwamba hata kama sheria zitabadilika na baadhi ya kodi kupungua lazima kuna nyingine zitapanda ili kufikia lengo la Trillion 2. Sasa nani atatumika kuenforce ukusanyaji huo? Je ni hao hao TRA? Je wataweza ku-enforce huo ukusanyaji bila support yako? Au kuna watu wanaku-sabotage ili ushindwe kufikia malengo hayo?

Naomba kuhitimisha kwa kukushukuru kwa muda wako.

Wako,
Raia aliye na wasiwasi.
15 April, 2021

Nyongeza muhimu kutoka kwa baadhi ya wadau 👇








Postscriptum (PS): Kuna baadhi ya wachangiaji katika uzi huu wana attack mleta mada wakisema alikuwa mnufaika wa utaratibu wa awali i.e mfanyakazi TRA, alikuwemo kwenye taskforce n.k.

Inasikitisha sana pale mtu badala ya kusikiliza na kuijibu hoja anadhani wewe ni mnufaika, umehongwa, kibaraka sababu tu umenena jambo tofauti na aloamini. Ni legacy mbaya sana hii.

Niseme tu, mimi sio mfanyakazi wa TRA na sio mnufaika wa mfumo. ILA nimetoa experience yangu baada ya kuona realities mtaani (mfano suala la risiti limenikuta mimi kama mimi si mara moja) na pia katika mijadala yetu sisi wananchi pamoja na maoni ya baadhi ya maafisa wa TRA ambao tupo nao mitaani maana nao ni binadamu wa kawaida tunaishi nao.

So in simple terms, I did this not for any personal gain rather, I decided not to keep quite for National Interest.
Mimi ni miongoni mwa pro-Magufuli kindakindaki na niliyeamini na bado naamini katika sera za Magufuli nyingi. Ila miongoni mwa vitu vilivyonipa/vinavyonipa ukakasi katika utawala wa Magufuli ni inshu ya kodi na nifafanue.

Naamini katika kodi na ni lazima kila mfanyabiashara na wafanyakazi tulipe kodi. Tusipolipa kodi nchi yetu tuipendayo itajengwaje? Lakini kuna suala la kulipa kodi na kuna suala la unyanganyi katika kodi. Mtazamo wangu katika kodi ni kwamba kodi anazostahili kulipa mfanyabiashara au mfanyakazi ni zile kodi za msingi na zinazolipika. Mfanyabiashara hawajibiki kwa serikali peke yake, anawajibika pia kwake mwenyewe, kwa familia yake, kwa wafanyakazi anaopaswa kuwalipa mshahara, rejeshi benki kama amechukua mkopo na wakati huo huo ahakikishe biashara yake haifi bali ikue siku hadi siku.

Mama Samia alishauri TRA wajiongeze katika kupanua tax base badala ya kuwakomalia wafanyabiashara hao hao. Ng'ombe unaye mmoja, huyo huyo unamkamua hadi damu, hutaki kuongeza ng'ombe wengine, si atakufa huyo? Maana ya kuongeza tax base ni kwa TRA kuwa wabunifu na kuhakikisha inatengeneza au kuwafikia walipa kodi wengi badala ya kujikita tu kuwafuata walipa kodi hao hao tu.

Mimtu ya TRA ni miongoni mwa wafanyakazi wazembe sijapata kuona. Yaani yenyewe inajua kukaa kwenye computer na kukadiria watu kodi tu wale wafanyabiashara wa mjini walio karibu karibu na ofisi za TRA. Ukiwa mfanyabiashara wa ndani ndani huko pembezoni ambako TRA hawajiongezi kufika (watafikaje na mitambi yao?) labda ujipendekeze mwenyewe kujipeleka TRA kulipa kodi. Hiyo ndiyo maana ya kuongeza tax base. Hii nchi ina watu milioni 60, haikufutwa kodi ya kichwa ili mzigo uwaelemee vichwa vichache.

Kama tunajenga nchi moja tukubaliane kwamba watu tulipe kodi wote lakini inayolipika. Serikali pia ijue kwamba kodi ni jasho la watu. Hatulipi kodi ili itafunwe na matakataka yaliyomo serikalini kwa kujinunulia magari ya kifahari, kujilipa miposho na mishahara minono. Nina uhakika kwamba kuongeza tax base pia ni kutumia kodi kwa matumizi sahihi katika huduma bora kwa walipa kodi. Utamshawishi vipi mfanyabiashara kulipa kodi kwa moyo wakati barabara zinazotengenezwa hazifiki mwaka zinaanza kuharibika?
 
Back
Top Bottom