Nimejipanga vizuri, nimesoma kila sehemu. Lakini ile kuingia tu kwenye chumba cha wadosi nikawekwa mtu kati, watu wananikodolea macho, mungu wangu…… Nikajikuta kila kitu nimesahau.
Maswali yalikuwa rahisi sana, nilipotoka tu kwenye kile chumba cha Oral na kufika nyumbani, majibu yakaanza kushuka… ila pale ndani ubongo ulipararaiz huwezi amini.
Nimefanya Oral ya Tax Management Officer II.
MASWALI YAO HAYA👇
1. Introduce yourself
2. Four Entities required to register with VAT apart from those reached threshold
3. Five Characteristics of a good taxation
4. Five Advantage of double taxation
5. Four Methods of Trade protection
6. Four Circumstances that make a commissioner to adjust or Jeopardy Assessment
EXTRA👇
What is your salary expectation
ZINGATIA👇
Najua utasema rahisi kwa kuwa uko nje ya kile chumba, hata mimi nilipofika nyumbani nilijipiga makofi ya uso kwanini sikuyajibu vyema. Of course ni rahisi sana, lakini sio ukiwa umebananishwa chobingo unexpected huku ubongo wako ukiimba baadhi ya materials yaliyopo kichwani ili yasikutoke.
UPDATE 28/05/2025:
Nimefanikiwa kuwa TMO as per TRA Email I have received now. Much thanks to God for this Blessing…