KERO Open University wamefanya suala la Research kuwa kitega uchumi, Supervisor anataka kutumia El Nino kunipressure nimlipe TZS 250,000 ili nimalize chuo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hawa wamezoea, na baada ya kesi yangu kwenda viral watu wanaobisha kuhusu hili jambo watakuja kusoma comments za wanafunzi waliopitia pale. Huwa najilaumu sana kuapply kile chuo, ni vile mishemishe zangu za mjini ngumu sana kukaa darasani.

Kesho naaza TAKUKURU, nikiona hawachukulii kiuzito, atajikuta mitandaoni, nitalipia mpaka matangazo
Tanzania asilimia kubwa ya watu ni waongo, wezi na wala rushwa. Huko vyuoni ndiyo kabisaa. Imekuwa kama viwanda. Ni matokeo ya kuwa na viongozi wahuni. Kama rais au mkuu wa majeshi au usalama anaweza kupora fedha na kununua magari ya kifahari halafu watu wanapohoji wanauawa unategemea nini kwa watu wa chini? PS: USI-COMMENT CHOCHOTE KUHUSU MCHANGO WANGU, UNAWEZA KUJIKUTA KWENYE MATATIZO ZAIDI.
 
Hawa wamezoea, na baada ya kesi yangu kwenda viral watu wanaobisha kuhusu hili jambo watakuja kusoma comments za wanafunzi waliopitia pale. Huwa najilaumu sana kuapply kile chuo, ni vile mishemishe zangu za mjini ngumu sana kukaa darasani.

Kesho naaza TAKUKURU, nikiona hawachukulii kiuzito, atajikuta mitandaoni, nitalipia mpaka matangazo
Shikiria hapo hapo mwanangu me mwenyewe ni muhanga sema mimi ilikuwa tofauti kidogo mimi nilikuwa naingia class mwalimu miyeyusho hatari kuna muda haji kufunddisha anatufundisha lab technician alomaliza form four! na hapo coz ni anatomy and physiology mimi nilikataa kitendo hicho ndio mwanzo wa matatizo nikawa nakatwa marks ovyo ovyo!
 
Mpaka sasa wamenipotezea zaidi ya miaka 6, na tokea 2023 nafanya hiyo research, nilipause 2024 nilipata ajali,mke wangu alikwenda kutoa taarifa kwa idara yangu, alafu leo mtu anakuja tu kukuambia umpe hela. Hawa naende nao kihuni na chuo sihami
We nenda nao hadi mwisho uenda mwanangu wewe unakomboa wengi degree uchwara bora usiipate ila unyooshe washenzi
 
Kwa hiyo mkuu unataka nitoe hela, jambo ambalo tuna utaratibu wa kulifanya mwenyewe kama mwanafunzi, ingekuwa mimi ndiyo naforce mazingira ni sawa. Mimi niko tayari na kuendelea na research na tumebakiza miezi miwili chuo kiishe, yeye anaforce ili niende stage inayofuata lazima nimkatie pesa.
Hakuna chuo duniani cha ******* kama open, me msema ukweli hao walimu wenu ni takataka sijawahi ona kila mtu analalamika hivyo hivyo aisee sasa si wakifunge tu tujue moja..
 
Hawa wamezoea, na baada ya kesi yangu kwenda viral watu wanaobisha kuhusu hili jambo watakuja kusoma comments za wanafunzi waliopitia pale. Huwa najilaumu sana kuapply kile chuo, ni vile mishemishe zangu za mjini ngumu sana kukaa darasani.

Kesho naaza TAKUKURU, nikiona hawachukulii kiuzito, atajikuta mitandaoni, nitalipia mpaka matangazo
Kama unamsg zake screenshot ziweke live huko na majina yake uyaweke alafu lipia matangazo Kwa wale majamaa wanoko kuliko wote huko Instagram na TikTok na kote alafu watag wizara husika ili wajitekebishe chuo gani kila mtu analalamika me nilivyokuwa sio mvumilivu na najua kufuata Sheria nisingevumilia kuna siku wangesikia nimemlamba mtu makofi...wangese sana walimu wa hapo.
 
We nenda nao hadi mwisho uenda mwanangu wewe unakomboa wengi degree uchwara bora usiipate ila unyooshe washenzi
Lazima niwakazie, tunapoteza ajira kibao kisa kukosa cheti/transcript alafu wewe unashinda chuo kisa research? Nani anafanya research miaka yote hiyo level ya bachelor's degree?
 
Kama unamsg zake screenshot ziweke live huko na majina yake uyaweke alafu lipia matangazo Kwa wale majamaa wanoko kuliko wote huko Instagram na TikTok na kote alafu watag wizara husika ili wajitekebishe chuo gani kila mtu analalamika me nilivyokuwa sio mvumilivu na najua kufuata Sheria nisingevumilia kuna siku wangesikia nimemlamba mtu makofi...wangese sana walimu wa hapo.
Yeah lazima niwakazie, sema ngoja nianzie Takukuru kwanza, nikiona nako hakuelewekieleweki, namalizia mazima. Kuna mwenzangu mmoja naye amekubali twende wote, ana kesi kama yangu. Kwasababu uongozi wote wa chuo unajua kinachoendelea, najua kuongea nao kistaarabu haitosaidia na hakuna mabariko yoyote yatatokea
 
Jichunge dogo yasije yakakukuta ya yule mwamba mmoja alikuwa T.O akaishia kuwa Mwalimu wa twisheni mchikidown wanafunzi wake akawa anatuita NYUMBU🥹🥹Naskia yeye aliminywa UDSM
 
Mkuu mpe tuu hiyo 250k wala sio issue
 
Mkuu mpe tuu hiyo 250k wala sio issue
Lazima nimkazie, nitawapa feedback, nina ushahidi wote, yani yeye hana angle ya kujitetea, liwalo na liwe. Huyu mzee ukiachana na research kwenye anatoaga marks za ajabu, ukimuuliza anasema tu "hamjui kujibu maswali".

