Oscar Oscar, kama kumuita kiongozi wako mpuuzi sio kosa, fanya hivyo basi kwa bosi wako Majizo kama utabaki salama

Oscar Oscar, kama kumuita kiongozi wako mpuuzi sio kosa, fanya hivyo basi kwa bosi wako Majizo kama utabaki salama

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Mchambuzi anayetafuta umaarufu wa kijinga Oscar Oscar anamtetea Manara kuwa ameonewa, hivyo hastahili adhabu.

Kwake yeye kumuita kiongozi wa soka mpuuzi ni jambo la kawaida, namuuliza Oscar kama anaweza kumuita mpuuzi majizzo akabaki salama.

Hoja hapa ni matusi, kiongozi kaambiwa mpuuzi, wewe Oscar ni mwajiriwa hapo efm, unaweza kumuita mpuuzi bosi wako?

Muite siku moja tuone kama utaendelea kukaa mjini, lazima waandishi muwe na logic mnapofanya uchambuzi, mnaipoteza tasnia.

Badala ya kukemea ujinga huo mnaendekeza kwa sababu kuna watu mtawakasirisha, wanawanunulia pombe kali, wanawanunulia suti, shame on u.
 
Huu mfano hauna uhalisia kama utakuwa unahusishwa na kufungiwa Haji Manara. Maana huyo Karia siyo mwajiri wa Manara!

Karia cheo chake siyo kuzuia watu kukaa jukwaa kuu! Jukumu hilo ni la walimzi maalum.

Ni kiherehere chake ndicho kilichomfanya kujibizana na Haji Manara katika mazingira ambayo mtu amepandwa na munkari baada ya timu yake kuwa katika mazingira magumu ya kushinda fainali.

Simtetei Haji Manara kwa sababu siyo shabiki wake. Lakini Wallace Karia pia siyo malaika.

Na ikiwezekana aondokane kabisa na tabia zake za hovyo za kujiona mungu mtu, na pia kutaka aogopwe kwa sababu tu ni rais wa TFF.
 
Mpuuzi maana yake ni mtu anayepuuzia kitu sio tusi, Haji aanzie BAKITA then akate rufaa anashinda mapema tu.
 
mpuuzi/m pu:zi/nominoWord forms: wapuuzi (plural)Ngeli za nomino: a-, wa-mtu mwenye tabia ya kufanya mambo yasiyokuwa na maana; mtu asiyefaa kufuatwa mambo yake
 
Nchi za wenzetu wenye akili, kiongozi sio mungu. Ukizingua, watu "wanarara mbere" na wewe bila wasiwasi. Trump mwenyewe alikua anayakoga matusi kila siku. Kule kwao, uongozi ni dhamana na wananchi ndio maboss wako.

Hapa kwetu sasa. Hata rais wa TFF nae ni mungu mtu.

NB: Manara nae apunguze mdomo!
 
Back
Top Bottom