Uvumi ni mwingi lakini mpaka recently imeshathibitishwa aliyemuua 2pac ni Orlando Anderson,yule jamaa aliyepigwa na 2pac mapema siku ile kwenye pambano la Tyson na Bruce Seldon.Na alikuwa mtu wake wa karibu.BIG alikufa sababu wapambe wa 2pac waliamini ye ndo alimuua.Kimsingi theories zipo nyingi Kuna hadi wanaoamini waliuawa na serikali ya marekani sababu ya bad influence Kwa vijana na makundi Yao ya east side na west side.Na Kuna wengine wanaoamini pia hakufa sababu hawakuona mazishi yake.
KWANINI TUPAC ALIMCHUKIA SANA BIGGIE MPAKA KUFA?
___________________
Watu wengi wamekuwa wakiniuliza maswali inbox, je, ni nini haswa kilisababisha ugomvi wa magwiji wawili duniani, Tupac Shakur na Notorious BIG kuchukiana mpaka kufa ?
Majibu ya swali hilo napenda niyaanzie mnamo February 13 mwaka 1993 wakati wamba hao wawili yaani Tupac na Biggie walipokutana kwa mara ya kwanza jijini Los Angeles.
Wakati huo Tupac tayari alikuwa ameshakuwa Staa wa filamu na muziki hivyo Biggie alitamani ukaribu naye kwa sababu naye alikuwa akiimba mtaani.
Kiroho safi, Tupac akamkaribisha Biggie nyumbani kwake na kisha wakala, kunywa na kuimba, huku wawili hao wakionekana kuzoeana kama walifahamiana muda mrefu.
Hata hivyo, Big alionekana kuhitaji msaada kwa Tupac wa kumshauri afanyaje ili naye aweze kuwa msanii mkubwa.? Tupac akamwambia Big "Usiwe na shaka, nitakusaidia".
Kwa mujibu wa Rapa wa kundi la Outlawz, E.D.I. Mean (Iddi Amini), anasema kuwa Tupac alitoa chupa ya Hennessy na kumpa Big kisha akawa anamsikiliza namna anavyorap.
Hata baada ya Tupac kutakiwa kutumbuiza kwenye tamasha la muziki huko Madison Square Garden, 'alimpa shavu' Big na kuweza kuimba naye pamoja.
Mara zote Tupac alitembea na Big kwenye Limousine, huku akimchukua kutumbuiza naye, japo Big alikuwa underground huku Tupac akiwa msanii mkubwa.
Wakiwa nyumbani, Tupac akamwambia Big, "Wacha leo nikupe siri hii.. kama unataka kupata pesa, hakikisha nyimbo zako huwaimbii Masela bali unawaimbia mademu".
Tupac akaendelea kumwambia Big kuwa, "Masela siku zote hupenda kuwanunulia mademu vitu wanavyotaka, hivyo mademu wakipenda kazi zako masela watawanunulia tu".
Big alikuwa makini sana kumsikiliza Tupac anachomshauri. Albamu yake ya kwanza ya 'Ready to Die' ikawa na kibao cha 'Big Poppa' kilichoonekana kupendwa mno na mademu.
Kabla ya Big kuachia albamu hiyo ya 'Ready to Die' alikuwa na wasiwasi wa kushindwa 'kutoboa' kutokana na record label iliyokuwa ikimsimamia ya Bad Boy Record kutokuwa maarufu.
Big akatoa pendekezo kwa Tupac kuomba kuwa meneja wake badala ya Sean Combs (Puff Daddy), lakini Tupac akamwambia "Hapana, fanya kazi na Puff Daddy, usimwache..ni mzuri...atakufanya kuwa Staa".
Big na Tupac wakaendelea kuwa washkaji wa karibu, walioshirikiana katika mambo mbalimbali ya muziki, wala haikuwepo dalili kama ipo siku watakuja kukorofishana.
Mapema mwaka 1994, Tupac akiwa jijini New York ku-shoot muvi ya 'Above the Rim' aliingia kwenye klabu moja na kumkuta jamaa flani akiwa kazungukwa na mademu huku meza yake ikichafuka kwa vinjwaji vya gharama.
Tupac akajikuta akishoboka kutaka kumjua jamaa huyo ni nani. Hakujua kumbe kijana huyo alikuwa mtu hatari sana pale Manhattan anayefahamika kwa jina la Jaques Agnant maarufu kama 'Haitian Jack'
Kando ya meza ya 'Haitian Jack' ilikuwepo chafu nyingine inayofahamika kwa jina la Jimmy Henchman. Big aliyekuwepo ndani ya klabu ile na Tupac, alishtushwa na Tupac kutaka ukaribu na watu wale.
Big akamwita Pac na kumwambia kuwa asithubutu kuhitaji ukaribu na Jack na Jimmy, lakini Tupac hakusikia na kuendeleza ukaribu na watu wale aliokutana nao klabu juu juu bila kuwajua vizuri.
Big alimtahadharisha Tupac kuhusu kutokuwa na ukaribu na Jack 'Haitian' na Jimmy, kwa sababu watu hao ni hatari na wangeweza kutumia fursa ya ukaribu wao na Tupac kujipatia pesa hata kwa njia za hatari.
Hata hiyo, siku iliyofuata Tupac na Jack wakakutana kwenye baa moja maarufu iitwayo Queens. Ndani ya baa hiyo walikuwapo wanamuziki mastaa Lady Madonna, Shaba Ranks na Buju Banton nao wakipata kilaji.
Itaendelea........[emoji3578]
#Balozi