Maswali yako mazuri sana nitayajibu katika show mojawapo, nakuahidi.
KinachoShangaza ni kuwa watu wanataka tuamini watu wengi watamchagua Lowassa. Lakini inaonekana hawaamini hilo ni kweli. Kama ni kweli hoja zangu hazina wasikilizaji na hazimbadili yeyote hivyo ni za kupuuzia. Hampuuzii mnaomtaka Lowassa kwanini?
Nitajibu: kwa sababu hamuamini Lowassa atakubaliwa na wengi kama mnavyotamani.
Liulize hili swali kivingine..nguvu kubwa ya kumsukumizabLowassabkwa Watanzania ya nini na kwanini? Ukipata jibu la swali hili utapata na jibu lako.
KinachoShangaza ni kuwa watu wanataka tuamini watu wengi watamchagua Lowassa. Lakini inaonekana hawaamini hilo ni kweli. Kama ni kweli hoja zangu hazina wasikilizaji na hazimbadili yeyote hivyo ni za kupuuzia. Hampuuzii mnaomtaka Lowassa kwanini?
Nitajibu: kwa sababu hamuamini Lowassa atakubaliwa na wengi kama mnavyotamani.
Mkuu MM,
Unapoteza mwanya na hii digital operation. Labda ungeendesha hii operesheni vijijini labda ungeweza kuambulia baadhi ya watu ambao wangevutiwa na msuli unaotumia kuwahadaa watanzania tena ukiwa nje ya mipaka ya nchi. I don't think huu msuli kutoka Chicago will work.
Views from Chicago can't change people's views in Tanzania kwa wakati huu uliobaki. Watu wamepigika, sometimes muwe mnakuja nyumbani muangalie watu walivyopigika kuliko kuangalia through online digital files.
Supply ya umeme haiko stable kwa wakati huu nchini, huku serikali inaendelea kuwala wananchi Megabit (Mb) every time wanapojaza kwenye devices zao. Now, what do you expect? Do you think people will utilize their Mbs watching personal views from Chicago kuliko kushuhudia what is going on the ground!!!? Strategically, mmepotea maboya since a day before you teamed up with the so called "JPM" (Jerk Push-up Maniac) Team.
Huyu ameshachanganyikiwa njia rahisi kuanzia sasa ni kususa kuchangia makala zake yeye asubiri tu matokeo.Mtu kama mimi ambae ninamzidi mwanakijiji umri nimeshaamua kuikata CCM na mfumo waje vijana itakuwaje ?!!
tusubiri tuone.NB: Video Inafuata
Operesheni Zinduka imeanza kama nilivyoahidi (jana haikuwezekana kwa sababu moja tu ya heshima ya Mch. Mtikila na haihusiani na mipango ya watu wengine). Nitajitahidi kuwa na onesho hili kila siku (ukiondoa mwisho wa Juma) na nitazungumzia mada mbalimbali. Wiki hii ya kwanza zaidi nitagusia hoja nyingi zilizoibuliwa kutushangaa tunaomkataa Lowassa kama mgombea Urais kwa tiketi ya upinzani.
La pili nitajitahidi hasa wiki ile inayokuja kutoa nafasi kwa wagombea wa CHADEMA kwenye Ubunge (ambao tutaweza kuwafikia) ili wajiuze kwani ninaamini Bunge lenye nguvu lililoundwa na watu waliolelewa na kukomaa katika upinzani na wenye kuelewa hasa ajenda ya upinzani ndio chachu ya kweli ya mabadiliko tuyatakayo. Hivyo, wiki ile inayokuja tutatoa nafasi hii kwa wote tutakaoweza kuwapata.
Tatu, kwa vile nina uhakika wapo wengi ambao hawajakubaliana na uamuzi wangu huu (ambao naamini ni sahihi) basi nitatoa nafasi pia kwa watu wengine kutoa hoja zao dhidi ya ninachosema (sikiliza onesha hili juu ya 'mashart kuzingatiwa'). Kwa barua pepe anuani yangu ipo chini na namna nyingine ya mawasiliano nitawajulisha siku chache zijazo.
Nitajitahidi kuweka shows zote kwenye uzi huu huu kila siku, na video zitafuata chini toka ya zamani zaidi hadi mpya zaidi.
Mwisho, ninaamini na nina uhakika kuwa kwa atakayeamua kunisikiliza kuanzia sasa hadi kuamkia Uchaguzi Mkuu hatoweza kumpigia Lowassa kura ya Urais. Ni kwa sababu hiyo wale ambao tayari wameshaamua kuwa haijalishi nini kitasemwa juu ya Lowassa nawaomba au kuwashauri wasisikilize mada hizi wasije kujikuta wanabadili mawazo. Mada hizi ni kwa wale tu ambao bado hawajaamua au wale ambao wameamua lakini bado wanajikuwa wanavuta na upepo wa 'nyomi' kiasi kwamba bado hawajathibitika katika msimamo wao.
"Uamuzi Makini, Uamuzi wa Lazima, Uamuzi Sahihi"
MMM
ONESHO 1. "Baada ya Kelele Sauti za Hoja Zitashinda"