Orodha ya Miji na Wilaya zenye mzunguko mkubwa wa Fedha na Uhakika wa Mapato

Orodha ya Miji na Wilaya zenye mzunguko mkubwa wa Fedha na Uhakika wa Mapato

Kweli kabisa, hivi karibuni nilienda kijijini kwetu nikakuta barabara ya lami inayounganisha na makao makuu ya wilaya ikikaribia kukamilika na umeme wa REA una almost miaka mitano jambo ambalo lilikuwa ndoto enzi hizo nikiwa mdogo, sasa serikali ikiwa focused kwenye initiative kama hizi tutajikuta tunafungua fursa nyingi zaidi kwenye nchi ambazo zitasaidia ku-absorb tatizo la upungufu wa ajira kwa vijana na hata kujenga jamii ya watu wa kisasa ambao wataachana na mediocre minds za kuishi kwa hisia au kwa imani za kishirikina......
Ukirudi 2025 utakuta tofauti Sana maana saizi serikali imeongeza bajeti za barabara,maji na masuala ya Afya na Elimu.La umeme tayari kwa hiyo hakuna haja tena ya kukimbilia miji mikubwa.
 
CC = City Council na DC = District Council sasa hapo inabaki mipAka ya kiutawala
Sio kwanba sikujua tofauti ya DC na CC... tatizo sijajua mipaka ya kiutawala iko wapi... Na hiyo mbona hatuioni Dar Es Salaam? Ningependa kuona Ilala CC na Ilala DC i
 
Tuomeshwe na Ilala CC Vs Ilala DC kama ipo mipaka ya kiutawala.

Kiongozi ulidhanj nilikuwa sijui CC ni City Council?
Hii sio maudhui ya Uzi iLa ukienda kwa mkurugenzi au Meya atakupa mipaka ya Ilala CC na ukienda kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala atakupa ramani ya mipaka ya Ilala DC .

Hizo unazoona zina DC pekee inamaanisha makao makuu ya Wilaya hayajakidhi vigezo vya miji na hivyo kuwa consired as Rural areas tofauti na maeneo ya Miji, Manispaa na Majiji(TC,MC na CC) .

Kuna Wilaya yaani DC mfano Mimba DC ina makao makuu ya Wilaya sehemu fulani ni kamji kadogo lakini ndani ya Wilaya husika kuna Mji mkubwa ambao ni Tunduma TC,,hapo Mkuu wa Wilaya ya Momba anaongoza Halmashauri 2 nk.

Pia utashangaa zaidi maana kuna Mkoa ambao makao makuu ya mkoa hayana hadhi ya Mji,Manispaa wala Jiji ni just Mji mdogo kama Mkoa wa Songwe ambao makao makuu yake yako kwenye Mji mdogo unaitwa Vwawa ambao ni makao makuu ya Wilaya ya Mbozi yaani Mbozi DC.
 
Hii sio maudhui ya Uzi iLa ukienda kwa mkurugenzi au Meya atakupa mipaka ya Ilala CC na ukienda kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala atakupa ramani ya mipaka ya Ilala DC .

Hizo unazoona zina DC pekee inamaanisha makao makuu ya Wilaya hayajakidhi vigezo vya miji na hivyo kuwa consired as Rural areas tofauti na maeneo ya Miji, Manispaa na Majiji(TC,MC na CC) .

Kuna Wilaya yaani DC mfano Mimba DC ina makao makuu ya Wilaya sehemu fulani ni kamji kadogo lakini ndani ya Wilaya husika kuna Mji mkubwa ambao ni Tunduma TC,,hapo Mkuu wa Wilaya ya Mimba anaongoza Halmashauri 2 nk
Asprin says thank you Opportunity Cost for this useful post
 
Mzunguko wa fedha mbeya kuwa mzuri ni changizo kubwa la kuwa center ya mpaka wa nchi mbili na lango la nchi hizo
Siyo chini ya serikali hii ya kipumbavu.
wanashindwa hata kuendeleza miundombinu tu ya jiji kwa sababu za kibaguzi na kisiasa.
 
Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Tanzania.

Ifuatayo ni List ya Miji,Majiji,Manispaa na Wilaya 50 Kati ya 184 ambazo zina mzunguko Mkubwa wa fedha na kwamba wananchi wake Wana kipato cha uhakika na hivyo kuwa maeneo yanayofaa zaidi kwa fursa za biashara mbalimbali.

