1. Kuota mwezi kunajulisha waziri, mfalme mkubwa, au sultani, nakama mwezi utakua umeambatana pembezoni mwake nyota basi ni kiongozi Na askari wake, Na inajulisha makazi ya kiongozi huyo Na maskani yake Na wakeze Na jirani zake.
2. Lakini huenda Njozi ya mwezi ikajulisha elimu, fiqih, na kila kinachojulisha uongofu Kwa mtu akaongoka kwacho katika magiza ya bara Na bahari.
3. Lakini pia mwezi unajulisha mtoto au mume au bwana.
4. Lakini pia nuru ya mwezi unajulisha uzuri Wa wanawake Na uzuri wa wanaume.
5. Lakini pia mwezi unajulisha kuongezewa kipato au kupungukiwa kipato, kwakua mwezi kawaida yake huongezeka ukubwa na unapungua ukubwa, kama jinsi zilivyo kazi za watu, huongezekewa Na kazi Na hupungukiwa kazi, huongezekewa na kipato Na hupungukiwa Na kipato.
6. Lakini pia kama utauona mwezi ukiwa kipande basi Njozi inakujulisha kupungukiwa umri na kukaribia ajali yako, kulingana Na masiku yaliyobaki ya mwezi huo kipande tokea ulipo uona.
7. Lakini pia utakapouona mwezi ukiwa umechomoza tena Kwa kujificha katika mawingu, basi utatoka maeneo yako na utasafiri.
8. Lakini pia utakapo uona mwezi ukiwa ndio umefikia siku ya mwisho wa mwezi, utasfiri safari ya mbali kutoka katika mji wako.
9. Lakini pia utakapouona mwezi upo nyumbani kwako, au chumbani kwako, au upo mkononi kwako, basi utaoa mke mzuri au utaolewa Na mume mzuri kulingana na ukubwa Wa mwanga wa mwezi Na kulingana Na ukubwa wa nuru ya mwezi.
10. Lakini pia ukiuona mwezi unazama mpaka ukapotea, basi jambo ambalo ulilokua ukilitafuta la Kheri au la shari limekwisha malizika.
11. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi umekamilika duara lake Na mwezi huo upo katika anga la nyumbani kwake, basi Njozi inakujulisha kua:
"Hakika waziri Wa mfalme, au waziri Wa raisi atawanufaisha watu Wa sehemu hiyo"
12. Mtu anapolala kisha akaota kua, kautazama mwezi kisha akajiona sura yake katika mwezi, basi Njozi inakujulisha kua:
"Ajali yako imekaribia"
13. Mtu anapolala kisha akaota kua, Amening'inia mwezini, basi Njozi inamjulisha kua:
"Utapata Kheri nyingi kutoka Kwa sultani, raisi, waziri"
14. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi mwezi umefifia na akaona malaika akitoka mwezini, basi Njozi inakujulisha kua:
"Wachungwa wake watamuudhi Na watamkana"
15. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi umegeuka na umekua jua, basi Njozi inakujulisha kua:
"Muotaji atapata Kheri nyingi, atapata utukufu mkubwa, atapata Mali nyingi, yote hayo kutoka umamani kwake au Kwa mwanamke wake"
16. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi umejificha mawinguni, basi Njozi inakujulisha kua:
"Hayo ni maradhi yatakayompata waziri, na atapona baadae"
17. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi unakatiza mawinguni, basi Njozi inakujulisha kua:
"Utajiuzuru kazi ya uongozi"
18. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi umemuongelesha, basi Njozi inakujulisha kua:
"Utapata cheo Na utasogezwa karibu Na waziri, au raisi"
19. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi upo nyumbani kwake, na huyo muotaji ni mwanamke mjamzito, basi Njozi inakujulisha kua:
"Utazaa mtoto wa kiume"
20. Mtu anapolala kisha akaota kua, analisujudia jua au anausujudia mwezi, basi Njozi inakujulisha kua:
"Unapandanisha madhambi juu ya madhambi, au unamtii mfalme au raisi au kiongozi katika batili"
21. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi na jua vinamsujudia, basi Njozi inakujulisha kua:
"Wazazi wako wawili wamekuridhia"
22. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi unang'ara vizuri, lakini yeye mwenyewe muotaji yupo gizani, basi Njozi inakujulisha kua:
"Nimaongezi yatakayoongelewa Kwa waziri au raisi au kiongozi yatakutia matatani"
23. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi umepasuka vipande viwili, basi Njozi inakujulisha kua:
"Mfalme, au raisi, au waziri ataangamia"
24. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi umegeuka muonekano wake ikawa unaonekana Kwa sura ya mtu unaemjua, basi Njozi inakujulisha kua:
"Waziri, au raisi, au kiongozi atajiuzulu nafasi yake"
25. Mtu anapolala kisha akaota kua, kauona mwezi nae akawa anafanya siri wenzie wasiuone mwezi, basi Njozi nakujulisha kua:
"Siri zako zitafichuka"
26. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi umepatwa na jua, au mwezi umekua mwekundu, au mwezi umekua mweusi, basi Njozi hiyo inakujulisha kua:
"Hayo ni maharibiko katika maisha yako"
MENGINEYO: