Oreshnik: Silaha mpya tishio iliyotumiwa na Urusi. Hakuna mfumo unaweza kuzuia duniani, isipokuwa S550 wa Urusi wenyewe

Sorry mkuu nilidhani umeandika S-500. Sasa batteries za S-550 ziko wapi kwa wingi mpaka zizuie ICBM. Unajua kuwa na silaha moja mbili na kuzitumia kwa impact ya maana vitani ni vitu viwili tofauti.
Russia ina Su-57 chache hata kama zingekuwa na uwezo kidogo zaidi ila haziwezi zidi J-20 zaidi ya 200 za China.

Russia kwenye missiles wanapenda kutumia kauli za "should be, will be able, can..." yaani hawana uhakika 100% au system haiko na probability kubwa.

Ukiwauliza Marekani wana Aegis ships ngapi, watakwambia ni meli zaidi ya 100 na zaidi ya 60 ziko planned kuundwa. Ukiwauliza wana THAAD batteries ngapi na zimefungwa wapi inajulikana ni South Korea, Guam na Middle East.

Sasa S-550 zimefungwa wapi na wapi kwamba zina hata namba inayoshawishi.
 
Kwanza hii tabia ya kutoa taarifa kwa marekani kabla ya kushambulia malengo ni kwa nini haswa?
Iran ilipoishambulia israel mara ya kwanza ilitoa taarifa pentagon kwamba masaa 8 yajayo wataishambulia israel. Na wakashambulia.
Jana Russia nao wanawapa taarifa Pentagon kwamba watashambulia huko dnepo. Hii imekaaje?
 
Kwa nini hawalitumii kuwalenga Ukraine kule Kursk ? Supa pawa wa mchongo.
 
Bwashee tatizo sio MIRVs ila Shido ni speed and accuracy ku hit target,kwasasa technology ya silaha za kivita zinawekeza zaidi kwenye utafiti kuhusu speed
Ukiendesha gari kwa speeed ya 250km/h ukapinduka mara nne linakuua, ili ufe kuna haja gani ya kuendesha kwa 350km/hr kwanza likiwa hata na 140km/h unakufa.

Sasa hypersonic speed ya haya makombora mapya ya Urusi unayosema ni kubwa haina mantiki na haibadili chochote. ICBM ya Marekani Minuteman III ni ya mwaka 1970 ina maximum speed ya 15,000km/h hebu tuambie ni mfumo gani duniani unaozuia reentry speed hii?
 
Sijui Kama umesoma na kuelewa au umejibu kwa hisia.
Tafadhali pitia tovuti za BBC, CNN na nyinginezo zenye mlengo wa kuisaidia Ukraine uone taarifa hii niliyo weka hapa.
Ukiona haitoshi nenda za Russia mfano Sputinik na RT news.
Acha kuumiza kichwa na huyo form sex level
 
Wanaolazimisha ligi ya makombora hawataki kukubali kwamba ni vita ngumu.

Ndio maana Marekani inazingatia nuclear triad, hata Urusi ina kitu kama hiki.
1. ICBM hizi kama Minuteman III na Sentinel inayokuja. Urusi ardhini wana makombora mengi mengine yanabebwa na magari makubwa kama RS-24 Yars.

2. Submarine launched ballistic missiles. Hapa wana makombora yapo kwenye nyambizi na muda wote wa mwaka ziko majini hazijulikani wapi. Hizi hata nchi nzima ishambuliwe zinaweza shambulia zikiwa deep under water mbali na nyumbani. US Navy wana Ohio class nuclear sub inabeba makombora 24 ya Trident II D5 na kila kombora lina MIRVs kati ya 4 hadi 12. Hizi nyambizi za Ohio zipo 14.
Similarly Urusi ana Borei class nuclear subs 5 zinazobeba makombora 16 ya Bulava yenye MIRVs kadhaa.

3. Nuclear bomber. Marekani ana ndege za kubeba mabomu ya nyuklia B1B Lancer, B-52 Stratofortless, B-2 Spirit, B-21 Raider hizi mbili za mwisho ni stealth. Urusi ana Tu-160 Blackjack "White Swan" na Tu-95.

Ikitokea exchange wataumia wote ila kuna mmoja atachakaa zaidi sababu ya uwezo wake wa delivery ulivyo.
 
Juzi storm shadow imepiga kurks hakuna hata moja wameintercept naona nadharia zao tu za kujifurahisha baada ya ghawa na alkasusu
 
Kuna mfumo wa kupeana taarifa unaporusha ballistic missile kuepuka kushambuliana kwa silaha za nuclear kimakosa.
Unaweza kurusha hilo kombora mwenzio akadhani umerusha la nyukilia akajibu shambulizi kwa nuclear missile pia kumbe umerusha la kawaida.
Hiyo inatokana na ballistic missiles za kawaida au za nuclear zote zinatumia teknolojia moja tofauti warheads tu.
Mfumo huo wa taarifa ni automatic, waliwekeana mkataba wafanye hivyo.
 
Juzi storm shadow imepiga kurks hakuna hata moja wameintercept naona nadharia zao tu za kujifurahisha baada ya ghawa na alkasusu
Siyo kweli.
Wamefanya interception makombora yote, mengi hayakufika ardhini Ila moja debris zake zilifika karibu na makazi au facility ya kijeshi.
Otherwise prove hiyo taarifa yako kupitia neutral source ya taarifa yako.
 
Juzi storm shadow imepiga kurks hakuna hata moja wameintercept naona nadharia zao tu za kujifurahisha baada ya ghawa na alkasusu
Hapohapo wanalinganisha na Arrow 3 ABM ya Israel ambayo ilishambuliwa na makombora zaidi ya 200 kwa wakati mmoja wanasema haiwezi kazi. Wakati hata wao hapo Kursk Wakorea Kaskazini wameuwawa na air defense systems zipo nyingi layers tofauti.

Hakuna system iko 100% sure kila kitu ila zipo zinazofanya sana kazi hadi kupenya lazima ushambulie kama full scale war.
 
Sawa, lakini siamini kama wazungu wote watashindwa kuipiga Urusi
 
Hizi sifa kwamba hakuna mfumo unazuia duniani wakati haujawahi kutumika kushushambulia mifumo mingine ni hoax
 
Wanafunzi wasumbufu lazima waripot kwa kiranja mkuu
Maana inaweza ikatokea shambulia likaingiliwa kati mshambuliaji akaumbuka

View: https://x.com/clashreport/status/1859603066783162638?t=vDP8_949Me_nPUCdgOTo-w&s=19
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…