Elections 2015 Operesheni Zinduka: Uamuzi Sahihi 2015

Elections 2015 Operesheni Zinduka: Uamuzi Sahihi 2015

MMM ni mtu au kikundi cha watu?? Kauli za tume..., tuta...., tuli.... wakati wewe unajiita mzee mwanakijiji (mmoja) ni kujifananisha na Mungu. Halafu unazidi kujikweza kwa kuongea nasi bila kujionyesha kama mfano wa Mungu alivyoongea na mitume wake. Usijifiche, au unaishi huko kwa kodi zetu??
Kama ndivyo kaa ukijuwa kuwa huo mfereji tutaufukia kwa zege October 25 mwaka huu. Ulaghai wako hautasaidia kitu watz wa leo siyo wa jana.
 
Mwanakijiji, nakushukuru sana kwa ajili ya kampeni hizi, utatusaidia sana kuwaelewesha wale wanaotaka kuelewa kwa nini Sio Lowasa, na kwa kuwa sio Lowasa, lazima tuwe na mtu atakayeingia ikulu, na kwa sababu sio Lowasa, inamaana ni magufuli.

Upinzani wakatae au wakubali, uchaguzi wa kumweka Lowasa kuwa mgombea wao wa uraisi, ni kosa kubwa sana, na litawagharimu upinzani.

Nitakufuatilia kwa umakini sana, na kufoward kila unachoandika kila kwa ninayemjua, hatuwezi kufanya makosa yatakayoligharimu taifa hili
 
Mkuu MM,

Unapoteza mwanya na hii digital operation. Labda ungeendesha hii operesheni vijijini labda ungeweza kuambulia baadhi ya watu ambao wangevutiwa na msuli unaotumia kuwahadaa watanzania tena ukiwa nje ya mipaka ya nchi. I don't think huu msuli kutoka Chicago will work.

Views from Chicago can't change people's views in Tanzania kwa wakati huu uliobaki. Watu wamepigika, sometimes muwe mnakuja nyumbani muangalie watu walivyopigika kuliko kuangalia through online digital files.

Supply ya umeme haiko stable kwa wakati huu nchini, huku serikali inaendelea kuwala wananchi Megabit (Mb) every time wanapojaza kwenye devices zao. Now, what do you expect? Do you think people will utilize their Mbs watching personal views from Chicago kuliko kushuhudia what is going on the ground!!!? Strategically, mmepotea maboya since a day before you teamed up with the so called "JPM" (Jerk Push-up Maniac) Team.
 
Mzee Mwanakijiji kwanza nikupe pole kwa kutumia muda, nguvu na akili katika kutuletea andiko ambalo hata wewe mwenyewe unajua halina tafakuri ya kutosha..

Kwa taarifa yako siku zote Majeshi huandaliwa wakati wa amani... Ikifika wakati wa vita ni kusongesha majeshi mbele na kupiga. Hushindi na hutashinda endapo upo katikati ya vita wewe uko busy na kuandaa majeshi utapigwa tu.!!

Itoshe kukwambia kwamba.. Lowassa amejiandaa kwa muda mrefu sana na pengine kuliko mwanasiasa mwingine yoyote katika harakati za kugombea URAIS... Kwa sasa hakuna mbinu yoyote labda kifo ndicho kitakachomzuia LOWASSA kuwa Rais wa Tano wa Tanzania..

Labda nikushauri Mzee wangu Mwanakijiji.. ni vyema muda huu ungeanza kuandaa material kwa makala na machapicho ya Historia mpya ya nchi yetu ya Tanzania baada ya Chama cha Mapinduzi Kudondoka.
 
MMM una tofauti gani na H.Pole Pole!
Sidhani kama utambadili mtu yeyote km tuliowategemea wamekuwa na hofu kiasi hiki ni heri vipofu waendelee na safari yao hata kama hawaoni mbele-hisia zao zitawaongeza njia.


Umeshindwa kwa kuandika sijui kama sauti na video kutabadili mambo na jua wale wa Lumumba watatumia hizo clip kuzisambaza uswahilini kujaribu kuwa tafuata wafuasi.


 
KinachoShangaza ni kuwa watu wanataka tuamini watu wengi watamchagua Lowassa. Lakini inaonekana hawaamini hilo ni kweli. Kama ni kweli hoja zangu hazina wasikilizaji na hazimbadili yeyote hivyo ni za kupuuzia. Hampuuzii mnaomtaka Lowassa kwanini?

Nitajibu: kwa sababu hamuamini Lowassa atakubaliwa na wengi kama mnavyotamani.

