Tetesi: P Diddy ahusishwa na kifo cha Notorious B.I.G

Kwa mara nyingine unapotosha. Dre hakutakiwa kuwa shahidi kwenye kesi ya Snoop. Angetakiwa lazima angefika vinginevyo angefungwa kwa kosa la kutoitii mahakama (contempt of court). Alitegemewa kufika ili kumpa Snoop support kwa kuwa alikuwa mshikaji wake na ndio maana Tupac akamaindi.

Pia Dre hakuondoka Deathrow kwa sababu ulizotoa. Dre hakutaka kufanya kazi kwenye mazingira ya kitaa (gang banging environment) ambayo Suge aliyaendekeza kwenye lebo Deathrow. Dre hajawahi kuwa mtu wa kitaa na huwa anahitaji utulivu kwenye kazi zake. Uvumilivu ulimshinda baada ya rafiki zake kupigwa vibaya na Suge na goons wake baada ya kukutwa wakitumia simu ambayo ilikuwa maalum kwa ajili ya kuwasiliana na sponsor wa Deathrow Michael Harris aka Harry O ambaye alikuwa jela kipindi hicho. Akaamua kusepa.
 
Hii ya kukiri au kusema kwamba fulan ndio alikuwa shooter baada ya mtu huyo kufariki wala haileti maana.

Ukishafariki lolote unaweza kupakaziwa iwe kwa kusifiwa au kupondwa.

Kwahiyo asimuamini kwa asilimia 100 alichokiongea.
Nani kasema anaamini asilimia 100? Mimi nimem-quote alichosema. Halafu kwa nini unasema kwamba Keefe D anaweza kuwa anamsingizia Orlando wakati Orlando mwenyewe kabla hajafa aliwaambia washkaji zake wa Compton kwamba ndiye shooter?
 
Nani kasema anaamini asilimia 100? Mimi nimem-quote alichosema. Halafu kwa nini unasema kwamba Keefe D anaweza kuwa anamsingizia Orlando wakati Orlando mwenyewe kabla hajafa aliwaambia washkaji zake wa Compton kwamba ndiye shooter?
Pia wakati akiwa hai Orlando alikuwa na kazi ya kusafisha jina lake dhidi ya tuhuma za mauaji ya pac. Mwenyewe alikuwa anaogopa kuwa atamalizwa na yeye kwenye revenge. Tabia zake kbl ya kifo chake zilibadilika sana.

Kuna video moja niliiona yutube kuna mtaalamu mmoja hv mwanamama alikuwa anaifanyia analysis interview ya Orlando (video) ambapo anaulizwa umemuua tupac akakataa. Sasa yule mmaza (mtaalamu) akawa anaanalyse body language, facial expressions, na vitu vingine na kuconclude jamaa alikuwa anaongopa. Pia kwenye hiyo interview Orlando anaulizwa wakati Tupac anashambuliwa yeye alikuwa wapi akasema nyumbani. Nyumbani kwake ni Compton wakati siku hiyo alikuwa Vegas na ndio akashambuliwa na tupac na wahuni wengine wa deathrow na alifile mpk complaints. In short alijisahau kwa sababu alikuwa hasemi ukweli!!! Angalia video hiyo


Kwa story ya jamaa ilivyokuwa street hitter, genge alilokuwa, watu waliokuwa nyuma yake kina keefe D jumlisha na kutaka kulipa kisasi kwa kushambuliwa na Pac ni lzm itakuwa yeye ndio mhusika
 
Kwa maelezo haya basi 2pac na hao vijana wengine wote wa enzi zake walikuwa hawajastaarabika hata kidogo.... kwa superstaa mkubwa kama 2pac huwezi kujihusisha na upumbavu wa kwenda kunyang'ana cheni... walikuwa na upuuzi mwingi sana.
 
Kwa maelezo haya basi 2pac na hao vijana wengine wote wa enzi zake walikuwa hawajastaarabika hata kidogo.... kwa superstaa mkubwa kama 2pac huwezi kujihusisha na upumbavu wa kwenda kunyang'ana cheni... walikuwa na upuuzi mwingi sana.
Pac hakuwa anapenda dharau, ujinga au uonevu. Ukimuonea mtu mbele yake basi anachukulia kuwa umemuonea yeye, kwahiyo atakuvamia tu.
 
Nani kasema anaamini asilimia 100? Mimi nimem-quote alichosema. Halafu kwa nini unasema kwamba Keefe D anaweza kuwa anamsingizia Orlando wakati Orlando mwenyewe kabla hajafa aliwaambia washkaji zake wa Compton kwamba ndiye shooter?
Kabla Orlando hajafa aliwaambia washkaji zake 😂😂😂😂?
Je ulikuwepo wakati akiwaambia? Kama ulikuwepo tupe visibitisho.
Na kama haukuwepo una uthibitisho gani usiokuwa na shaka ambao utatufanya sisi tuamini kile walichokisema kuhusu Orlando?

