Opinion: Dr. Shika Ana Hali Fulani, Anahitaji Msaada, Huruma, Upendo na Protection of His Right to Privacy!.

Hizi lugh za kingereza mnazochomekea mnanifanya nisiambulie kitu
 
ULIPOANZIA KWA HUYO DR UKATUMIA NENO MOJA LA KIGENI, UKAJA KWA YONO UKALITUMIA TENA HILO NENO ILA NIMESHANGAA KWA JESHI LETU HUJALITUMIA KABISA HILO NENO.
 
Nilipoangalia mahojiano yake kwa Millard na alipomention electoral shock,nikasema enhee... Umeongea sawa kabisa Paskali. Niliwashangaa sana Yono, na Polisi. Ila there is a story behind ambayo Dr anayo. Hiyo insanity haijaja hivi hivi tuu
 
Bahatika kupata torturing kama ile halafu utaona ni Insane au siyo Insane sawa Mayalla
 
Nimeipenda logic yako Mkuu
 
Dr. Shika ni mtu aliyechanganyikiwa tu na ameamua kufunguka mwenyewe na bila shaka majibu yote yatapatikana. Tusiwe na shauku ya kumchimba sana, anahitaji kufarijiwa na kupokelewa kwa upendo.

Kwa wale waliowahi kukaa nchi za ulaya mashariki watakuwa hawashangai kinachomkuta Dr Shika kwa kuwa wako wengi wana dalili na mienendo inayofanana na alichokifanya Dr wetu mpendwa.

Miaka ya 1980 mpaka 1990 nchi za kikomunisti zilianza kuingia kwenye uasi uliopelekea kuuondoa ukomunisti na kuukumbatia ubepari. Wananchi wengi walikuwa na tamaa ya kutoka kwenye utawala wa kikomunisti kuelekea kwenye ubepari ambapo kila mtu aliiona USA kama mbingu hapa duniani.

Dollar ilikuwa kitu adimu sana na Dollar moja ilikuwa pesa nyingi inayoweza kufanya mambo makubwa na kwa Dollar 100 ungeweza kukabidhiwa mke ili mradi tu uwe nazo za kutosha. Dollar 100 ilikuwa ni nadra kuiona na kama mtu anayo ni hela nyingi sana na hasa unapozibadilisha na pesa za ndani.

Njia ya kuipata Dollar kwa wenyeji ilikuwa ni kupitia wageni waliobahatika kuwepo kwenye nchi husika kwa muda mrefu, na hasa kama wanakuwa na kipato cha Dollar kila baada ya kipindi fulani, iwe baada ya miezi sita au mwaka. Kwa kumsikiliza Dr Shika hapa ndipo alipoingia kwenye mtego ambao huwa ni wachache sana wanaofanikiwa kuibadilisha hali - Nadhani ni sawa na hukumu ya kifo.

Wanafunzi wa nchi za kigeni na hasa za kiarabu,Nigeria na baadaye Angola ndio walikuwa wana uwezo mkubwa kifedha kwa maana ya Dollar na hapa tuzungumzie kitu kama USD 1200 kwa mwaka. Kwa hela hiyo unaweza kuona ni jinsi gani mwanafunzi alivyokuwa na uwezo katika nchi ambazo wananchi wake waliisha kata tamaa, chukulia mfano wa lile BOOM la hapo mlimani wanafunzi wanavyotanua wakizipata.

Dr Shika kwa maelezo yake aliisha fikia mafanikio kielimu na kutamani kupigana na umasikini, Uwezo wa mtaji kwa kutumia Dollar alikuwa nao, ukimtazama na kumsikiliza unaona kabisa alikuwa analenga kufikia mafanikio ya kipato. Kwa nchi hizi za mashariki hasa Russia ili uweze kuingia kwenye mfumo unahitaji mshirika ambaye ni mzawa na vizuri zaidi awe mtu mwenye mahusiano au na watunga sera au watendaji kwa ngazi yoyote ile. Hapa ndipo anapoingia MWANAMKE na ile pombe ya VODKA kama kilainishi kulingana na utamaduni.