Mzee umeishiwa pumzi, ni vizuri ukipumzika kwenye benchi
 
Mi hua najiuliza, why not Lowasa? Sielewi, why nguvu nguvu kubwa hivi inatumika? Sielewi, hivi kama lowasa mwizi si wamkamate tu yaishe? Sielewi, kuna experiment kubwa sana ya kufanya, why not vote for him ili nigundue? Duh huyu lowasa ni binadamu wa aina yake. Mara fisadi, mara mgonjwa, mara mlutheri, mara mkaskazini duh, nimezindukaaaaa
 
Liulize hili swali kivingine..nguvu kubwa ya kumsukumizabLowassabkwa Watanzania ya nini na kwanini? Ukipata jibu la swali hili utapata na jibu lako.

Sijaona wanaomsukuma Lowassa kwa watanzania. Labda unitajie. Lakini wanaompinga Lowassa nimewaona na wengi wao hawana hata hoja ya msingi ya kumpinga. Nikumbushe hapa kwamba kwenye List of shame hakuwa Lowassa peke yake.
 
KinachoShangaza ni kuwa watu wanataka tuamini watu wengi watamchagua Lowassa. Lakini inaonekana hawaamini hilo ni kweli. Kama ni kweli hoja zangu hazina wasikilizaji na hazimbadili yeyote hivyo ni za kupuuzia. Hampuuzii mnaomtaka Lowassa kwanini?

Nitajibu: kwa sababu hamuamini Lowassa atakubaliwa na wengi kama mnavyotamani.


Inaonyesha umepewa fungu Fulani ili ufanye unachokifanya, tazama watu kuvuka 75% ya wachangiaji katika hoja zako humu wanaona hutoshi wala huna ushawishi tena, labda na pengine umechelewa sana!

Hivyo kwakuwa unapiga hela, na umeamua kuweka pamba masikioni, wewe endelea tu kula za mlevi ukiwa kwenye pc yako! Wananchi wameamua mabadiliko, Lowassa amekuja kutia nguvu Zaidi katika mabadiliko hayo! Kwahiyo issue hapa siyo EL tena, ila MABADILIKO ya mfumo kwa maana ingine watu wanataka tugawane fito ili tuanze upya ujenzi wa nyumba yetu TANZANIA!
 
Mkuu MM,

Unapoteza mwanya na hii digital operation. Labda ungeendesha hii operesheni vijijini labda ungeweza kuambulia baadhi ya watu ambao wangevutiwa na msuli unaotumia kuwahadaa watanzania tena ukiwa nje ya mipaka ya nchi. I don't think huu msuli kutoka Chicago will work.

Views from Chicago can't change people's views in Tanzania kwa wakati huu uliobaki. Watu wamepigika, sometimes muwe mnakuja nyumbani muangalie watu walivyopigika kuliko kuangalia through online digital files.

Supply ya umeme haiko stable kwa wakati huu nchini, huku serikali inaendelea kuwala wananchi Megabit (Mb) every time wanapojaza kwenye devices zao. Now, what do you expect? Do you think people will utilize their Mbs watching personal views from Chicago kuliko kushuhudia what is going on the ground!!!? Strategically, mmepotea maboya since a day before you teamed up with the so called "JPM" (Jerk Push-up Maniac) Team.

Wenzake wenyewe walioko mstari wa mbele wa mapambano pamoja na kupiga push ups na kualika wasanii maarufu hali bado tete...kila siku wanafikiria ni style gani itawasaidia kushawishi watu. Na kama kweli amelenga ambao hawajafanya maamuzi basi JF sio mahali pake kuleta hii kampeni yake..
 
Huyu ameshachanganyikiwa njia rahisi kuanzia sasa ni kususa kuchangia makala zake yeye asubiri tu matokeo.Mtu kama mimi ambae ninamzidi mwanakijiji umri nimeshaamua kuikata CCM na mfumo waje vijana itakuwaje ?!!

kingozi, umeshasoma na kuchangia tayari bila kujijua!
 