Mpangilio umewekwa kwa kuangalia wingi wa mapato halisi kuanzia kiasi cha Tsh. bilioni 3.5 na kuendelea yaliyokusanywa na Halmashauri mwaka wa fedha 2020/21 kutoka vyanzo vya shughuli za kiuchumi za wananchi kama biashara,kilimo,ufugaji,viwanda nk. Figures in Tsh.bilion

1.Dar es Salaam CC(Ilala) = 48.17

2.Dodoma CC=36.32

3.Kinondoni MC=33.11

4.Temeke MC=28.05

5.Mbeya CC=15.27

6.Ubungo MC=14.22

7.Mwanza CC=12.70

8.Arusha CC=12.36

9.Tanga CC=11.07

10.Chalinze DC=9.64

11.Geita TC=9.38

12.Kahama MC=7.98

13.Ilemela MC=7.76

14.Mkuranga DC=7.65

15.Njombe TC=7.50

16 . Morogoro MC=7.18

17.Kigamboni MC=6.90

18.Mufindi DC=6.52

19.Tunduma TC=6.33

20.Tarime DC=5.76

21.Rungwe DC=5.53

22.Moshi MC=5.21

23.Rufiji DC=5.21

24.Mbarali DC=5.13

25.Geita DC=4.92

26.Muleba DC=4.84

27.Kibaha TC=4.54

28.Mafinga TC=4.36

29.Nachingwea DC=4.30

30.Kilwa DC=4.22

31.Hanang' DC=4.16

32.Kilosa DC=4.16

33.Tandahimba DC=4.10

34.Mbeya DC=4.06

35.Ruangwa DC=4.03

36.Mbozi DC=3.95

37.Msalala DC=3.92

38.Mbinga DC=3.76

39.Kyela DC=3.75

40.Misenyi DC=3.68

41.Kaliua DC=3.65

42.Morogoro DC=3.62

43.Masasi DC=3.62

44.Karatu DC=3.57

45.Arusha DC=3.54

46.Njombe DC=3.54

47.Tunduru DC=3.51

48.Meru DC=3.50

49.Mtwara MC=3.46

50.Chato DC=3.46




My Take.Hizi Takwimu zinaonesha Uchumi unakua,mwaka wa fedha uliopita kulikuwa na Halmashauri 37 tuu lakini sasa ziko 50 zilizokidhi vigezo.

Takwimu hizi ni kwa Mujibu wa website ya Tamisemi.[emoji116]

Mr Opportunity vipi Makambako haipo mbele ya Njombe?
Vipi takwim za kila mkoa zikoje?
Yaani miji kama Tarime, Korogwe,Namanga, Tabora, Kigoma, Iringa haina kitu? Takwim hizi mmmmh
 
Mr Opportunity vipi Makambako haipo mbele ya Njombe?
Vipi takwim za kila mkoa zikoje?
Yaani miji kama Tarime, Korogwe,Namanga, Tabora, Kigoma, Iringa haina kitu? Takwim hizi mmmmh
Kale kamji ka Makambako na hiyo miji mingine ni Utopolo towns as usual..ni maarufu kwa uchuuzi usio na tija kulinganisha na maeneo yenye shughuli rasmi za maana.

Makambako TC ni aibu tupu yaani wali collect only 2.62 bln na inaaibisha Mkoa wetu ,jina kubwa lakini hamna kitu.
 
Kwahiyo wilaya yangu pendwa ya musoma mjini aipo[emoji23] hakika kumbe nilikuwa sahihi kuikimbia hiyo wilaya kama mpaka tumezidiwa na wilaya ya mwenda zake bac hatuna maana yoyote

Nashangaa sana kuna machimbo ya Lwabasi, Buhemba, kinyambwiga na maeneo mengine ukienda ofisi ya madini mapato yanayokusanywa pale si mchezo eti Musoma haipo wajita wakwaya nimewagwaya
 
Nashangaa sana kuna machimbo ya Lwabasi, Buhemba, kinyambwiga na maeneo mengine ukienda ofisi ya madini mapato yanayokusanywa pale si mchezo eti Musoma haipo wajita wakwaya nimewagwaya
Madini sio chanzo cha Halmashauri bali wizara husika ndio inatoa leseni na kuratibu shughuli zote za Madini.
 
Back
Top Bottom