Dr Shika nadhani alikuwa na mahusiano na mwanamke ambaye alikuja kuanza nae harakati za kusaka kipato kwa kuwekeza kile alichokuwa nacho- ambacho hakikuwa kidogo asilani. Upo uwezekano mkubwa kwamba walianza kununua viwanda vilivyokuwa vinajifia na mimi sishangai sana hata akisema ana kampuni Russia labda kwa sasa mshirika wake ndio BOSS.

Umiliki wa kampuni aliyofungua huko Russia nadhani ndio kilikuja kuwa chanzo cha matatizo baada ya miaka kupita na thamani ya mali walizonunua kupanda mara kadhaa. Yawezekana alianza kutafutiwa namna ya kumuondoa kwenye huo mfumo na hapa ndipo alipoanza kugundua kuwa kuna watu wamemchezea.Ukihesabu miaka aliyosota huko Russia na pengine kupoteza kabisa uwekezaji wake na kuja kuanza zero uzeeni, kuchanganyikiwa ni kitu kisichoepukika.

Yawezekana atakuwa na stori tofauti lakini yule sio kichaa, ni mtu msomi aliyedhurumiwa na hakupata mtu wa kumtetea, atakuwa ameanza kuchanganyikiwa na hasa ukizingatia kuwa umri nao unaenda na yeye sio kijana wa kuanzisha harakati upya. Ni vizuri tumsaidie zaidi kuliko kumfanya kituko cha mwaka huu. Historia inaonyesha kuwa hata Adam Smith alikuwa anafanya mambo ambayo ungeweza kusema yanafanywa na vichaa tu, lakini pamoja na hilo ataendelea kuwa mmoja kati ya mapapa wa uchumi Duniani.
 
Nilipoangalia mahojiano yake kwa Millard na alipomention electoral shock,nikasema enhee... Umeongea sawa kabisa Paskali. Niliwashangaa sana Yono, na Polisi. Ila there is a story behind ambayo Dr anayo. Hiyo insanity haijaja hivi hivi tuu
Nakubaliana na wewe. Dr kuna kitu hajakisema na hajakiweka wazi.

1. Alipata wapi mtaji wa kuanzisha a very successful business within a short period of time baada ya kumaliza shule?

2. Ilikuaje ubalozi wa marekani wajihusishe kumtorosha kutoka urusi tena kwa ndege ya malkia wa uholanzi hadi Armsterdam na kisha kuja Dar kama anavyosema.

3. Baada ya kufika hapa nchi alipata wapi nauli ya kumpeleka Malaga Hispania na akaweza kuishi huko kwa miaka 8 hafi aliporudi nchini mwaka 2013.

4. Kwa nini baada ya kutoroka toka Urusi bado amekua na wasiwasi kua warusi watamtafta popote alipo wamuue, wasiwasi wake ni wa nini? Kweli vibaka wanaweza kukufuatilia hadi nje ya nchi wakuue?!

5. Anasema warusi wana chuo cha kufundisha jinsi ya kuua, tena anataja KGB ambayo ni taasisi ya serikali, je alitekwa na KGB au alitekwa na vibaka, vibaka gani wanaweza kusomea chuo kikuu jinsi ya kuua mtu na jinsi ya kumtesa?

6. Anasema hataki kuwasiliana na mke wake wasije kumtambua alipo, kwamba simu zote zinarekodiwa ziazotoka nje, hao ambao anahofu kua watamjua alipo ni wale vibaka waliomteka au watu wengine, vibaka wanawezaje kurekodi au kuingilia mawasiliano ya watu toka nje ya nchi?

7. Dr alikimbilia hispania ili kupoteza ushahidi wa uwepo wake, kisha akarudi Tanzania ili kuwapoteza tena kama wanadhani yuko hispania, ni kina nani hao ambao dr anawakimbia kiasi hicho, wale vibaka waliomteka au wengine?

Dr ana kitu hataki kukisema. Kuna kitu kimejificha nyuma yake.

Zaidi Dr ni loser, huwezi kwenda kusoma ukalowea huko ukasahau hata wazazi wako.
 
