Orodha ya makabila yaliyojaza sehemu mbali mbali DSM

Orodha ya makabila yaliyojaza sehemu mbali mbali DSM

sema it happens people who are friends and they look like themselves tend to be in the same circles
Sikupingi...

Ila kwenda mikoa ya watu then mnaishi vikundi vya kikabila sidhani kama inaleta picha nzuri...

Kwamba kunakua na kimtaa mmejaa kabila moja tu, mnakua kama wakimbizi kwenye mikoa ya watu...

Sio vibaya ila mimi hufurahia makabila ambayo yakienda mikoa ya watu hawajitengitengi.
 
Ngoja nione watu wa mikoani mnavyofurahia kukimbia vijijini na kuishi Daslaam
 
1. Wachaga - Kimara
2. Wakurya - Ukonga hasa Kitunda
3. Wahaya - Mwananyamala na sinza
4. Wapemba - Kigamboni
4. Wanyakyusa - Nyomi lao lipo keko
5. Mbagala - wamakonde

Hii inaweza kutumika kwa watu wa marketing kweny kutaget wateja
Nautuambie kimara soko la nini,kigamboni,mbagala,mwananyamala,kitunda,😀.ili nasi tuzione fursa
 
Masai wengi dar hawana kwao wanalala popote wengi wasusi Saluni Rasta saluni Mwenge na Ilala na kuuza dawa za kimasai na bidhaa xa mikononi wa kimasai ili wanaishi kusikojulikana Dar
Sawa sawa ,maana hata hy Masaki ni hivyo hivyo usemavyo ,kingine walinzi magetini
 
Sikupingi...

Ila kwenda mikoa ya watu then mnaishi vikundi vya kikabila sidhani kama inaleta picha nzuri...

Kwamba kunakua na kimtaa mmejaa kabila moja tu, mnakua kama wakimbizi kwenye mikoa ya watu...

Sio vibaya ila mimi hufurahia makabila ambayo yakienda mikoa ya watu hawajitengitengi.
Cha kwanza na wewe ni mbaguzi kama sisi wabaguzi wengine lakini still una mbavu za kunyooshea wengine kidole

Kwanza umetaja "mikoa ya watu" maana yake unabagua wengine which means ni kama ukabila tu

Kununua ardhi mahali au kupata ardhi ni umauzi wa mtu na mfuko wake,huwezi pangia mtu mfuko wake

Hawa watu wanatoka vijiji vimoja huko watotakako,kama kuna ardhi wanaitana,watakuitaje wakati bado hamjafahamiana?

Kwenye vijiji wanakotoka wanaisha kabila moja,unaona sawa ila wakiamia pengine wakiishi pamoja si sawa?Hoja mufilisi kabisa

Kama upo sawa vunja kabisa na vijiji wanakotoka maana bado ni ukabila ule ule sema establishment ni miaka tofauti

Hoja yako ya hovyo sana

Na huwezi pangia watu pa kuishi,kama unapangia basi utakua mtu wa ajabu sana na kwanza hutaweza hiyo kazi ya kupangia watu pa kuishi

Sana sana watakupeleka mahakamani kwa kuvunja basic human rights za watu za kuishi watakako

Umeangalia makabila tu,jee matajiri wanaojitenga Masaki huwaoni?Wahindi wanaojitenga Posta huwaoni?Viongozi wanavyojitenga Mikocheni huwaoni?

Wanajeshi wanaojitenga huwaoni?

Masikini waliojitenga Mbagala na Uwanja wa Fisi mbona huwalalamikii utenganifu wao wanawabagua matajiri na middle class?

Middle class waliojitenga Mbezi bEach,Mbweni,Bahari BEach,etc mbona huwalalamikii?Au huo sio utenganifu?

Waojitenga kwa misingi ya kidini kama waislamu kivyao,walokole kivyao,wakristo huwaoni,etc?

Tukianza kuchambua kabila utakua umefungulia pandora box then anything goes,slippery slope hiyo.

Wee jamaa utakua na kichaa
 
Back
Top Bottom