Tumeshakaa naye vikao, tumekaa vikao na idara mzima, bahati mbaya nikapangiwa yeye kuwa supervisor wangu. Yeye huwa anajisifu bila mimi hakuna anayemaliza chuo. Tutaonana.

Mimi nitakuja na feedback hapo au unaweza kukutana na habari kwenye page za Jamiiforums au hata Millard Ayo, nitawakazia. Ningekuwa nimemuomba marks, au ninatengeneza mazingira ya uvivu na kutotaka kufanya kazi, ningemlia buyu na kukubali ila kwa hili,HAPANA
 
Jichunge dogo yasije yakakukuta ya yule mwamba mmoja alikuwa T.O akaishia kuwa Mwalimu wa twisheni mchikidown wanafunzi wake akawa anatuita NYUMBU🥹🥹Naskia yeye aliminywa UDSM
Hana cha kufanya, nitakuja na feedback ngoja nianze na TAKUKURU
 
Hii si hadithi ya kusimuliwa bila ushahidi, nina vielelezo vinavyothibitisha ninachokizungumza.

Nimekuwa nikijiuliza kama niwashirikishe hapa kwa kuwa wahusika wanaonekana kuwa na kiburi na hawajali malalamiko ya wanafunzi, nimeamua pia kuweka wazi suala hili kupitia mitandao mingine kama Instagram na TikTok ili ukweli ufahamike.

Jambo hili si geni. Inaonekana baadhi ya wanafunzi wamezoea hali hii na wameamua kulikubali kwa sababu wanataka kumaliza masomo yao. Lakini kwangu binafsi, siwezi kuona ni jambo la kawaida kuomba pesa kwa msimamizi wangu wa utafiti (Supervisor) ili niweze kuendelea na utafiti wangu na hatimaye kumaliza chuo.

Kuna utaratibu unaodaiwa kuwepo miongoni mwa baadhi ya wasimamizi wa utafiti katika Chuo Kikuu Huria, ambapo wanafunzi hucheleweshwa kukamilisha tafiti zao hadi kipindi cha karibu na mahafali. Upungufu huo hutumiwa kama njia ya kuwapa shinikizo wanafunzi ili walipe fedha zisizo rasmi kwa ajili ya kukamilisha masomo yao.

Bila kufanya hivyo, baadhi ya wanafunzi hudaiwa wanaweza kucheleweshwa hadi miaka miwili au mitatu. Nina ushahidi wa jambo hili, pamoja na wanafunzi wengine ambao wanaweza kuthibitisha uzoefu wao.

Kuanzia Januari hadi Septemba, baadhi ya wanafunzi hukutana na changamoto mbalimbali kutoka kwa wasimamizi wao, ikiwemo kutopokelewa simu, kuambiwa wakutane baadaye wanapofika ofisini, au kupewa marekebisho yanayorudiwa mara kwa mara bila kumaliza mchakato wa ufuatiliaji wa utafiti.

Mwezi Agosti mwaka huu, Supervisor wangu aliniambia wazi kuwa bila kumpatia Shilingi 250,000 sitaweza kumaliza chuo. Hivi karibuni pia aliniambia, "Dogo, si unaona kuna El Niño? Toa umalize."

Nilifikisha suala hili kwa Mkuu wa Idara, lakini sikupata msaada wa kuridhisha zaidi ya kuambiwa kuwa angezungumza naye. Baada ya hapo, hali imekuwa mbaya zaidi kwani hata ninapomfuata ofisini hataki kukutana na mimi.

Ninafahamu kuwa chuo kinaweza kuja kukanusha tuhuma hizi, na baadhi ya wanafunzi wameamua kukaa kimya kwa sababu wanataka kumaliza masomo yao. Lakini hili si jambo la kupuuzwa. Wanafunzi wanastahili mazingira ya haki, uwazi na msaada katika kukamilisha masomo yao bila kulazimishwa kutoa fedha zisizo rasmi.

Suala hili linahitaji uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane na hatua stahiki zichukuliwe. Sio kila Mtanzania yuko tayari kukubali hali isiyo ya haki kimya kimya.
Mwbie akupe control number
 
Nilifikisha suala hili kwa Mkuu wa Idara, lakini sikupata msaada wa kuridhisha zaidi ya kuambiwa kuwa angezungumza naye. Baada ya hapo, hali imekuwa mbaya zaidi kwani hata ninapomfuata ofisini hataki kukutana na mimi.
Kwa hiyo ulienda kunishitaki siyo? Basi tutaona nani bingwa kati yangu na wewe!
 
Tatizo ni mtawala aliyepo madarakani, kwa sasa kila taasisi ya serikali imeoza.
Nina kijana wangu nilipeleka VETA Tanga kujifunza udereva wameambiwa watoe (50000)- wapewe vyeti bila ukaguzi wa polisi na wametoa.
Rais kasema wale kwa urefu wa kamba zao.
 
Back
Top Bottom