KERO Open University wamefanya suala la Research kuwa kitega uchumi, Supervisor anataka kutumia El Nino kunipressure nimlipe TZS 250,000 ili nimalize chuo

KERO Open University wamefanya suala la Research kuwa kitega uchumi, Supervisor anataka kutumia El Nino kunipressure nimlipe TZS 250,000 ili nimalize chuo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hii si hadithi ya kusimuliwa bila ushahidi, nina vielelezo vinavyothibitisha ninachokizungumza.

Nimekuwa nikijiuliza kama niwashirikishe hapa kwa kuwa wahusika wanaonekana kuwa na kiburi na hawajali malalamiko ya wanafunzi, nimeamua pia kuweka wazi suala hili kupitia mitandao mingine kama Instagram na TikTok ili ukweli ufahamike.

Jambo hili si geni. Inaonekana baadhi ya wanafunzi wamezoea hali hii na wameamua kulikubali kwa sababu wanataka kumaliza masomo yao. Lakini kwangu binafsi, siwezi kuona ni jambo la kawaida kuomba pesa kwa msimamizi wangu wa utafiti (Supervisor) ili niweze kuendelea na utafiti wangu na hatimaye kumaliza chuo.

Kuna utaratibu unaodaiwa kuwepo miongoni mwa baadhi ya wasimamizi wa utafiti katika Chuo Kikuu Huria, ambapo wanafunzi hucheleweshwa kukamilisha tafiti zao hadi kipindi cha karibu na mahafali. Upungufu huo hutumiwa kama njia ya kuwapa shinikizo wanafunzi ili walipe fedha zisizo rasmi kwa ajili ya kukamilisha masomo yao.

Bila kufanya hivyo, baadhi ya wanafunzi hudaiwa wanaweza kucheleweshwa hadi miaka miwili au mitatu. Nina ushahidi wa jambo hili, pamoja na wanafunzi wengine ambao wanaweza kuthibitisha uzoefu wao.

Kuanzia Januari hadi Septemba, baadhi ya wanafunzi hukutana na changamoto mbalimbali kutoka kwa wasimamizi wao, ikiwemo kutopokelewa simu, kuambiwa wakutane baadaye wanapofika ofisini, au kupewa marekebisho yanayorudiwa mara kwa mara bila kumaliza mchakato wa ufuatiliaji wa utafiti.

Mwezi Agosti mwaka huu, Supervisor wangu aliniambia wazi kuwa bila kumpatia Shilingi 250,000 sitaweza kumaliza chuo. Hivi karibuni pia aliniambia, "Dogo, si unaona kuna El Niño? Toa umalize."

Nilifikisha suala hili kwa Mkuu wa Idara, lakini sikupata msaada wa kuridhisha zaidi ya kuambiwa kuwa angezungumza naye. Baada ya hapo, hali imekuwa mbaya zaidi kwani hata ninapomfuata ofisini hataki kukutana na mimi.

Ninafahamu kuwa chuo kinaweza kuja kukanusha tuhuma hizi, na baadhi ya wanafunzi wameamua kukaa kimya kwa sababu wanataka kumaliza masomo yao. Lakini hili si jambo la kupuuzwa. Wanafunzi wanastahili mazingira ya haki, uwazi na msaada katika kukamilisha masomo yao bila kulazimishwa kutoa fedha zisizo rasmi.

Suala hili linahitaji uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane na hatua stahiki zichukuliwe. Sio kila Mtanzania yuko tayari kukubali hali isiyo ya haki kimya kimya.
Kwa serikali ipi bro!!!!, alafu mdomo tayari umekuponza, bora ungekaa kimnya
 
Sikumjibu, nilijua nitamjibu vibaya angepata angle zaidi ya kujitetea, nikaenda kwa mkuu wa idara, ila naona naye kama anapuuzia, ni kama anaona poa.
Wale ni staff moja inawezekana ni michezo yao ni kama kesi ya nyani umpelekee ngedere
 
Back
Top Bottom