Uchaguzi 2020 Orodha ya matusi mazito ya Tundu Lissu kwa CCM na Mgombea

Uchaguzi 2020 Orodha ya matusi mazito ya Tundu Lissu kwa CCM na Mgombea

“Mtu anawaambia hamtolipa kodi,halafu akimaliza anaanza kuwachangisha pesa, analeta vibakuli, vinaendana hivyo Ndugu zangu!?, Watanzania mjitambue, si angekuwa hawaombi hata nyinyi anaowahubiria, akiingia fedha zilizokusanywa watazila zote,Majuto ni Mjukuu”-JPM akiwa Kagera
Lissu haijawahi sema kwamba hatutalipa kodi,au wewe anaposema tax payer bill of right unaelewa kuwa anafuta kodi?
 
Mwenye kujua definition ya matusi atoke mbele kutunyambulishia maana ni kama maana ya neno matusi halieleweki na wengi
 
Ku list tu hakutoshi, aseme yeye kama Rais mtarajiwa atafanya nini akipewa nafasi. Wao ni mafundi wa kuweka lists eg. List of shame na nyingine, hawakuonyesha solutions ndio maana pamoja na ma list yote wenzao wanapeta tu na hata oct 28 watapeta vile vile huku yeye akibaki na hayo matusi mkononi. Watanzania sio wajinga, tunajua tufanyacho.

Kwani wewe umekwenda kwenye kampeni za wapi ambako hajasema atakacho fanya hujasikia kiwa atapeleka madaraka kwa wananchi kwa kuanzisha serikali za majimbo ili wawe na maamuzi kuhusu maendeleo yao badala ya kuwa ombaomba kuna sera nzuri na ya ukweli kama hiyo ulipe kodi halafu mtu asema hawezi kukujengea barabara sababu umechagua upinzani kukiwa na serikali za majimbo hakutakuwa na mtu wa kuamuwa akenge uwanja wa kimataifa chato badala ya kujenga Njombe ambayo ilikuwepo kwenye ilani, pamoja na mitano mingine.
 
Yeye Lissu atafanya nini akipewa nchi,watanzania mpaka sasa wanakaa kusubiri labda atatueleza siku zijazo lakini Lissu ameshindwa kabisa kutueleza.

Mbona kila siku anaeleza atakacho fanya labda wewe umasikiliza mgombea mwengine maana yeye hana media zinazomcover kama huyo ,wenzake lakini kila mkutano anaeleza sera za chama chake. Na alipohojiwa ITV pia hukusikia sera zake au utakuwa huwa unaangalia TBC ndiyo maana huwezi kusikia sera za CDM
 
“Mtu anawaambia hamtolipa kodi,halafu akimaliza anaanza kuwachangisha pesa, analeta vibakuli, vinaendana hivyo Ndugu zangu!?, Watanzania mjitambue, si angekuwa hawaombi hata nyinyi anaowahubiria, akiingia fedha zilizokusanywa watazila zote,Majuto ni Mjukuu”-JPM akiwa Kagera

Imawezekana alimsikiliza Lisu mwengine siyo yule tuliyemsikiliza wote aliyesema atafuta kodi zisizolenga kumwendeleza mfanyabiashara kama hizo za kulipia vitambulisho vya machinga na hizo za kutoza mazao barabarani.
 
Wenyewe wakisoma kichwa hapo wanakimbilia. Wakishasoma wanafunga kimya kimya bila comment!
 
Yeye Lissu atafanya nini akipewa nchi,watanzania mpaka sasa wanakaa kusubiri labda atatueleza siku zijazo lakini Lissu ameshindwa kabisa kutueleza.
Inaelekea hufuatulii mikutano yake,maana bila hiana anaelezea nini atakachofanya pindi atakapochaguliwa.
 
