Orodha ya Miji yenye hadhi isiyostahili

Sijajua mtaani kupoje, ila kwenye Lodge niliyopo sijakutana na changamoto ya maji mwezi wa pili sasa.

lakini pia utamaduni wao wa namna wanavyojenga nyumba zao kidogo unaharibu muonekano wa mji
Mwezi wa pili unakaa lodge mkuu?

Yes kuhusu ujenzi wengi naona bado hawana exposure. Hata mafundi ni wachache wanaoweza kufanya ujenzi makini sana
 
Kwingne huko sijawahi kbs kufika ila naomba nikiri Singida na Shy hiyo mikoa haina hadhi ya Manispaa, Shinyanga imezidiwa na wilaya yake kbs ya Kahama kwa kila kitu.

Lindi hata sitaman kwenda, Songea sijawah kupafikiria kbs.

Majiji yasiyo na hadhi na yamekaa kiboya ni Tanga na kaka yake Mbeya, Dodoma kwa sasa imeivaaa.
 
Bukoba manispaa ingekua imebadilika mpaka sasa, ukilinganisha na umri wake Toka tuipate ila viongozi wetu wamehudika pakubwa katika kuikosesha sifa, hata mwonekano unaoipamba angalau kidogo ni kwa sababu ya mabadiliko tulio kua tumefanya ya kuweka viongozi wengi wa upande wa Chadema.
 
Mara ya mwisho kutembelea Singapore ilikuwa lini?
 
Huwa natoka kwenda vijijini na kurudi, sio mkazi mkuu. Njaa tu ndio imenifikisha huku, Kirando, Kipili, Kabwe, Mtowisa na maeneo mengine ndo nimekuwa nikizinguka mara nyingi
Mi kila nikija Sumbawanga kuna samaki fulani ni mtamu anaitwa Kuhe ila anauzwa bei kubwa kiasi. Siwezi acha kumla aseeh. Wanamuita kuku wa ziwani.
Kwa mara ya kwanza nimefika kipili ilikua 2005 ila Kirando sikuwahi kufika.

Umenikumbusha mbali aseeh. Nataka kufanya tour nyingine nifike Lupita Island
 
Majiji ni matatu tu
Dar
Mwz
Dom
Hebu ondoa dodoma hapo, kumbuka dodoma ilipandishwa hadhi kisiasa tu, na hata magufuli alikiri hivyo siku anaitangaza dodoma kuwa jiji, alisema "dodoma ndiyo makao makuu ya nchi, sasa itakuwa ajabu kama makao makuu yasipokuwa na hadhi ya jiji, hivyo kuanzia leo natangaza kuwa dodoma ni jiji," so factors nyinginezo hazikuzingatiwa, unlike Arusha ambayo tayari ilishakuwa jiji kwa vigezo stahiki, learn or perish
 
Labda utazame hii video kuhusu Bukoba na utaona waliioita Bukoba municipality miaka ya 90 hawakuwa wajinga....

Huu mji una busy Airport, uwanja mzr wa kapeti kaitaba, bandari ya pili kwa ukubwa kanda ya ziwa, hotel za nyota 3 kibao, mtandao mkubwa wa Barabara za lami na kwa kanda ya ziwa Bukoba ndo mji wa pili baada ya mwanza kwa idadi ya maghorofa ( sensa 2022)

Miradi inayoendelea ni ujenzi wa Barabara ya njia nne km 5, stendi ndogo ya mjini kati, stendi kubwa, chuo kikuu nk


View: https://youtu.be/rBYKFm9U19w?si=h1GCv0cpy0sG_sQN
 
Mkuu umetisha sana. Hujamla kuhe wa Ziwa Victoria hautamtamani wa Ziwa Tanganyika tena 🤣 🤣
 
Video yako inazunguka eneo moja tu, haina maana yoyote.
 
Babati
 
Singida nilipita ila pazuri, shinyanga wala kahama sijawahi kufika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…