Mpaka sasa hakuna amsha amsha zozote zile za kuonyesha kama huu ni mwaka wa Uchaguzi mkuu wa Serikari,
Mtaani hakuna majadiliano tena kama zamani, "kwamba mimi nitagombea udiwani mwaka huu au fulani atagombea ubunge,
Flani hafai tumtimue uchaguzi ukifika tumchukue na kumshawishi flani Agombee na kushika nafasi yake"
Hakuna tena, Sio Upinzani wala Chama Dola wote wapo kimya. Kila mtu yuko busy na January, kila mtu yuko busy kukimbizana kutafuta elfu 3 ya kununua kilo ya Unga kwa Ajiri ya familia,
Kila mtu anawaza Maisha yake kwanza, Cha kwanza ni vipi ataweza kupata mkate wake wa kila siku, pili watoto watasomaje, Tatu na mwisho ni vipi atamtunza mzazi mwenzie na Wazazi wao kwa ujumla,
Jamii haijadili tena Siasa kwa kishindo kama zamani ni wachache mno"Je ile Nia yao ya kutaka Kuua Demokrasia imefanikiwa"?
Mimi sijui ila nafikiri wanaelekea kushinda.
Kikubwa ni kwamba Kesho kutwa tu hapo mhe/Dr/Raisi John Pombe Magufuri anakwenda kulivunja Bunge kwa Ajiri ya kujiandaa kuingia kwenye Uchaguzi mkuu kwa maana ya kuchagua Madiwani, Wabunge na Raisi mwenyewe.
Ni Nani atatetea kiti chake cha Udiwani/Ubunge/Uraisi hatujui, na ni nani Atapoteza pia hatujui na ni kina nani watakuja baada yao pia hatujui,?
Ni karata inachezwa
Uchaguzi 2020.
Cc Zero IQ
Sent using
Jamii Forums mobile app