Nilibahatika kufanya kazi kwenye crew yake,hapahapa bongo,nakumbuka ilikuwa 2007,alikuja ku shoot na wakapiga kambi arusha,walikodi magari yetu mawili na mimi nikawa naendesha mojawapo,ila kwa wiki takriban mbili walizokuwa hapo nilibahatika kumwona mara mbili tu,siku kadhaa baada ya kuja na siku wanavunja kambi,jamaa yupo simple sana,alikuja kutusalimu na kutuaga,akaisifia sana Tanzania na kuahidi kurudi tena,mwisho tulienda naye kutembelea kiwanda cha nguo cha AtoZ na alipotoka hapo akasepa zake airport kurudi marekani,tulipiga naye picha kadhaa za pamoja,mwingine niliyebahatika kuwa naye kwa karibu ni jamaa anaitwa BONO huyu alikuwa kiongozi na mpiga gita wa kundi la U2,huyu tulizurura naye kwa siku tatu,yeye alikuwa ni balozi wa WHO kwa kanda ya afrika,aliniachia na vijizawadi kadha wa kadha.