Opinion: Dr. Shika Ana Hali Fulani, Anahitaji Msaada, Huruma, Upendo na Protection of His Right to Privacy!.

Mi sina jipya zaid ya kusisitiza jamaa alikuwa agent wa CIA Kuhusu akili yake inasemekana alikuwa injected some materials ya kuwewesesha akili yake, na anaonekana yeye kuficha mambo mengi mno


Most probably hata hiyo hijacking aliyofanyiwa na hao anaosema walitaka pesa ni watu waliokuwa na connection na KBG.Kuna mtu huyo aliyeratibu mpango Wa yeye kuchukuliwa mateka( pamoja na genge lake) naye naona hakuwa Wa Kawaida. Inasemekena alinyatia documents za kampuni na kila detail iliyomhusu Dr. Shika. Watu wenye nia ya pesa tu ilitosha tu kuhakikishiwa na mhasibu kuwa kampuni inazo pesa za kutosha kisha wakasuka racket ya kumchukua Dr. Shika lakini mpaka sio ku-access classified info za kampuni kiasi kile.Hoja hadi sasa sio kama ni amepata kuwa Agent au la bali je bado yuko deployed na kama ndivyo na nani?

Pili: ni kweli jamaa bado ni part ya management ya kampuni anazoziongelea? Na kweli kampuni bado zina-exist? Hoja ya website kuthibitisha uwepo Wa kampuni siiamini!

Tatu: Stahiki zake zitokanazo na yeye kuwa sehemu ya kampuni kama shareholder na Mkurugenzi zikoje? Zinapitia wapi? Inakuwaje anakosa dola 150 za BIMA ya Transfer ya pesa zake?
 

Kaka SANCTUS ANACLETUS , naomba umeulize kaka Pascal Mayalla , kuwa alishawahi kupata mauimivu ya kidole?, alishawahi kupata maumivu ya kucha? Hivi alishawahi kujiuliza ni kwa nini watekwaji wote huwa wanangolewa kucha bila ganzi?

Cha ajabu, Dr Shika alikatwa vidole viwili kwa Panga/Shoka na kidole cha mkono mwingine kikasagwasagwa nyundo, lakini mzee aliweza kufungua mlango, akatoka nje, akaruka ukuta wa kwanza kisha akaruka wa pili na kisha akafanikiwa kukimbia akiwa akijihami, hapo kumbuka alikuwa mateka kwa siku 28 zenye mateso kila siku

Anasema alirudi bongo akiwa hovyo, aliwezaje kufika spain, nani aligharamia safari yake, alikuwa anafanya nini huko Spain?

Kuna maswali mengi kuliko majibu, hatujajua meno yalitokaje
 
Hao wamepata nafasi ya kumuuliza maswali lakini mwisho wa siku wanauliza yaleyale ambayo ashaelezea badala ya kumchimba zaidi.

Hv hawaoni kuwa kuna mengi anayaficha katika maelelzo yake!
Kuficha kitu maana yake ni kutakiwa kitolewe ukakizuia, katika maelezo hapo sijaona swali aliloulizwa akakaidi kulijibu
 
Ni vyombo vipi vya usalama unavyoviingelea wewe? Ni hawa ambao wametangaza mtu amekimbia nchi ndani ya masaa 24 mtu yuleyule anakanusha?
 
Binafsi nikifuatilia threads zako ndugu Paskali hapa Jf na nikikumbuka harakati zako tokea unaendesha kipindi cha Kiti Moto THEN nikimuangalia Dr Shika tokea akiwa mnadani hadi anapotoka polisi na mahojiano aliyofanya pale Tabata naweza kusema pasipo shska kwamba, kati yenu ninyi wawili nikiwalinganisha basi wewe Paskali ndiyo " mgonjwa zaidi " kama kweli umeshindwa kumuelewa Dr Shika!! Labda kama una ajenda ya siri!
 
Hata mimi kuna vitu fulani ambavyo nilivisikiliza nikagundua there's problem kwenye hili suala la Dr Shika!

