Othman Masoud wa ACT Wazalendo amfagilia Hayati Magufuli. Hii ina maana gani?

Othman Masoud wa ACT Wazalendo amfagilia Hayati Magufuli. Hii ina maana gani?

Kila mtu anatrend kwa Uzuri Na ubaya wake....Hitler alikuwa mtesi kwa mataifa mengine hasa wayahudi...Magufuli kafungua njia Watu kujitambua kama Akina Halima mdee na wenzake,ww huon kwamba hiyo ni hatua kwa Chama chenu cha Nyumbuzi peoples!!!?
Mi sio nyumbu ila jpm alikuwa fashisti na dikteta muuaji,Mungu fundi katuondolea balaa
 
Mmh.......
Hivi hakuona, namna watu wasiojulikana, walivyoshamiri Katika kipindi hicho cha Mwendazake?
Hivi hakuona namna Demokrasia, ilivyominywa Katika kipindi hicho?
Hivi hakuona namna watu, kama akina Saanane, Azory Gwanda nk, walivyopotea Katika kipindi hicho cha Magu?
Sasa inakuwaje Makamu Mwenyekiti huyo wa SUK wa Zenj, amuone Magu kuwa bora zaidi ya Mama?
Ao wasiojulikana walikuwepo kabla ya Magu na wataendelea kuwepo mpk kesho, Kuminya Demokrasia kwani sasahivi mmeipata? Watu mlikuwa mkifanya mikutano lazima usikie kuna mabomu hamelipuka au kifo cha mwandishi wa habari!

Tunaitaji fikra pevu katika taifa letu hasa la viongozi wetu wa kisiasa, tunaitaji watu ambao kweli wameshiba itikadi za vyama vyao na maslah ya nchi zao kuliko maslah yao binafsi.
 
Akihojiwa na mwandishi wa BBC kuhusu mchakato wa katiba mpya, mtaalamu huyo wa Sheria ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, kupitia ACT Wazalendo amesema kwenye utawala uliopita wa awamu ya 5 chini ya Magufuli tumejifunza kwamba kumbe tukipata mtu jasiri tunaweza kupiga hatua.

Na akashauri tunahitaji Katiba Mpya ili kuwajengea mifumo watu jasiri kama huyu ili haya aliyofanya yafanywe kimfumo na si kumtegemea mtu.

Sijui hii tafsiri yake nini kuhusu hiki chama.!
Sifa moja ya Mtanzania ni kumpenda sana Marehemu.
Halafu pia na kumsifia sana aliyestaafu.
Si unaona wengine wanamponda Samia, akimaliza muda wake watamsifia.
Ukiwa raisi wa TZ inabidi uwe kama JK hata usijali sana wanachosema maana hata wenyewe hatujielewi tunataka nini
 
Akihojiwa na mwandishi wa BBC kuhusu mchakato wa katiba mpya, mtaalamu huyo wa Sheria ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, kupitia ACT Wazalendo amesema kwenye utawala uliopita wa awamu ya 5 chini ya Magufuli tumejifunza kwamba kumbe tukipata mtu jasiri tunaweza kupiga hatua.

Na akashauri tunahitaji Katiba Mpya ili kuwajengea mifumo watu jasiri kama huyu ili haya aliyofanya yafanywe kimfumo na si kumtegemea mtu.

Sijui hii tafsiri yake nini kuhusu hiki chama.!
kipindi cha Magufuli angebwabwaja hayo anayoyaleta leo? Kulikuwa na SUK? Hana lingine zaidi ya chochoko hawazaoea amani, mioyo yao haina amani
 
Tafsiri yake ni kwamba hiki chama wanafikiri nje ya box ukilinganisha na kile chama kingine ambacho uwezo wao wa kufikiri ni kama hawa 👇View attachment 2281059
Na hawa jee?

1657089450657.png
 
Akihojiwa na mwandishi wa BBC kuhusu mchakato wa katiba mpya, mtaalamu huyo wa Sheria ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, kupitia ACT Wazalendo amesema kwenye utawala uliopita wa awamu ya 5 chini ya Magufuli tumejifunza kwamba kumbe tukipata mtu jasiri tunaweza kupiga hatua.

Na akashauri tunahitaji Katiba Mpya ili kuwajengea mifumo watu jasiri kama huyu ili haya aliyofanya yafanywe kimfumo na si kumtegemea mtu.

Sijui hii tafsiri yake nini kuhusu hiki chama.!
Amepata ulaji wa mbeleko chini ya Magufuri
 
Na inakupasa uelewe kwamba hizo nchi mnazoziona zikiwa juu kimaendeleo Duniani.

Hazikuanza kwa kuendekeza Demokrasia.

Afrika bila kusukumana mambo hayaendi.

Wengine kupiga kelele nako imegeuka ajira ya kujipatia kipato.

Lissu ni mmojawapo ya hao wanaoabudu kushitaki serikali kwa wazungu kwa kila jambo linaloihusu nchi hii.

Nadhani kama akipata urais, kila maamuzi yataamuliwa na wazungu kwanza.
Kwa nini mmeshindwa kumshughulikia kisheria badala yake mnataka kumuua kwa risasi.
 
Kama uliwahi kusoma neno kinyume kwahiyo mh Othmani hapo kaongea kinyume chake huyo ni mzanzibar na unawajua wa Zanzibar kwa mafumbo hilo ni fumbo lifumbue maaana utajua alicho kusudia

Huyu jamaa wala haelewi alichokuwa anasema Othman. Hapo ndio huwa ninajua kuwa watu wengi wana uwezo mdogo wa kuelewa mantiki ya mtu.
 
Na inakupasa uelewe kwamba hizo nchi mnazoziona zikiwa juu kimaendeleo Duniani.

Hazikuanza kwa kuendekeza Demokrasia.

Afrika bila kusukumana mambo hayaendi.

Wengine kupiga kelele nako imegeuka ajira ya kujipatia kipato.

Lissu ni mmojawapo ya hao wanaoabudu kushitaki serikali kwa wazungu kwa kila jambo linaloihusu nchi hii.

Nadhani kama akipata urais, kila maamuzi yataamuliwa na wazungu kwanza.
Kama kutokujali demokrasia ndio kunafanya uwe na maendeleo, basi Afrika ilipaswa kuwa yenye maendeleo makubwa, maana huku demokrasia ni ndogo sana.

Halafu inaonekana kwako serikali ndio nchi. Kuna tofauti kubwa sana kati ya nchi na serikali.
 
Back
Top Bottom