Mzee anzisha opereshen.... Kuna samaki wengi sana utawavua.. Wanaoshabikia kwa upepo tuu
 
Mwanakijiji umemdharirisha sana Mtikila kuimba nyimbo ya Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote. Mtikila mpaka anafariki alikua haitambui Tanzania yeye alikua anaitambua Tanganyika. Ningekushauri ungeimba wimbo wowote unaohusina na Tanganyika kama upo. Pia ningekushauri urekebishe yafuatayo unapokuja kwa mara ya pili
1. Maneno kama NINGE, NITA, etc usiyatumie sababu inaonesha unapenda kutukuzwa
2. Tuna wagombea tayari, unatushauri nini sisi wapiga kura ie nani anafaa kua urisi ?
3. Maoni yako yanamlenga zaidi Lowasa, kwanini usifanye uchambuzi wako kwa wagombea wote ili sisi wapiga kura tuweze kuchuja yupi anafaa na yupi hafai?
4. Kwa hii clip inaonesha unachuki zaidi kwa Lowasa, huoni kwamba kuna kitu kimefichika nyuma ya pazia kinachokusukuma kwenye hili.

Asante
 
NB: Video Inafuata

Operesheni Zinduka imeanza kama nilivyoahidi (jana haikuwezekana kwa sababu moja tu ya heshima ya Mch. Mtikila na haihusiani na mipango ya watu wengine). Nitajitahidi kuwa na onesho hili kila siku (ukiondoa mwisho wa Juma) na nitazungumzia mada mbalimbali. Wiki hii ya kwanza zaidi nitagusia hoja nyingi zilizoibuliwa kutushangaa tunaomkataa Lowassa kama mgombea Urais kwa tiketi ya upinzani.

La pili nitajitahidi hasa wiki ile inayokuja kutoa nafasi kwa wagombea wa CHADEMA kwenye Ubunge (ambao tutaweza kuwafikia) ili wajiuze kwani ninaamini Bunge lenye nguvu lililoundwa na watu waliolelewa na kukomaa katika upinzani na wenye kuelewa hasa ajenda ya upinzani ndio chachu ya kweli ya mabadiliko tuyatakayo. Hivyo, wiki ile inayokuja tutatoa nafasi hii kwa wote tutakaoweza kuwapata.

Tatu, kwa vile nina uhakika wapo wengi ambao hawajakubaliana na uamuzi wangu huu (ambao naamini ni sahihi) basi nitatoa nafasi pia kwa watu wengine kutoa hoja zao dhidi ya ninachosema (sikiliza onesha hili juu ya 'mashart kuzingatiwa'). Kwa barua pepe anuani yangu ipo chini na namna nyingine ya mawasiliano nitawajulisha siku chache zijazo.

Nitajitahidi kuweka shows zote kwenye uzi huu huu kila siku, na video zitafuata chini toka ya zamani zaidi hadi mpya zaidi.

Mwisho, ninaamini na nina uhakika kuwa kwa atakayeamua kunisikiliza kuanzia sasa hadi kuamkia Uchaguzi Mkuu hatoweza kumpigia Lowassa kura ya Urais. Ni kwa sababu hiyo wale ambao tayari wameshaamua kuwa haijalishi nini kitasemwa juu ya Lowassa nawaomba au kuwashauri wasisikilize mada hizi wasije kujikuta wanabadili mawazo. Mada hizi ni kwa wale tu ambao bado hawajaamua au wale ambao wameamua lakini bado wanajikuwa wanavuta na upepo wa 'nyomi' kiasi kwamba bado hawajathibitika katika msimamo wao.

"Uamuzi Makini, Uamuzi wa Lazima, Uamuzi Sahihi"

MMM

ONESHO 1. "Baada ya Kelele Sauti za Hoja Zitashinda"

tusubiri tuone.
 
Last edited by a moderator:
Ww mwanakijiji upo marekani umekaa nyuma ya keyboard unaandika tu oo oparesheni zinduka .. Zinduka kwanza ww mwenyewe kwamba kitu unachofanya siyo au mmenunuliwa? Watanzania wanataka mabadiriko na mda ndio huu harafu ww usujione una akili kuliko maelfu wanaomkubali lowassa..
 
great thinkers hatuhitaji kudeal na lowasa, tungeanza kuweka mikakati ya kuimarisha taassisi za utawala,

lowasa ni mtu mmoja tu kati ya watu mill 45 hata kama tutamchagua kwenda ilkulu tunaouwezo wa kumdhibiti, afuate matakwa ya wamanchi, hii ndo falsafa ya nguvu ya umma inayoongoza itikadi ya chadema,

nadhani mzee mwanakijiji amechoka akili. tujadili nyufa zinazotaka kuli pasua taifa alafu tujadili mikakati ya kuziba nyufa,

tukijielekeza huko jibu linalokuja ni - mabadiliko- kuanzia hapo tujadili mabadiliko ya namana gani na yataletwa na nani??.

ukiona watu kama MM wanakwepa kujadili haya ujue kuna shida kwenye bongo zao.
 
Back
Top Bottom