1. Anaeleza kwamba masharti ya mnada yalikuwa kulipa ć@sh 25% ya fedha papo hapo lkn yeye akasema cash hana hatembei na hela mfukoni ila Bank-Bank Transfer akakubali.....
Utakubalije kutransfer pesa ambayo unajua iko kwenye Controversy kiasi hicho na haiwezi kupatikana leo wala kesho?

2. Hali halisi aliyokuwa nayo. Kiukweli kabisa kama angelikua na fedha kiasi hicho na yuko well Mentally asingekubali kuishi kihasara hasara vile. Pesa ipo???? Suala ni kufuatilia tu zije kwanini asifuatilie,..... Ameingia Tz 203 kama miaka 4 sasa huna Fedha ya Kula, Kupanga Chumba, Kufanya matumizi Mengine Muhimu NguoViatu nk na Unajua ni billionaire lazima ufight Fedha zako uzipate lkn mzee hakufanya vyote hivi. He was Not ok mentally

3. Baada ya kusikiliza jinsi ambavyo alitekwa na kuteswa, alivyoumizwa sehemu mbali mbali za mwili wake kama vile mbavuni ambavyo alivunjwa mbavu tano, kukatwa vidole vya mikono, kupigwa shoti ya umeme, shingoni na hasa hasa kwenye masikio ambapo ndio yapo jirani zaidi na Ubongo, ni wazi kabisa kuwa yamemsababishia kuwa mentally and physically not okay!

Sasa basi kwa haya na mengine mengi, Mtu unamgundua kuwa huyu dr Shika Lunyalula Kidola hakuwa okay hata kama aliweza kuongea kwa ufasaha wa matamshi na kimantiki lakini co-ordination ya vitu alivosema haikuwepo na kwasababu hiyo basi alikuwa ni mtu anayehitaji kusaidiwa, apate counseling ya kutosha kumsaidia kurejesha matumaini na nguvu ya kuishi kwani anaonekana kukata tamaa ya kuishi na kuwa tayari kufa kitu ambacho hakukubaliwi. Kila mtu haki yake ya kwanza duniani ni kuishi hivyo apewe counseling ya muda na ahakikishiwe mazingira bora ya kuishi na sio kumuacha aendelee kuishi pale kwenye stoo ni kumuangamiza zaidi

Apatiwe msaada wa chakula, milo mi3 angalao. Chakula ni msaada mkubwa sana kufanya Ubongo urejeshe afya yake ya asili na kufanya kazi kwa kipimo chake kinachotakiwa.

Tukubali kuwa Tanzania bado ni Unmatured kwa karibu kila kitu. HUWEZI kudhani kuwa kampuni kubwa ya udalali kama YONOina wafanyakazi wasio na uwezo wa kusoma saikolojia ya mtu na kujua huyu ni mnunuzi ama La wao wanaangalia pesa tu. Tamaa tu. Wanajua ni kama muujiza umedondoka kutoka juu wanapiga pesa ya Ajabu siku hiyo. Poor tz

Police wenyewe uchwara tu. Hawana taaluma yeyote zaidi ya kupiga virungu tu. Bado sana kufikia levo za wenzetu

Mpaka kina mayalla waongee huku JF ndio utakuta eti na wenyewe wanashituka sasa ha ha haaaaa bado sana
 
Mkuuu naomba tushikane Mkono ... Asante..
 
Asante
 
Cha ajabu hao wanaomuhoji wanashindwa kuuliza maswali kama haya!
 
Dr ameshafanya interviews na vyombo kama vitano mpaka sasa videos zote ukizisikioiza maelezo Dr anayotoa ni yaleyale hayaongezi wala hayapunguzi kama angekua anasema uongo ni rahisi kumkamata kwenye interrogations zaidi ya moja lakini context ya mazungumzo yake ina mantiki.

Zaidi sana Vielelezo vinamuunga mkono
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…