KERO Open University wamefanya suala la Research kuwa kitega uchumi, Supervisor anataka kutumia El Nino kunipressure nimlipe TZS 250,000 ili nimalize chuo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

migomigokwetu

Senior Member
Joined
Sep 27, 2026
Posts
106
Reaction score
70
Hii si hadithi ya kusimuliwa bila ushahidi, nina vielelezo vinavyothibitisha ninachokizungumza.

Nimekuwa nikijiuliza kama niwashirikishe hapa kwa kuwa wahusika wanaonekana kuwa na kiburi na hawajali malalamiko ya wanafunzi, nimeamua pia kuweka wazi suala hili kupitia mitandao mingine kama Instagram na TikTok ili ukweli ufahamike.

Jambo hili si geni. Inaonekana baadhi ya wanafunzi wamezoea hali hii na wameamua kulikubali kwa sababu wanataka kumaliza masomo yao. Lakini kwangu binafsi, siwezi kuona ni jambo la kawaida kuomba pesa kwa msimamizi wangu wa utafiti (Supervisor) ili niweze kuendelea na utafiti wangu na hatimaye kumaliza chuo.

Kuna utaratibu unaodaiwa kuwepo miongoni mwa baadhi ya wasimamizi wa utafiti katika Chuo Kikuu Huria, ambapo wanafunzi hucheleweshwa kukamilisha tafiti zao hadi kipindi cha karibu na mahafali. Upungufu huo hutumiwa kama njia ya kuwapa shinikizo wanafunzi ili walipe fedha zisizo rasmi kwa ajili ya kukamilisha masomo yao.

Bila kufanya hivyo, baadhi ya wanafunzi hudaiwa wanaweza kucheleweshwa hadi miaka miwili au mitatu. Nina ushahidi wa jambo hili, pamoja na wanafunzi wengine ambao wanaweza kuthibitisha uzoefu wao.

Kuanzia Januari hadi Septemba, baadhi ya wanafunzi hukutana na changamoto mbalimbali kutoka kwa wasimamizi wao, ikiwemo kutopokelewa simu, kuambiwa wakutane baadaye wanapofika ofisini, au kupewa marekebisho yanayorudiwa mara kwa mara bila kumaliza mchakato wa ufuatiliaji wa utafiti.

Mwezi Agosti mwaka huu, Supervisor wangu aliniambia wazi kuwa bila kumpatia Shilingi 250,000 sitaweza kumaliza chuo. Hivi karibuni pia aliniambia, "Dogo, si unaona kuna El Niño? Toa umalize."

Nilifikisha suala hili kwa Mkuu wa Idara, lakini sikupata msaada wa kuridhisha zaidi ya kuambiwa kuwa angezungumza naye. Baada ya hapo, hali imekuwa mbaya zaidi kwani hata ninapomfuata ofisini hataki kukutana na mimi.

Ninafahamu kuwa chuo kinaweza kuja kukanusha tuhuma hizi, na baadhi ya wanafunzi wameamua kukaa kimya kwa sababu wanataka kumaliza masomo yao. Lakini hili si jambo la kupuuzwa. Wanafunzi wanastahili mazingira ya haki, uwazi na msaada katika kukamilisha masomo yao bila kulazimishwa kutoa fedha zisizo rasmi.

Suala hili linahitaji uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane na hatua stahiki zichukuliwe. Sio kila Mtanzania yuko tayari kukubali hali isiyo ya haki kimya kimya.
 
Attachments

  • 38d50e7f-f12c-4de4-a360-de8861c2ff92.jpeg
    38d50e7f-f12c-4de4-a360-de8861c2ff92.jpeg
    50.8 KB · Views: 12
Pole ila Tii sheria bila shuruti hakuna hasara. Huoni hadi Nchimbi wamemnyamazisha wewe ni nani na elimu yako ya majungu hiyo?
Kwa hiyo mkuu unataka nitoe hela, jambo ambalo tuna utaratibu wa kulifanya mwenyewe kama mwanafunzi, ingekuwa mimi ndiyo naforce mazingira ni sawa. Mimi niko tayari na kuendelea na research na tumebakiza miezi miwili chuo kiishe, yeye anaforce ili niende stage inayofuata lazima nimkatie pesa.
 