Na maswali mawili ya mwisho je hayo maneno waliyasema baada ya Orlando kufa au akiwa hai?

Kama walizisema wakati Orlando akiwa hai, polisi walichukua hatua gani juu ya hicho walichosema kuhusu Orlando kuhusika na kifo cha Pac?

Na kama walizisema baada ya Orlando kufariki una uhakika gani kwamba ni kweli Orlando aliwaambia? Kama walikuwa wanatafuta kiki je, au haujui kama wasanii wengi hauishi kwa kiki haswa haswa kwa kutumia habari ambazo zitaleta ufuatiliaji katika jamii?

Ninachokushauri ndugu yangu, usipende kujiona kuwa wewe ndio uko sahihi kwa kila kitu. Hizi habari mimi na wewe tumezisoma tu kutoka kwa watu mbali mbali huko Marekani. Na kila mtu huja na maelezo yake haijalishi waliokuwa kwenye tukio au wasiokuwa kwenye tukio.
Ndio maana hadi leo wameshindwa kuwajua wauaji halisi wa 2pac na Big kwa sababu hata hao waliokuwepo kwenye matukio, pindi walipokuwa wanawahoji kwa nyakati tofauti tofauti kila mmoja alionekana kuja na maelezo ya kupishana na mungine aidha kwa kuogopa street code, au kutokumuona vizuri muuaji sura yake.

Sasa nashangaa wewe unataka kutulazimisha sisi tuamini kile unachoamini wewe hata kama pengine alieongea aliamua kutumia uwepo wake katika tukio au ukaribu wake na muuaji au 2pac na Big kuulisha matango pori ulimwengu ili kujitengenezea mazingira ya kufuatiliwa kupitia vifo hivyo.

Bwana mdogo Orlando afanye mauaji mahali ambapo kuna camera za barabarani, afu FBI, Polisi na vyombo vingine vya usalama vya taifa kubwa duniani kama Marekani kwa muda wa miaka miwili ya mwisho wa uhai wake vishindwe kumtambua! Labda uniambie kuwa mauaji hayo yalifanyika Burundi au Congo ambapo watu wanaweza kuuwawa kiholela bila wauaji kutambulika.

Na kama ni USA basi kunakuwa na mkono wa mamlaka. Ila bila hivyo sio rahisi kuuwa maeneo kama yale afu uendelee kudunda mtaani miaka miwili bila kukamatwa.
 
Hakuna anaekulazimisha kuamini. Kama unaamini kwamba Tupac aliuawa na FBI, CIA, KGB, Delta Force, Illuminati au yuko hai kama wengine wanavyoamini ni juu yako. Mi naongea kutokana na taarifa mbalimbali ambazo zina-corroborate na kuonyesha kwamba Orlando alihusika na mauaji hayo.

Wewe unayebisha una uthibitisho gani? Ulikuwepo? Kwa nini Keefe D amsingizie Orlando kama haikuwa kweli? Unajua kwamba Keefe D ni mjomba wa Orlando (mtoto wa dada yake)? Kwa nini amsingizie kuua kama hakufanya hivyo? Una uhakika sehemu aliyouawa Tupac kulikuwa na kamera? Ulikuwepo na uliziona?

Unapohoji kwamba kama Orlando aliwaambia washikaji zake kwa nini polisi hawakufanya kitu una maana gani? Hao polisi wangeota kwamba Oralndo amewaambia homies wake kwamba alikuwa shooter? Au washkaji zake Orlando ni polisi? Unajua street code za gangs? Au unategemea kwamba jamaa zake Orlando baada ya jamaa ku-brag kwamba amemshoot Pac wangeenda polisi kuripoti?

Tatizo hata nikikupa reference kuhusu hii ishu utasema huamini kwa kuwa hukuwepo. Halafu unaamini unachoamini wakati hukuwepo! Maajabu!
 
Siku anakufa September 7, 1996 kesho yake asubuhi September 8, 1996 natoka kuamka nafungua radio habari ya kwanza kuisikia ni hio kwa hio siwezi sahau
Hiyo ni siku aliyopigwa risasi kabla ya kufariki hospitalini siku sita baadae. Nilikuwa kwenye daladala asubuhi nikielekea shule, nikaisikia habari ya kupigwa kwake risasi kupitia Radio One.
 
