Orodha ya Miji na Wilaya zenye mzunguko mkubwa wa Fedha na Uhakika wa Mapato

Orodha ya Miji na Wilaya zenye mzunguko mkubwa wa Fedha na Uhakika wa Mapato

Hivi inamaana iyo miji yenye mzunguko wa pesa, watu wanaishi kwenye hio miji wote wana maisha mazuri(wana pesa)?
 
Hizo ni Manispaa uchwara,huko wanawakilishwa na Muleba na Misenyi
Mkoa wa kagera umeendelea zaidi vijijini kuliko mjini.

Na hizi report ndo zinaonyesha jinsi vijiji vya nshomile wahaya vilivyoendelea


Ni kawaida kukuta shule nzr,nyumba nzr vijijini.


Na niipongeze wilaya za muleba na misenyi wanajitahidi Sana kujenga barabara za vijijini na maji na umeme. Nyumba za watu katika wilaya hiz ni mahekalu.



Acha bukoba mjini izidi kuwa mji mdogo wenye mandhari na hali ya hewa nzr maana wahaya hufanya shopping mjini hapo na kurudi vijijini kwao ndo maana bukoba Kuna stendi nyingi za daladala za vijijini
 
Hizo ni Manispaa uchwara,huko wanawakilishwa na Muleba na Misenyi
Vijijini huko muleba.


Maisha ya vijiji vya kagera hakuna wa kuyafikia tz nzima.


Bukoba sio manispaa uchwara Ina hadhi yake na umekaa kistarehe na mapumziko zaidi. Wacha hubaki hivyo hivyo mdogo lakin uliopangiliwa na kujengeka na zile beach zake
Screenshot_20210730-103856.jpg
 
Mbeya on top kila siku.
Halafu kuna kenge za mashambani huko zinabana pua "Mbeya mnaendekeza ushirikina"
Nyie walokole mko wapi?
Mzunguko wa fedha mbeya kuwa mzuri ni changizo kubwa la kuwa center ya mpaka wa nchi mbili na lango la nchi hizo
 
Figure nilikosea kidogo ni 1.45bView attachment 1875045

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Angalia table nyingine hii ya mikopo ina mislead na ni ya robo ya mwisho ila table nyingine ni ya jumla.

Tamisemi wanazingua Sana ukisoma taarifa ya Waziri ni tofauti na attachment walizoweka .Hata Lindi MC madiwani wamelalamika kwamba wameitwa wa mwisho wakati kiuhalisia sio wa mwinyo.

Wameenda mbali kwamba mapato aliyotoa Waziri na asilimia sio sahihi.
 
Kongole sana, serikali izidi kuwekeza kwenye miundombinu ya barabara, maji, umeme, afya, elimu na kuchochea uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali ili wilaya nyingi zaidi zifunguke.
 
No 8.. Arusha CC
No 45. Arusha DC

Inakanganyisha hii....

Hii list naona kanda ya Kaskazini imepigwa dafrao la kufa mtu...
Waongo hawa, hawana utafiti yakinifu na wa kutosha

Eti Karatu na Masasi inaizidi Arusha DC???
 
Kongole sana, serikali izidi kuwekeza kwenye miundombinu ya barabara, maji, umeme, afya, elimu na kuchochea uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali ili wilaya nyingi zaidi zifunguke.
Umeongea jambo la msingi,maeneo mengi yalikuwa hayafikiki Ili kuyafungua kwa fursa mbalimbali ikapelekea maendeleo kuwa Dar na mikoa ya Kaskazini pekee.

Lakini kadiri miaka inavyokwenda mambo yanaenda kuwa tofauti nadhani unaweza ona hapo juu mikoa kama Lindi,Mtwara,Pwani imeanza kutokea kwenye list.

Kwa miaka mingi Tulikuwa tunaambiwa niaskini sababu ya miundombinu hafifu lakini ni maeneo yenye fursa nyingi.
 
Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Tanzania.