Hii ilikuwa ni njia yake Dr. Shika kuomba msaada kwa jamii ya Kitanzania na Ulimwengu kwa ujumla. Wahusika wamsaidie na wengine tusio na nguvu tumuombee kwa Mungu mpendwa wetu.
 
Siyo lazima kila kitu kisemwe mkuu mengine jiulize mwenyewe kisha unyamaze tu. Ukishajijibu hayo yote basi na wengine tuache kiherehere kwenye kila jambo mengine ni ya kuona na kuyaacha yalivyo kama huhusiki au hauna msaada wowote.
 
Yaani hiyo story tu kama una akili timamu hauwezi kuhoji haya maswali!yule mzee ana hallucinate anaunganisha na matukio ya kweli;Watanzania wengi kwenye story ya huyu mzee ndio imekua kipimo cha IQ;Yaani utafutwe na KGB alafu unaenda kununua nyumba za Lugumi wakati hata mwanafunzi wa ujasusi anajua atakua front pages the next day!
 
Umeongea point sana bro.

Ndio maana mm nawaona scientists are so insane to believe that big bang explosion ndiyo ilipelekea kutokea kwa an extremely fine tuned universe.

How insane is this [emoji28] [emoji28]
 
Jambo la shika halikupaswa kuwa story hadi Leo hii hadi tukasahau kodi tunayo idai kutoka kwa lugumi na jinsi gani tutakavyo ipata kupitia mali zake.
billion 3 in fedha nyingi kwa maendeleo ya wananchi, je mali za lugumi ni hizo nyumba tu?
tabu yetu sisi wa tz hatuko serious kwenye mambo ya msingi ndio maana tumefika hapa tulipo. kwa sasa tusipoteze muda kuhangaka na shika!
 
Well noted and written kuna kimoja hapa umekisahau niwatanzania walioshadadia hili swala Jee Watanzania ni wa Kawaida au Insane?

Watu walivyolipokea kiukweli ukimuondoa Mambosasa wamelifurahia mno, waandishi wamendika sababu jamii kwa ujumla wake hili swala limewapa faraja kubwa mno katika kipindi hiki kigumu na wamelipenda. Haiwezekani jamii ihame ghafla kutoka katika mambo magumu na-serious kulishika hili la Dr. Shika.

Watanzania ni responsible society lakini wanataka habari za mzaha pia, ukiyachuku Ma bombadier, Water Gauge, Chato Airport, Noah kilaMtz, dhahabu kupimwa kwa tipper za mchanga, kuongeza mishahara wafanyakazi wa serikali, kuwa donor country wakati budget yetu hatuwezi hata kufikia 50% ya vyanzo vyetu tunakuwaje wazima hapa kaka? : Haki ya Mungu sio Dr. Shika peke yake Paskali anayehitaji msaada wa kijamii. Kwa Kesi hii angefungwa Dr. Shika tungeshangaa tena kuliko ya DAB kuwa amiri jeshi mtoto.

 
Hata yeye Shika akija kusona hapa, atatoka na list ya watu atakaowaita wehu na lazima tutashangaa tutapoona na jina la mtoa mada limo.
Kwa ufupi mijitu yenye akili nyingi huonekana kama hazimo hivi na wakati huo huo wao wanatushangaa sisi ni kwa nini akili zetu zipo hivi kama zilivyo, mfano Newton anatushangaa kwa nini tupo hivi.
 
Acha kumuita Mwehu Mtu ambaye humjui! Usije onekana mwehu mwenyewe! Kwanza kwa Elimu yake tu na yako, tayari Mwehu keshajulikana!
 
Cha ajabu kila mtu amebaki akimtangaza NA kuendelea kumfukunyua ila sijaona aliyejitokeza kumsaidia......hii inaonyesha wabongo wenyewe hatuna uhakika NA hali halisi ya Dr Shika Bali tunahisi hisi tu .
 
mimi nathani upo right kuna kitu umekisema hapa kwa kukificha,na umetumia science kushawishi.

Contrary na mada hiii think watz ndio sio watu wazima kiakili.
Sijui tunapata wapi muda kuongea mambo ambayo hatuyajui.
Huku tukipotez muda mwingi.
Hawa waandishi wa habari wa tz ni mzigo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…