Suala hili linahitaji uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane na hatua stahiki zichukuliwe. Sio kila Mtanzania yuko tayari kukubali hali isiyo ya haki kimya kimya.
Saizi nikujipigia tuu hela mianya ya Rushwa iko kila sehemu sidhani kama mchunguzwaji anepokea Rushwa ataacha kutoa Rushwa kwa mchunguzaji.
 
Wanazingua mno, mi naona nimlipue tu kesho, maana naona ananizoea, yani research nifanye tokea 2023 mpaka 2026 alafu kitu, amenizungusha kinoma alafu mwisho wa siku anakuja kunichana kiutani utani tu. Naweka picha, screenshots, na recordings Instagram na Tiktok, atajua mwenyewe

N.B: Mwaka 2024 nilipata ajali nikakaa nyumbani
 
Pole mkuu hao wanalindana hamna cha maana.
 
Lazima nideal nao , wao ni wanajisifu kwamba wanaamua nani amalize nani asimalize
 
Mkuu afadhali umeliweka wazi humu jamvini jambo lako. Ukweli ni kuwa vyuo vikuu karibu vyote vya Tanzania vimekuwa vya hovyo sana siku hizi

Ukiwauliza wanafunzi ambao wanasoma shahada za kwanza utasikia habari za kusikitisha sana Hadi unajiuliza kumetokea nini hapa nchini mpaka wahadhiri wa vyuo vikuu wamegeuka watu wa kuomba omba pesa au rushwa za pesa kutoka Kwa wanafunzi kiasi hiki?

Wanafunzi wanauziwa vitini Kwa lazima, Wanachangishwa fedha Kwa lazima na mhadhiri ili wawape alama za ufaulu mzuri ktk mitihani etc.

Kwa Hali ilipofikia TCU inapaswa kuwajibishwa Kwa kushindwa kusimamia vizuri elimu ya juu. Hali hii ikiachwa tutegemee wasomi vihiyo huko mbele ya safari.
 
UDSM hakuna research kwa degree ya kwanza inakuaje hao OPEN wawe na research??

Wizi mtupu!!
 
Hii si hadithi ya kusimuliwa bila ushahidi, nina vielelezo vinavyothibitisha ninachokizungumza.

Nimekuwa nikijiuliza kama niwashirikishe hapa kwa kuwa wahusika wanaonekana kuwa na kiburi na hawajali malalamiko ya wanafunzi, nimeamua pia kuweka wazi suala hili kupitia mitandao mingine kama Instagram na TikTok ili ukweli ufahamike.

Jambo hili si geni. Inaonekana baadhi ya wanafunzi wamezoea hali hii na wameamua kulikubali kwa sababu wanataka kumaliza masomo yao. Lakini kwangu binafsi, siwezi kuona ni jambo la kawaida kuomba pesa kwa msimamizi wangu wa utafiti (Supervisor) ili niweze kuendelea na utafiti wangu na hatimaye kumaliza chuo.

Kuna utaratibu unaodaiwa kuwepo miongoni mwa baadhi ya wasimamizi wa utafiti katika Chuo Kikuu Huria, ambapo wanafunzi hucheleweshwa kukamilisha tafiti zao hadi kipindi cha karibu na mahafali. Upungufu huo hutumiwa kama njia ya kuwapa shinikizo wanafunzi ili walipe fedha zisizo rasmi kwa ajili ya kukamilisha masomo yao.

Bila kufanya hivyo, baadhi ya wanafunzi hudaiwa wanaweza kucheleweshwa hadi miaka miwili au mitatu. Nina ushahidi wa jambo hili, pamoja na wanafunzi wengine ambao wanaweza kuthibitisha uzoefu wao.

