Othman Masoud wa ACT Wazalendo amfagilia Hayati Magufuli. Hii ina maana gani?

Ingia mtaani kwa wenye nchi uongee huo ugoro wako uone ka na wewe hujawafuata hao.
 
Pamoja na mapungufu yake, lakini kuna baadhi ya maeneo alifanya vema. Si jambo jema kudhani kwamba Magufuli alikuwa mbaya kwa 100%.

Kila binadamu ana mazuri na mabaya yake. Ni viwango tu vinatofautiana. Wengine mabaya yao yanakuwa mengi kuliko mazuri, na wengine mazuri yanakuwa mengi kuliko mabaya. Wengine wanakuwa nusu kwa nusu; Mabaya nusu na mazuri nusu.
 
Ndio maana amesema anatakiwa apatikane MTU mwingine siku za usoni ambaye atakuwa jasiri kama Magufuli lakini atakuwa anaongoza nchi kupitia mifumo imara itakayokuwa imewekwa na katiba mpya !! Sio kumtegemea MTU jasiri aendeshe nchi kwa matakwa yake binafsi !! Mimi nimemuelewa hivyo !!
 
Ujasiri wa Magufuli ni kumwaga damu za Wazanzibari


 
Na inakupasa uelewe kwamba hizo nchi mnazoziona zikiwa juu kimaendeleo Duniani.

Hazikuanza kwa kuendekeza Demokrasia.

Afrika bila kusukumana mambo hayaendi.

Wengine kupiga kelele nako imegeuka ajira ya kujipatia kipato.

Lissu ni mmojawapo ya hao wanaoabudu kushitaki serikali kwa wazungu kwa kila jambo linaloihusu nchi hii.

Nadhani kama akipata urais, kila maamuzi yataamuliwa na wazungu kwanza.
 
D
Kama ipo mifumo imara kila kiongozi anawekewa mipaka yake katika utendaji kazi wake sio kwamba anaweza kuamuru chochote anachotaka kifanyike na akakubaliwa ! Lakini kwa katiba yetu hii iliyopo Rais amepewa madaraka makubwa sana ambayo hayahojiwi na taasisi yeyote ile ! Hapo ndipo matatizo yanapoanzia maana hakuna wa kumfunga speed governor !! Kwahiyo kwa katiba hii ya sasa iliyopo akipatikana Rais mkali ujue kweli watu wanaweza wakalimia meno !!
 
Tumeuziwa mabahewa ya mtumba, kiongozi anaona ufahari kwenda kutembeza bakuli ughaibuni
 
Huwa si support swalakatiba mpya sana, lakini jinsi alivyoliweka huyu mh. hapo namuunga mkono.
 
Kwani lazima amuone kulingana na hisia zako na mawazo yako..una akili huna jomba...kubali mawazo mbadala na hiyo ndio demokrasia
 
Ewe nguruwe Usitake kulazimisha kila mtu aone vitu jinsi unavyoona wewe.

Wewe kama unaona hayo wenzako wanaona mengine.

Kwani kina Anzory na kina Saanane ndio watu wa kwanza kupotea nchi hii?

Muache aone anavyoona yeye, wewe ona unavyoona wewe. Tusipangiane mitazamo.
 
Jamaa kaanza chokochoko naona kachoka kuwa Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Maana nafuatilia Ziara zake na Jussa wanampiga mawe Dkt Mwinyi kama wao hawako Serikalini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…