Ifuatayo ni List ya Miji,Majiji,Manispaa na Wilaya 50 Kati ya 184 ambazo zina mzunguko Mkubwa wa fedha na kwamba wananchi wake Wana kipato cha uhakika na hivyo kuwa maeneo yanayofaa zaidi kwa fursa za biashara mbalimbali.

Mpangilio umewekwa kwa kuangalia wingi wa mapato halisi kuanzia kiasi cha Tsh. bilioni 3.5 na kuendelea yaliyokusanywa na Halmashauri mwaka wa fedha 2020/21 kutoka vyanzo vya shughuli za kiuchumi za wananchi kama biashara,kilimo,ufugaji,viwanda nk. Figures in Tsh.bilion

1.Dar es Salaam CC(Ilala) = 48.17

2.Dodoma CC=36.32

3.Kinondoni MC=33.11

4.Temeke MC=28.05

5.Mbeya CC=15.27

6.Ubungo MC=14.22

7.Mwanza CC=12.70

8.Arusha CC=12.36

9.Tanga CC=11.07

10.Chalinze DC=9.64

11.Geita TC=9.38

12.Kahama MC=7.98

13.Ilemela MC=7.76

14.Mkuranga DC=7.65

15.Njombe TC=7.50

16 . Morogoro MC=7.18

17.Kigamboni MC=6.90

18.Mufindi DC=6.52

19.Tunduma TC=6.33

20.Tarime DC=5.76

21.Rungwe DC=5.53

22.Moshi MC=5.21

23.Rufiji DC=5.21

24.Mbarali DC=5.13

25.Geita DC=4.92

26.Muleba DC=4.84

27.Kibaha TC=4.54

28.Mafinga TC=4.36

29.Nachingwea DC=4.30

30.Kilwa DC=4.22

31.Hanang' DC=4.16

32.Kilosa DC=4.16

33.Tandahimba DC=4.10

34.Mbeya DC=4.06

35.Ruangwa DC=4.03

36.Mbozi DC=3.95

37.Msalala DC=3.92

38.Mbinga DC=3.76

39.Kyela DC=3.75

40.Misenyi DC=3.68

41.Kaliua DC=3.65

42.Morogoro DC=3.62

43.Masasi DC=3.62

44.Karatu DC=3.57

45.Arusha DC=3.54

46.Njombe DC=3.54

47.Tunduru DC=3.51

48.Meru DC=3.50

49.Mtwara MC=3.46

50.Chato DC=3.46




My Take.Hizi Takwimu zinaonesha Uchumi unakua,mwaka wa fedha uliopita kulikuwa na Halmashauri 37 tuu lakini sasa ziko 50 zilizokidhi vigezo.

Takwimu hizi ni kwa Mujibu wa website ya Tamisemi.👇
2021 kilimanjaro inaongoza kwa mzunguko n watu wenye maisha bora
 
Umeongea jambo la msingi,maeneo mengi yalikuwa hayafikiki Ili kuyafungua kwa fursa mbalimbali ikapelekea maendeleo kuwa Dar na mikoa ya Kaskazini pekee.

Lakini kadiri miaka inavyokwenda mambo yanaenda kuwa tofauti nadhani unaweza ona hapo juu mikoa kama Lindi,Mtwara,Pwani imeanza kutokea kwenye list.

Kwa miaka mingi Tulikuwa tunaambiwa niaskini sababu ya miundombinu hafifu lakini ni maeneo yenye fursa nyingi.
Kweli kabisa, hivi karibuni nilienda kijijini kwetu nikakuta barabara ya lami inayounganisha na makao makuu ya wilaya ikikaribia kukamilika na umeme wa REA una almost miaka mitano jambo ambalo lilikuwa ndoto enzi hizo nikiwa mdogo, sasa serikali ikiwa focused kwenye initiative kama hizi tutajikuta tunafungua fursa nyingi zaidi kwenye nchi ambazo zitasaidia ku-absorb tatizo la upungufu wa ajira kwa vijana na hata kujenga jamii ya watu wa kisasa ambao wataachana na mediocre minds za kuishi kwa hisia au kwa imani za kishirikina......
 
Back
Top Bottom