Kwa kweli mgombea Tundu Lissu anasikitisha sana kutoa matusi mazito kabisa na kudhalilisha wenzie. Kwa haraka haraka nimeyanyaka baadhi ya matusi yake ambayo yanalalamikiwa sana:
  1. Ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato ambao haukufuata utaratibu na haukupitishwa na bunge
  2. Wafanyakazi kutopata nyongeza ya mshahara kwa miaka mitano
  3. Kukosekana kwa uhuru wa kutoa maoni kulikopelekea kutungwa sheria kandamizi
  4. Kujali maendeleo ya vitu badala ya watu
  5. Kunyima vyama vya siasa uhuru wa kikatiba wa kufanya siasa
  6. Matumizi mabaya ya fedha za mifuko ya bima ya afya na hifadhi, matumizi kinyume na malengo. Zikikopwa hazirudishwi
  7. Ongezeko kuuuubwa la makato ya Bodi ya Mikopo toka 8% mpaka 15%
  8. Elimu duni isiyowajenga watoto wetu kujitegemea
  9. Kutokufanyika uchunguzi wa kina wa mauaji, utekaji na kupigwa kwake risasi
  10. Mbinyo kwa vyombo vya habari
  11. Ongeza na wewe matusi mengine, mi nimeweka machache tu
Kama haya ndiyo matusi yanayopigiwa kelele, nampa pole nyingi anayedaiwa kutukanwa. Ukiwa ulingoni unazorushiwa na kutua usoni ingawa ni kweli zinaumiza haziitwi matusi, zinaitwa ngumi na kama huzimudu kwa nini unapanda jukwaani? Ningewashauri mashabiki badala ya kulalamika kwa kushindwa kuita koleo kwa jina lake wamtupie bingwa wao taulo...hiyo inaruhusiwa.
 
Haahaa, pale tume makada wanaumia sana bossi wao anavyosemwa...kiujumla walipaswa kujiuzulu ili waende majukwaani kumsaidia bosi wao
 
Walivyo mshambulia Kwa Risasi 38 waliona Raha, wao ma CCM na mamluki wao maneno Tu yanawachoma kweli kweli
 
Kwa kweli mgombea Tundu Lissu anasikitisha sana kutoa matusi mazito kabisa na kudhalilisha wenzie. Kwa haraka haraka nimeyanyaka baadhi ya matusi yake ambayo yanalalamikiwa sana:
  1. Ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato ambao haukufuata utaratibu na haukupitishwa na bunge
  2. Wafanyakazi kutopata nyongeza ya mshahara kwa miaka mitano
  3. Kukosekana kwa uhuru wa kutoa maoni kulikopelekea kutungwa sheria kandamizi
  4. Kujali maendeleo ya vitu badala ya watu
  5. Kunyima vyama vya siasa uhuru wa kikatiba wa kufanya siasa
  6. Matumizi mabaya ya fedha za mifuko ya bima ya afya na hifadhi, matumizi kinyume na malengo. Zikikopwa hazirudishwi
  7. Ongezeko kuuuubwa la makato ya Bodi ya Mikopo toka 8% mpaka 15%
  8. Elimu duni isiyowajenga watoto wetu kujitegemea
  9. Kutokufanyika uchunguzi wa kina wa mauaji, utekaji na kupigwa kwake risasi
  10. Mbinyo kwa vyombo vya habari
  11. Ongeza na wewe matusi mengine, mi nimeweka machache tu
Replies #74
Likes #80[emoji1536][emoji818][emoji1536][emoji818][emoji818][emoji1536][emoji818][emoji777][emoji617][emoji777][emoji617][emoji777][emoji617]
 
Mi naona Magufuli aache kumjibu Lissu...

Maana ataumbuka pakubwa.

Sasa hili tusi la jana... Mjomba...mpwa na mme mwenza ...hakuna mccm yeyote anaweza jibu.
 
Hizo hoja azijibu siyo anatufokea
 
Ila Lissu naye apunguze matusi. Lile la 1.5 trillions mbona analisema chini chini?
1.5 trillion naona haigusii inabidi nayo atilie msumali, pia CAG Assad alivyofanyiwa figisu baada ya kugundua ufisadi huu
 
Back
Top Bottom