Orodha ya ndoto (karibia zote) na maana yake
Je ukiota unakula mahindi ya kukaangwa yatokayo kwenye ghorofa reefu kupita yote duniani kama mnara, ila anayeyateremsha haonekani zaidi ya kuona tu uwazi wa katikati ya hilo ghorofa afu unakinga kwa sufuria na kukaa chini unaanza kula?

Tafadhali msaada wa tafsiri ya hiyo ndoto Chifu.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Je ukiota unakula mahindi ya kukaangwa yatokayo kwenye ghorofa reefu kupita yote duniani kama mnara, ila anayeyateremsha haonekani zaidi ya kuona tu uwazi wa katikati ya hilo ghorofa afu unakinga kwa sufuria na kukaa chini unaanza kula?

Tafadhali msaada wa tafsiri ya hiyo ndoto Chifu.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Utapata neema

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, acha kabisa. Mimi vita ndio huwa ndoto zangu, hata sielewi ni nini yani. Huwa naota vita, yaani tumevamiwa, na wanajeshi huwa wamevaa kabisa nguo za kijeshi. Wanaingia mtaani, wanaanza kusaka watu. Mi nikiwa mmoja,wao, basi tunajificha. Mara nyingine wanatuona, nikikimbia nakutana nao, risasi zinakuwa zinapigwa. Ndoto zote za vita huwa zinakuwa mida ya jioni, yani kama saa 12 hivi kuelekea saa moja maana kunakuwaga hakuna jua. Juzijuzi tu, nimeota vita tena. Ndoto imeishia nimekmbia kuwakimbia wanajeshi, kumbe nilikokimbilia ndio nikakutana nao wawili. Mmoja akanielekezea bunduki, ile anataka tu kunifyatulia nikashtuka ghafla. Nilivyoshtuka nikakuta nwili wote unatetemeka, moyo unaenda mbio.
Sijui ndoto za vita huwa zina maana gani maana kwangu hiwa zinajirudia mara kwa mara.
Pole sana ndugu yangu, sasa sijui tuna wito wa kuingia jeshini ama ni vipi. Maana Da! Siyo mchezo
 
Nimeota nakutana na mwanamke mfupi sana kwenye ndoto nikawa namkemea, kwenye ndoto nilikuwa nawaza ni kibwengo.
 
Mkuu nimeota nipo mama kijijini tuna piga story vizuri tu lakini nimelala kwenye mkeka macho yangu yameelekea juu mawinguni

Naona anga la blue la usiku na nyota zake pamoja na mwezi lakini gafra nikaona jua linakamatwa na mwezi na pembeni pa hilo tukio niliona nyota 24 zikiwa zimeji panga nnenne mala 6 Yani Kama hivi

****
****
****
****
****
****
Nikiwa nashangaa hili tukio nyuma yangu Nika mwona mnyama poli anaye fanan napaa au swala alikuwa na langi ya kahawia

Nilipo mtazama vizuri niligundua nikama alijeruhiwa miguu ya nyuma na Simba huko alilo toka

Lakini nyuma ya yule paa Kama ulefu wa uwanja wa mpila nikaona Simba ambaye nahisi ndiye aliye mkosa yule paa akimkamata nguluwe pale nyumbani na kuondoka nae kwa speed

Na kilicho nishangaza zaidi nipale nilipo mwona mama akimsaidia yule paa na kizungumzia kwa lugha ambayo wanaelewana

Sasa najiuliza Nini maana ya kupatwa kwa jua nikiwa natazama?

Nini maana ya zile nyota 24 kupangika vile mbele ya macho yangu

Nini maana ya paa katika ndoto na ile maana ya kujeruhiwa miguu ya nyuma nakukimbilia pale nyumbani ili asaidiwe na akasaidiwa ?

Nanini maana ya yule Simba kumnyakua ngulue na kukimbia nae?

🙏🙏🙏
Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi umepatwa na jua, au mwezi umekua mwekundu, au mwezi umekua mweusi, basi Njozi hiyo inakujulisha kua:
"Hayo ni maharibiko katika maisha yako"
 
Je ukiota unakojoa?

Kuota unakojoa au kujisaidia mara kwa mara si vizuri.​

Kuota unakojoa si vizuri ila ni hatari sana kwa maisha yako, hii ni dalili za nguvu za giza ikiwemo mikosi na nuksi.

Ninakwambia jitahidi kufuatilia ndoto hizi ambazo ni mbaya kiafya katika ulimwengu wa kiroho:-

  • Kuota unakojoa, unajisaidia au uko sehemu chafu
  • Kuota unakula vitu au chakula mara kwa mara
  • Kuota maiti na watu waliokufa siku nyingi
  • Kuota vifo vya jamaa waliokaribu na wewe
  • Kuota nyoka na paka weusi mara kwa mara
  • Kuota unashambuliwa na watu
  • Kuota uko msituni na watu usio wajua
 
1. Kuota mwezi kunajulisha waziri, mfalme mkubwa, au sultani, nakama mwezi utakua umeambatana pembezoni mwake nyota basi ni kiongozi Na askari wake, Na inajulisha makazi ya kiongozi huyo Na maskani yake Na wakeze Na jirani zake.

2. Lakini huenda Njozi ya mwezi ikajulisha elimu, fiqih, na kila kinachojulisha uongofu Kwa mtu akaongoka kwacho katika magiza ya bara Na bahari.

