Orodha ya Watanzania maarufu waliokufa bila kujenga nyumba

Orodha ya Watanzania maarufu waliokufa bila kujenga nyumba

Utakufa bila kufunga macho wewe
Acha ujinga.walojenga hizo nyumba zinawasaidia nini huko kaburini?wangezikwa kwenye nyumba zao basi?? Tena wengine nyumba zao zilishauzwa tena bei chee tu na watu wakala hela wakapita hivi
Acheni kushauri us...Ng...kupangisha ni kuishi kama uko safarini usimame kwenye gari tusidanganyan
 
OP ameongea point sana vijana wa siku hizi hatuna misimamo. Na Jamiiforum forum ya zamani ilikuwa nzuri sana. Natamani Melo afungue jukwaa la wazee kuwafunza vijana. Jamiiforum ya wakina Nyani Ngabu watu walikuwa wanapata changamoto wanapata suluhu humu humu. Aisee nilijifunza mengi sana kipindi hicho. Nipo mbali na nyumbani lakini nikiingia mitandaoni nakereka sana. Yaani hakuna mambo constructive ya kitanzania kwenye internet. Leo nilikuwa YouTube naangalia Millard Ayo najuta stori ya mbwa Arusha akilishwa sumu anafufuka.
 
Mbona apo T I D hayupo nasikia nae anakaa kwa mama ake mpk leo
Yupo kwao kweli kinondoni na aligoma kuhama,aongezwe kwenye list au apotezewe sababu ana fail mwananyamala la watumiaji wa unga(sobber)Hayuko sawa mentally
 
Looo hakuna mtu wa mkoa wa Kilimanjaro hapo
Ila mtoa mada wewe ni mbea unafuatilia ya watu jiulize Elon Musk tajiri number one duniani ana nyumba?
Mohamed Dewji nina uhakika anayo ila sio kipaumbele chake
wanaojenga nyumba ni watu masikini wasiojiamini na maisha
Wewe hujatembea inaonekana nenda Marekani,Ulaya, na nchi zilizoendelea hakuna mtu eti anajenga nyumba wanachukua lease.Nyumba zinajengwa na real estates companies wewe unanunua
 
1. Dkt. Omar Alli Juma
Huyu alikuwa VP kipindi cha BWM, baada ya kufariki akiwa madarakani, familia yake ilitakiwa kupisha nyumba rasmi ya VP iliyopo nyuma ya St Peters Oysterbay ili Dkt. Shein VP mteuliwa aweze kuingia humo, wakawa hawana pa kuweka vyombo, hawana nyumba, ikabidi lori la erikali liwatoe kinguvu na kwenda kusitiriwa kwenye magofu ya Serikali


2. Gilman Rutihinda
Huyu alikuwa gavana wa BoT enzi za Mwinyi, tulimzika Buguruni Malapa maana kwao Ngara hakuwa na nyumba bali kijumba.


3.Brigedia Moses Nnauye
Huyu alikufa mwaka 2000 kama sikosei, ilibidi msiba tuupeleke kwa mzee Makamba maana tulikosa sehemu ya kufunga turubai kwenye zile flats za NHC, utafunga turubai kwenye flats?
Aliwahi kuwa brigedia jeshini,Naibu Waziri ulinzi,Mkuu wa wilaya Bagamoyo,mkuu w mkoa Singida,mhamasishaji wa CCM,Katibu mwenezi CCM,naibu katibu mkuu CCM Nk


4. Profesa Shaba
Huyu sijui yupo hai au, anasifika kuufanyia post mortam mwili wa hayati Sokoine, mpaka anastaafu na kumaliza kiinua mgongo hakuwahi kujenga hata choo. Alipostaafu aliigomea Serikali kuachia nyumba iliyokuwa mitaa ya Shaaban Robert karibu na Gymkhkana DSM.

Akiwatisha kuwa ataanika kilichomuua Sokoine if at all they try to vacate him, wakampotezea.


5. Steven Kanumba
Pamoja na kumiliki gari ya mamilioni kadhaa alikufa hajawahi kujenga hata kiosk

6. Ray Kigosi(yuko hai)
Bado anaishi kwa mama yake Sinza hajui hata mfuko wa cement inatoa tofali ngapi

7.

Itaendelea
😅😅😅 wakiambiwa kujenga wanakwambia samaki samaki hatuendi na nyumba wakifa wanadhalilika
 
Back
Top Bottom