Hiyo ni siju aliyopigwa risasi kabla ya kufariki hospitalini siju sita baadae. Nilikuwa kwenye daladala asubuhi nikielekea shule, nikaisikia habari ya kupigwa kwake risasi kuoitia Radio One.
Aisee mi nilishtuka kidogo maana tulikua tunamkubari by that time ndio ikawa ukumbusho Ila kashalala tayari, apumzike salama uko alipo
 
Imagine watu wapo kabisa wanamuamini na huu uharo alioandika. Wabongo bado sana yani.
 
Imagine watu wapo kabisa wanamuamini na huu uharo alioandika. Wabongo bado sana yani.
tafauti kati yangu mimi na wewe ni kwamba tupac na big walipouawa labda hata ulikuwa hujazaliwa kwa hivyo unasoma kwenye mitandao tu.

Sasa unakuja hapa na ujuaji wako - anyway hayo ni maoni yako
 
Dah!,style ile ile aiseee,sjawah isikia hii
Ndo ilivyokuwa mkuu, hapa nakuwekea picha ya kwenye mashambulio yao uone mazingira ya shambulio yanavyofanana.

Juu ni gari aliyokuwa amepanda 2pac

Na hizo zingine za chini ni gari aliyokuwa amepanda Big. Mashambulizi yote yalifanyika kwenye trafiki light.
Na chini picha ya wale madem waliomwita Big. Ambapo alipofungua dirisha tu akakumbana na risasi za kichwa kutoka kwenye gari iliyopaki ubavuni kwa gari yao. Hii ilikuwa hivyo hivyo kwa Pac pia.
 

Attachments

  • IMG-20230326-WA0008.jpg
    34.4 KB · Views: 10
  • IMG-20230326-WA0005.jpg
    35.2 KB · Views: 8
  • IMG-20230326-WA0005.jpg
    35.2 KB · Views: 8
  • IMG-20230326-WA0009.jpg
    44.4 KB · Views: 12
Mimi sina tatizo na ulichoandika maana sio wewe peke yako unaejiona unaijua vizuri ishu ya vifo vya 2pac na Big. Kuna watu wengi humu wanaojifanya wanaijua vyema ishu hii na mimi nimekuwa nikisoma tu na kuendelea na mjadala bila kuwapinga au kuwaonesha kuwa hawajui. Hii ni kwa sababu nafahamu katika mambo kama haya kila mtu ana aina yake ya upokeaji wa taarifa. Na haimaanishi kwamba kila taarifa zinazopokelewa ni za kweli.

Zipo za uongo kutoka kwa watu wa karibu na wahusika na zipo za kweli kutoka kwa watu wa mbali vile vile.

Kuwa mjomba au kaka wa 2pac, Big au Orlando haimaanishi kwamba mtu huyo kila atachoongea kuhusu muhusika ni cha kweli. Hii ni dunia ya kupigania tonge. Kwahiyo kuna mungine anaweza kutumia mazingira ya vifo hivyo kujipatia tonge.

Wewe unashangaa eti mjomba wake Orlando hawezi kumsingizia mpwa wake. Je wewe haujawahi kusikia mjomba anamfanyia ushenzi mpwa wake kwa sababu ya masilahi fulani.

Wewe unajua ni kiasi gani alichopata ili kuja kueleza ukweli au kupotosha taarifa za Orlando ilimradi mkono uingie kinywani? Je haujui kama toka miaka hiyo watu wengi walikuwa wanaishi kwa kiki mbali mbali zikiwemo hizi za kujifanya wanajua habari za kina 2pac na Big?

Sasa mimi sina tatizo na hilo, tatizo langu ni kujifanya kuniambia kuwa mimi napotosha ilihali kuwa hata na wewe haukuwa eneo la tukio, haukuwahi kuishi nao wote wawili na haukupata hata nafasi ya kuongea nae wewe mwenyewe mmoja wa wahusika wa Big, 2pac au Orlando.

Umeokoteza okoteza taarifa mbali mbali za kweli na uongo ukazileta humu na watu tuliona kama zipo kinyume na zile tunazofahamu na kuzielewa sisi ila tukaheshimu kile ulichoamini.

Sasa iweje na wewe usiheshimu kile walichoandika wenzako. Una mamlaka gani ya kukimbilia kumkosoa mwenzako kuwa kakosea ili hali hata wewe mwenyewe umesoma na kufuatilia hizi taarifa kupitia mitandaoni tu kama mimi na wachangiaji wengine!
 
Sipendagi jitu ongoongo alafu linajiamini kabisa. Ni hatari.
Kweli mkuu ndo maana kuna mwana anajifanya anajua kwa kuokoteza okoteza habari mitandaoni. Nimemchana live kwenye post namb #227.
Haiwezekani mtu mwenyew kaokota okota habari afu ajifanye anajua kila kitu zaidi ya kila mtu hapa JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…