Osama Bin Laden hakuuawa! Miaka zaidi ya 10 sasa

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Nakumbuka sana tulitangaziwa sehemu mbalimbali kuwa Osama hajauawa. Ni propaganda za Wamarekani. Na hoja ikawa kama kweli wamemuua kwa nini wasimwoneshe uso na mwili wake?

Leo hii ni zaidi ya miaka 10 imepita je Osama Bin Laden atakuwa sehemu ametulia tu kimya? Au tukubaliane na ukweli ambao ni mchungu kuwa huyu mwambata aliuawa?

 
....
Mmmmmmm dunia imetulia sanas
 
watu na nadharia zao tu huyo mwamba alijisahau kile kipindi cha ukimya kumbe wahuni wanatafiti taratibu alipo!, na walipobaini walihakikisha hawamkosi maana wangemkosa ile siku basi vyombo vyao vya ulinzi vingeisema ile kauli ya "mayday!".

Huyu mwamba sio kwamba picha zake hazikutoka, zilitoka na akazikwa huko baharini kama angekuwepo tayari angekuwa ameshapapasa ardhi ya marekani!, ikumbukwe na baadhi ya member wa familia yake waliuliwa sio kwa bahati mbaya ni maksudi!.

Watu hupenda tu kutoka na nadharia zao pasipo ukweli wa mambo! maana wanajua watu mnapenda kusikia hivyo vitu!
 
Nilishindwa kuelewa kwanini jamaa waliamua kuutupa mwili wake baharini

Kwanini wasingeuacha huko huko ndugu zake wakamzika

Ila Osama nae alikuwa ameshachoka kukaa kama digidigi
Hakuna ugonjwa wa akili mbaya kama imani!, so kwakulitambua hilo wakaamua wakazike sehemu ambayo ni ngumu kufikika na hapajulikani kwamaana ukiuzika mwili wa huyo jamaa watu wanaweza kwenda kuhiji!, na wakaanza kupata hasira kama zake kwa kusimuliwa hadithi na mambo aliyofanya so wangeibuka wakina osama wengine!..
ogopa kitu kinachoitwa imani na ndio maana mnafunzwa muwe makini na mnachowaaminisha watoto wenu!.
 
Osama angekuwa hai asingekubali kuzushiwa kifo. Lazima angepiga tukio moja halafu atoe video ya kuwasanifu USA.

Osama ni kinyago kilichochongwa na Marekani kutishia wengine ila hatimae kikaja kuitisha Marekani yenyewe.
 
Nilishindwa kuelewa kwanini jamaa waliamua kuutupa mwili wake baharini

Kwanini wasingeuacha huko huko ndugu zake wakamzika

Ila Osama nae alikuwa ameshachoka kukaa kama digidigi
Wazungu walitutangulia mbele kwa uelewa. Walikuwa hatua nyingi sana mbele. Pia kiisilamu mtu aliyekufa vitani anaweza zikwa baharini. Ila pia kama kungekuwa na kaburi lake Osama angeonekana ni shujaa na watu wangeenda kupata mafundisho ya kuwapandishia mzuka huko.
 
waumini wa conspiracy wanasema alishajifia mwenyewe kipindi cha ukimya kutokana na maradhi hivyo wa-US wakapiga tukio la mcongo kuchukua credit.

huo ni miongoni mwa upande wa conspiracy, ila taarifa rasmi US imemshambulia

sasa sisi watazamaji tunaenda na taarifa rasmi, hakuna namna otherwise watu walete uthibitisho
 
Kweli chizi bado hujapona, nikajua utasema sehemu alipo, na ushahidi ukiweka humu kumbe maneno matupu.

Rudi milembe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…