3. Lakini pia mwezi unajulisha mtoto au mume au bwana.

4. Lakini pia nuru ya mwezi unajulisha uzuri Wa wanawake Na uzuri wa wanaume.

5. Lakini pia mwezi unajulisha kuongezewa kipato au kupungukiwa kipato, kwakua mwezi kawaida yake huongezeka ukubwa na unapungua ukubwa, kama jinsi zilivyo kazi za watu, huongezekewa Na kazi Na hupungukiwa kazi, huongezekewa na kipato Na hupungukiwa Na kipato.

6. Lakini pia kama utauona mwezi ukiwa kipande basi Njozi inakujulisha kupungukiwa umri na kukaribia ajali yako, kulingana Na masiku yaliyobaki ya mwezi huo kipande tokea ulipo uona.

7. Lakini pia utakapouona mwezi ukiwa umechomoza tena Kwa kujificha katika mawingu, basi utatoka maeneo yako na utasafiri.

8. Lakini pia utakapo uona mwezi ukiwa ndio umefikia siku ya mwisho wa mwezi, utasfiri safari ya mbali kutoka katika mji wako.

9. Lakini pia utakapouona mwezi upo nyumbani kwako, au chumbani kwako, au upo mkononi kwako, basi utaoa mke mzuri au utaolewa Na mume mzuri kulingana na ukubwa Wa mwanga wa mwezi Na kulingana Na ukubwa wa nuru ya mwezi.

10. Lakini pia ukiuona mwezi unazama mpaka ukapotea, basi jambo ambalo ulilokua ukilitafuta la Kheri au la shari limekwisha malizika.

11. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi umekamilika duara lake Na mwezi huo upo katika anga la nyumbani kwake, basi Njozi inakujulisha kua:
"Hakika waziri Wa mfalme, au waziri Wa raisi atawanufaisha watu Wa sehemu hiyo"

12. Mtu anapolala kisha akaota kua, kautazama mwezi kisha akajiona sura yake katika mwezi, basi Njozi inakujulisha kua:
"Ajali yako imekaribia"

13. Mtu anapolala kisha akaota kua, Amening'inia mwezini, basi Njozi inamjulisha kua:
"Utapata Kheri nyingi kutoka Kwa sultani, raisi, waziri"

14. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi mwezi umefifia na akaona malaika akitoka mwezini, basi Njozi inakujulisha kua:
"Wachungwa wake watamuudhi Na watamkana"

15. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi umegeuka na umekua jua, basi Njozi inakujulisha kua:
"Muotaji atapata Kheri nyingi, atapata utukufu mkubwa, atapata Mali nyingi, yote hayo kutoka umamani kwake au Kwa mwanamke wake"

16. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi umejificha mawinguni, basi Njozi inakujulisha kua:
"Hayo ni maradhi yatakayompata waziri, na atapona baadae"

17. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi unakatiza mawinguni, basi Njozi inakujulisha kua:
"Utajiuzuru kazi ya uongozi"

18. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi umemuongelesha, basi Njozi inakujulisha kua:
"Utapata cheo Na utasogezwa karibu Na waziri, au raisi"

19. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi upo nyumbani kwake, na huyo muotaji ni mwanamke mjamzito, basi Njozi inakujulisha kua:
"Utazaa mtoto wa kiume"

20. Mtu anapolala kisha akaota kua, analisujudia jua au anausujudia mwezi, basi Njozi inakujulisha kua:
"Unapandanisha madhambi juu ya madhambi, au unamtii mfalme au raisi au kiongozi katika batili"

21. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi na jua vinamsujudia, basi Njozi inakujulisha kua:
"Wazazi wako wawili wamekuridhia"

22. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi unang'ara vizuri, lakini yeye mwenyewe muotaji yupo gizani, basi Njozi inakujulisha kua:
"Nimaongezi yatakayoongelewa Kwa waziri au raisi au kiongozi yatakutia matatani"

23. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi umepasuka vipande viwili, basi Njozi inakujulisha kua:
"Mfalme, au raisi, au waziri ataangamia"

24. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi umegeuka muonekano wake ikawa unaonekana Kwa sura ya mtu unaemjua, basi Njozi inakujulisha kua:
"Waziri, au raisi, au kiongozi atajiuzulu nafasi yake"

25. Mtu anapolala kisha akaota kua, kauona mwezi nae akawa anafanya siri wenzie wasiuone mwezi, basi Njozi nakujulisha kua:
"Siri zako zitafichuka"

26. Mtu anapolala kisha akaota kua, mwezi umepatwa na jua, au mwezi umekua mwekundu, au mwezi umekua mweusi, basi Njozi hiyo inakujulisha kua:
"Hayo ni maharibiko katika maisha yako"
MENGINEYO:
 
Je ukiota upo kanisani au msikitini? Na pia ukiota unaongea na kiongozi wa nchi ?msaada
 
mkuu mimi nimeota nipo uwanja wa ndege napanda ndege nasafiri na sijui naelekea wapi lakini watu wananiaga kwa kufaraha na wanasherekea mimi kuondoka huku wakinipa baraka zote
 
Sigmund Freud laiti akiona uliyooandika atabaki mdomo wazi, quite typically magic pseudo article of no scientific value.
 
Back
Top Bottom