Kuanzia Januari hadi Septemba, baadhi ya wanafunzi hukutana na changamoto mbalimbali kutoka kwa wasimamizi wao, ikiwemo kutopokelewa simu, kuambiwa wakutane baadaye wanapofika ofisini, au kupewa marekebisho yanayorudiwa mara kwa mara bila kumaliza mchakato wa ufuatiliaji wa utafiti.

Mwezi Agosti mwaka huu, Supervisor wangu aliniambia wazi kuwa bila kumpatia Shilingi 250,000 sitaweza kumaliza chuo. Hivi karibuni pia aliniambia, "Dogo, si unaona kuna El Niño? Toa umalize."

Nilifikisha suala hili kwa Mkuu wa Idara, lakini sikupata msaada wa kuridhisha zaidi ya kuambiwa kuwa angezungumza naye. Baada ya hapo, hali imekuwa mbaya zaidi kwani hata ninapomfuata ofisini hataki kukutana na mimi.

Ninafahamu kuwa chuo kinaweza kuja kukanusha tuhuma hizi, na baadhi ya wanafunzi wameamua kukaa kimya kwa sababu wanataka kumaliza masomo yao. Lakini hili si jambo la kupuuzwa. Wanafunzi wanastahili mazingira ya haki, uwazi na msaada katika kukamilisha masomo yao bila kulazimishwa kutoa fedha zisizo rasmi.

Suala hili linahitaji uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane na hatua stahiki zichukuliwe. Sio kila Mtanzania yuko tayari kukubali hali isiyo ya haki kimya kimya.
Una u lissu lissu fulani ivi! Safi sana kaza mwanangu hadi kieleweke usitoe hiyo hela
 
Mkuu afadhali umeliweka wazi humu jamvini jambo lako. Ukweli ni kuwa vyuo vikuu karibu vyote vya Tanzania vimekuwa vya hovyo sana siku hizi

Ukiwauliza wanafunzi ambao wanasoma shahada za kwanza utasikia habari za kusikitisha sana Hadi unajiuliza kumetokea nini hapa nchini mpaka wahadhiri wa vyuo vikuu wamegeuka watu wa kuomba omba pesa au rushwa za pesa kutoka Kwa wanafunzi kiasi hiki?

Wanafunzi wanauziwa vitini Kwa lazima, Wanachangishwa fedha Kwa lazima na mhadhiri ili wawape alama za ufaulu mzuri ktk mitihani etc.

Kwa Hali ilipofikia TCU inapaswa kuwajibishwa Kwa kushindwa kusimamia vizuri elimu ya juu. Hali hii ikiachwa tutegemee wasomi vihiyo huko mbele ya safari.
Mpaka sasa wamenipotezea zaidi ya miaka 6, na tokea 2023 nafanya hiyo research, nilipause 2024 nilipata ajali,mke wangu alikwenda kutoa taarifa kwa idara yangu, alafu leo mtu anakuja tu kukuambia umpe hela. Hawa naende nao kihuni na chuo sihami
 
Kamripoti TAKUKURU.
Nilitaka kuziweka mitindaoni taarifa zake, ila ngoja nianze huku. Chuo kama chuo hakijawahi kuwa msaada, nishasumbuana na mkuu wa Idara zaidi ya mara 3 anibadilishie supervisor kwasababu unaona kabisa anakupotezea muda
 
Una u lissu lissu fulani ivi! Safi sana kaza mwanangu hadi kieleweke usitoe hiyo hela
Hawa wamezoea, na baada ya kesi yangu kwenda viral watu wanaobisha kuhusu hili jambo watakuja kusoma comments za wanafunzi waliopitia pale. Huwa najilaumu sana kuapply kile chuo, ni vile mishemishe zangu za mjini ngumu sana kukaa darasani.

Kesho naaza TAKUKURU, nikiona hawachukulii kiuzito, atajikuta mitandaoni, nitalipia mpaka matangazo
 
Back
Top Bottom